Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

Unamfahamu vipi huyu tajiri wa Kilimanjaro express??

Hivi hizo gari bado zipo?

Huyu jamaa ni R. Sawaya!! Ana garage yake kitambo sana majengo kama unaenda kwa Mtei pale, enzi hizooo hakuna english medium

Alianza na vicosta vya kwenda Rombo na Marangu enzi hizooo viliitwa Neema!!

Baadae akaadvance akaanza na basi kubwa kutoka mkoa hadi mkoa akabadili jina zikaitwa Sawaya ambalo ni jina lake la ukoo!!

Basi la Sawaya miaka ya 90 lilipata ajali kubwa sana likau watu wengi na kabla ya hapo alikuwa na viajali vidogo vidogo so baada ya hiyo ajali kubwa akabadili jina akaita Kilimanjaro zilikuwa na rangi ya Kijani mgomba na nyuma alipaka kama nyeusi hivi zilitalakaa sana mpaka Mbeya, Singida zilifika!!

Baadae akayauza yote hasa baada ya kupata kashfa ya wizi wa matairi, akaja na mfumo huu wa basi chache mpya na Luxury!! Ambao kwa namna moja au nyingi amepiga bao la hatariii
 
Thats TRUE
 
Kuna yule jamaa wa pale moshi karibu na stendi anayejenga ghorofa kwa awamu na ana mgahawa mkubwa kwa pembeni ni nani? Na buffalo je? Bila kumsahau huyu mwenye Aquline hotel Arusha,wazee wengi wa kichaga waliupatia utajiri kenya,sikujua kenya kuna siri gani ila ndo naanza kung'amua
 
Je wadhani matajiri hawafanyi kazi?
Hata utoaji kafara ni kazi!
Na ujue kamwe hakuna tajiri atakayekupa siri ya utajiri wake, sembuse wewe hata mshahara wako unaficha kwa mkeo!
 
nani huyo mkuu ni kawa nini kipande kimoja cha baba kilikuwa na duka usawa wa baa ya makando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…