Mataifa yenye wanafunzi werevu zaidi duniani

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,654
48,432
Katika kutathmini viwango vya elimu duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?

Jambo la kushangaza ni kwamba orodha hii inaonyesha taswira tofauti sana na ile inayotolewa na utathmini wa vyuo vikuu.

Shirika la Kimataifa la Uchumi na Maendeleo (OECD) limefanya wazi matokeo ya mtihani wa kupima uwezo wa wanafunzi wanaohitimu kutoka nchi mbalimbali.

Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka Marekani na Uingereza kama vile Harvard, MIT, Stanford, Oxford, Cambridge na UCL.

Lakini baada ya OECD kuchunguza uwezo wa kusoma na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu, wanafunzi walio bora zaidi ilibainika wanatoka Japan na Finland na wala si Marekani na Uingereza..

Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanaohitimu kwa mujibu wa OECD

  1. Japan
  2. Finland
  3. Uholanzi
  4. Australia
  5. Norway
  6. Ubelgiji
  7. New Zealand
  8. England
  9. Marekani
  10. Jamhuri ya Czech
Nchi hizi zote huwa mara nyingi hazina chuo haka kimoja kinachokuwa kwenye orodha ya vyuo vikuu 10 bora duniani.

Badala ya vyuo vikuu vya Marekani kufana, yamkini vyuo vikuu vya Norway na Australia vina wanafunzi bora wanaohitimu.

Kwa mujibu wa orodha ya ubora wa vyuo ya QS World University Rankings, kulikuwa na vyuo 32 vya Marekani katika 100 bora, na chuo kikuu kimoja pekee kutoka New Zealand.

Lakini ripoti ya OECD inaonesha wanafunzi wa New Zealand wanafanya vyema kushinda wenzao Marekani.

Orodha ya ubora wa vyuo vikuu ya QS 2016-17

  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford University
  3. Harvard University
  4. University of Cambridge
  5. California Institute of Technology (Caltech)
  6. University of Oxford
  7. University College London
  8. ETH Zurich
  9. Imperial College London
  10. University of Chicago
Mataifa yenye wanafunzi werevu zaidi duniani - BBC Swahili
 
na sisi tungetumia kiswahili hadi chuo kikuu tungetoa wanafunzi bora sana. mwanafunzi hawezi kuwa mwerevu kama haelewi vizuri lugha anayojifunzia.

Mkuu uko hujakosea.
Mwanazuoni Noam Chomsky alishawahi kusema mtoto ataelewa sana endapo atajifunza kwa kutumia lugha yake mama. Na hili hata UNESCO kwenye ripoti yao ya mwaka 2000 walilikubali kabisa wakashauri nchi za ulimwengu wa tatu zifanye hivyo lakini walipiga gitaa kwa mbuzi.

Ukisoma mjadala wa mwaka 1984-85 baina ya akina Makweta na Nyerere juu ya matumizi ya lugha ya kiswahili kufundishia utapata ukakasi. Mambo yalipelekwa sana kisiasa, kuna wasomi wakubwa nchini walidiriki hadi kusema kuwa Kiswahili hakijitoshelezi na Kiingereza ndiyo lugha ya maendeleo.

Inafika kipindi mtoto haelewi kitu darasani.
Hajui hata kusema ahsante kwa kiingereza wanajuga tu maneno I LOVE YOU.
Mbaya zaidi hata kiswahili nacho hakijui vizuri, kifupi hali ni mbaya sana.

na tatizo ni kubwa zaidi kwa sababu hata walimu hawaielewi vizuri lugha wanayoitumia kufundishia.
 
na tatizo ni kubwa zaidi kwa sababu hata walimu hawaielewi vizuri lugha wanayoitumia kufundishia.

Acha tu mkuu.
Ila mbali na lugha hata nidhamu ya taaluma imekufa hapa nchini kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu.
Hebu pitia hii ripoti ya World Bank uone jinsi gani nchi za wenzetu wanamaanisha biashara kwenye elimu.
 
Attachments

  • Altbach_Salmi_2011_The_Road_to_Academic_Excellence.pdf
    2.5 MB · Views: 43
Mkuu uko hujakosea.
Mwanazuoni Noam Chomsky alishawahi kusema mtoto ataelewa sana endapo atajifunza kwa kutumia lugha yake mama. Na hili hata UNESCO kwenye ripoti yao ya mwaka 2000 walilikubali kabisa wakashauri nchi za ulimwengu wa tatu zifanye hivyo lakini walipiga gitaa kwa mbuzi.

Ukisoma mjadala wa mwaka 1984-85 baina ya akina Makweta na Nyerere juu ya matumizi ya lugha ya kiswahili kufundishia utapata ukakasi. Mambo yalipelekwa sana kisiasa, kuna wasomi wakubwa nchini walidiriki hadi kusema kuwa Kiswahili hakijitoshelezi na Kiingereza ndiyo lugha ya maendeleo.
cha kusikitisha ni kwamba hadi leo kuna wasomi wanatetea matumizi ya lugha za kigeni kwenye kujifunzia.
 
Si elimu yetu imekaa kisiasa mno
Hatuwez endelea kwa mtindo huu

Mkuu hebu tufanye tathmini kidogo.
Suala la elimu Tanzania tulikosea wapi?
Mbona miaka ya 85 kurudi nyuma wasomi walikuwa wachache lakini wenye uwezo mkubwa sana? Wahitimu wa mlimani walikuwa wanajiweza kweli kweli lakini kuanzia utawala wa Mwinyi mambo yalikuwa bora liende tu.
 
tunaamini kuwa elimu bora ni matokeo ya maendeleo wakati kiuekweli maendeleo (endelevu) ndiyo matokeo ya elimu bora.
Lazima kama taifa tujitathimi wapi tuli jikwaa
Umenikumbusha USA wameshuka kila sku nao wanataka kuwa kama sisi
Ila wanaongoza kuwa taifa linalo spend hela nyingi kwenye kuhudumia wafungwa
 
cha kusikitisha ni kwamba hadi leo kuna wasomi wanatetea matumizi ya lugha za kigeni kwenye kujifunzia.
Mkuu we vepe! Hao ndio walitetea kiswahili hadi kikawatokea puani kwa upuuzi Wa maendeleo tuliyonayo ni sawa na wajinga Duka hivi... Sisi sio Wa kuigwa Bali ni Wa kuiga milele.. Na huu upuuzi tunaoendelea nao tutabaki hivi milele nashauli kiswahili kifutwe mashuleni tulipo ndio matokeo yake
 
Back
Top Bottom