Maswali yalioninyima usingizi nilipokua mtoto

Mi nlikua najiuliza mtu akituma hela mpesa inamfikia je mtu mwingine aliye mbali ile hela inapita wapi yani we acha tu.
 

Ha ha ha ha ha hahhahahaahhahahahhahahahahaahahahhahahaha..iliwahi nitokea hii mwanzoni miaka ya 2000 ile midege ya jeshi..dahh
 

Hahahahah kweli utoto raha sana
 
haya magari yamenisumbua sana
1. dereva anawezaje kuwasha indicator huku akiendesha gari (washa zima washa zima)
2. utakuta home umeme umekatika alaf linapita gari na taa zake zinawaka.
 
Nilikuwa nawaza sana nikisikia mtu amekula hela,,
najiuliza amekulaje zile noti au sarafu? Anazitafuna?
 

hizo ni fikra potofu mabikra 72?? Pasua kichwa kweli kweli
 
nilikuwa najua shetani ana sura mbaya..nikiambiwa shetani uyo anakuja nalia natoka nduki then najificha!

Hapo kwenye "shetani" replace na sindbadi, home palikuwa hapatoshi ikibidi na msosi nasamehe kabisa. Nilikuwa namuogopa sindbadi aibuuuuu!!!!
We acha tu.
 
Mi mwanangu wa miaka 5 huwa ananiuliza 'hivi baba na wewe ulikuwaga mtoto kama mimi',basi nikamuonyesha picha yangu nilivyokuwa mtoto kabla sijaanza hata kutambaa lakini nakaa,alitoa macho kwa mshangao sana,sasa huwa najiliza hivi yeye huwa ananichukuliaje,kwamba nilizuka tu kama mzuka au la
 

Wewe lazima ulikuwa kipanga!!
 

Hako ka picha ka daslam wengi kanawachanganya. Hii hadi watu wazima ndivyo wanavyofikiri.
 
nikiwa darasa la tatu mama akiwa amekaa na wamama wenzie nilimsikia akisema siku hizi wanatumia MIPIRA kuzuia UKIMWI. baada ya mama kugundua kuwa niko eneo hilo alinifukuza nakunifokea kwa nini nasikiliza maongeza ya watu wazima. Nilipotoka hapo nilijiuliza saaaaaana, hiyo mipira wanayotumia kuzuia ukimwi ni ipi, ni kama hizi za manati tunayotumia kuwindia ndege? ni mipira/mirija inayotumiwa hospitalini, au ni mipira yaani kama mpira wa miguu(football) yaani gozi tunalosakata kabumbu. hilo swali lilinitesa sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…