Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,071
Rais wa chama cha soka hapa Tanzania (TFF), Wallace Karia siku za karibuni amesikika akitoa matamshi yenye utata kwa kusema kwa kipindi kirefu akiwa Rais wa TFF, yeye na TFF kwa ujumla wake kwa makusudi wamekuwa wakiibeba sana Yanga kwenye ligi kuu ya Tanzania na kwa sasa wamechoka kuendelea na huo mtindo, hivyo Yanga waanze kujipambania wenyewe badala ya kusubiri kuendelea kubebwa na TFF.
Matamshi hayo yamestua na kuwashangaza sana wadau wa soka ndani na nje ya Tanzania kwa kuwa hayakutegemewa kusikika tena kutoka kwa kiongozi wa juu wa shirikisho la soka la Tanzania, taifa lenye ligi inayosemwa kuwa ndani ya ligi tano bora zaidi hapa Afrika, likijiandaa (kwa ushirikiano na nchi za Kenya, Uganda, Tanzania) kuandaa mashindano ya CHAN mwaka huu na AFCON mwaka 2027, huku ikiwa ndio ligi iliyosheheni wachezaji wengi zaidi wa kimataifa katika ukanda wa afrika mashariki na ikitajwa ligi yenye udhamini mkubwa, mpana na uhakika katika ukanda huo.
Bila kujali matamshi hayo yana ukweli, uongo au utani kiasi gani, lakini kwa uzito wake na kwa nafasi aliyonayo mtu aliyeyatoa (yaani rais wa TFF), ni vyema hatua hizi zikakuchukuliwa mara moja;
1. Karia apigiwe kelele na wadau wote wa soka ili ajiuzuru ama asimamishwe kwa lazima nafasi aliyonayo sasa kama rais wa TFF na mjumbe wa FIFA, CAF, CECAFA nk.
2. Matamshi yake yachunguzwe kwa kina na mamlaka husika ili hatua stahiki za kinidhani kwenye soka zichukuliwe kwa wahusika wote.
3. Ashtakiwe na wadau wa soka (kama wadhamini), taasisi (kama vilabu) au mamlaka za kisoka zilizoathirika na matamshi au matendo yake kuhusiana na hilo.