Kama Kuna Ulazima kitangaza TPA CNN, basi tungetangaza kwenye masoko ya Asia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Wadadavuaji mnisaidie,hivi Kuna Tija ipi kulipia mamilioni kutangaza TPA huko CNN?

Ipi ingekuwa Bora kutangaza Utalii au Bandari?

Mwisho kama Kuna ulazima wa.kuitangaza Bandari yetu Kwa nini tusitangaze kwenye masoko ya Asia eg India, China, Thailand ,Vietnam,Arabs nk ambako ndio tunafanya nao biashara Zaidi?
---

TPA YAANZA KUJITANGAZA CNN
Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) imeanza kujitangaza kibiashara kwenye channeli mbalimbali za Television za Kimataifa ndani ya DStv ambapo tayari matangazo yake ya kwanza kwenye mpango huo wa kuliteka soko la Afrika Mashariki na Kusini yameanza kuonekana kupitia CNN.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka hiyo Dr. George Fasha amesema kabla ya hapo ilizoeleka kuona matangazo ya Nchi nyingine tunazoamini ziko mbele kimaendeleo zikinadi biashara zao kupitia Television kubwa za kimataifa na sasa Tanzania imetinga ili kuvutia zaidi biashara za kimataifa kwa ukanda huo na kulikamata soko.

“Taasisi yoyote inayodhamiria kufanya biashara kimataifa lazima ijizatiti kwa viwango vya kimataifa na ijitangaze kwenye anga za kimataifa, tumedhamiria kulikamata soko la Afrika Mashariki na Kusini pamoja na Wafanyabiashara kutoka dunia nzima wanaotaka kuingia kwenye soko hili, huu ni mwanzo tu kuna makubwa yanafuata” amesema Dr. George Fasha.

My Take
Hizi move zingine Zina harufu ya maokoto
 
Nchi ya beki tatu wa Waarabu hii kila mtoto anaamua afanye la kwake. Baba hayupo na aliyetakiwa kuwa mama kaamua awe beki tatu wa wajomba zake.

Ndio hapo unagundua hawa wasomi maandazi wanatutia hasara sana, bora wasiosoma huwa wanabeba magunia ya viazi sokoni.

Hao TPA kila siku naona ads zao mtandaoni wanaanza na kumtaja Samia. Something like "in the leadership of President Samia Suluhu Hassan, the Tanzania Po..." pumbaf kabisa kwani mmiliki wa shipping line ana haja ya kujua Rais wa nchi ni nani ili atumie bandari?

Hao vigagula wa TPA ni maandazi hata kuandaa tangazo hawawezi, tangazo utadhani limetolewa na sekretarieti ya CCM.

Badala wataje mambo ya msingi kama handling capacity, nchi gani zinategemea bandari yetu, connection na reli, future plans za kupanua, kujenga gati mpya au kuongeza kina wao wanatanguliza siasa.

Sasa maandazi hayo hayo ndio yamepeleka tangazo la bandari CNN. Ukute nalo litamtaja Samia na likose pointi muhimu.
 
Wadadavuaji mnisaidie,hivi Kuna Tija ipi kulipia mamilioni kutangaza TPA huko CNN?

Ipi ingekuwa Bora kutangaza Utalii au Bandari?

Mwisho kama Kuna ulazima wa.kuitangaza Bandari yetu Kwa nini tusitangaze kwenye masoko ya Asia eg India, China, Thailand ,Vietnam,Arabs nk ambako ndio tunafanya nao biashara Zaidi?

My Take
Hizi move zingine Zina harufu ya upigaji ziangaliwe Kwa jicho la utofauti.

Ushauri wako tunaufanyia kaz ngoja kwanza tupige hili dili chaaap!!!
 
Kuna shida gani kutangaza TPA CNN? Lengo nikuifikia East Africa na nchi zote za kusini mwa jangwa la Sahara, ebu mleta taarifa tuambie TV gani inaweza tumika hapo? Inayoweza fikia nchi zaidi ya 10 za kusini mwa Afrika?

Tatizo kwa akili yako ndogo unajua CNN wanalenga watazamaji wa marekani wanalenga nchi za sub Sahara

Lakini pia hata kama ni Marekani na kwingine kuna makampuni makubwa huko yanafanya biashara na nchi za Afrika. Kwaio kuwaonesha TPA ni sawa, kwakuwa wanaweza opt Dar es salaam kwa biashara na mizigo yao

Na kumbuka ni CNN chanel (DSTV) kwahio walengwa ni waafrika
 
Soma mada kwanza ndio uje ku comment kabla sijakudhalilisha
 
Back
Top Bottom