Maswali yalioninyima usingizi nilipokua mtoto

Maswali yalioninyima usingizi nilipokua mtoto

aisee nakumbuka ilikua 1992 new yr,sasa kanisan wanashangalia karibu mwaka mpya mi nakodoa jicho mlangon nione dah haikuishia hapo baada ya mkesha watu wanapga debe wanakmbia mi nimebebwa mabegan na baba nikawa najiulza sn huo mwaka mpya uko wap!?
 
Kuna baadhi ya mambo yalinifanya niumize akili enzi za uto to
1- mtu akivaa overall (kanyela mumo) anakunyaje?
2-mama akienda kujifungua, je mototo hupitia wapi kutoka tumboni?
3-baba na mama, walizalia pamoja?
4-mwalimu ndie mtu mwenye akili kuliko watu wote?
5-rais ndie mwenye nchi?

Ongezea maswali yalio kutatiza utoton

Wanaoendesha magari walizaliwa humohumo?
Kwa nini usukani wa gari usikae katikati ili mwendeshaji aweze kubalance kulia na kushoto?
 
1. Nilikuwa nikiangalia juu usiku jinsi nyota zilivyo nyingi nilikuwa najiuliza, "Hii yote inaishia wapi?".
2. Hivi ukiweka mafuta kwenye gari yanafanya nini mpaka gari linatembea? Kwanini tusiweke tu maji, actually I had a dream of making cars that use water instead of petrol.... usiniulize imeishia wapi

Haya ndio maswali machache yaliyonifanya nipende sana science....

3. Huyu Mungu tunayemwomba kila siku ni mkubwa kiasi gani na anapata wapi uwezo wote huo, tunamwomba tukienda kutafuta, tunashukuru tukipata, tunaomba kabla ya kula, kulala halafu tukiamka tunashukuru!!! Huyu Mungu ni nani hasa?

-- Maswali mengi nilikuwa nabaki nayo tu maana ningeitwa mpinga mkristo
 
Nilikuwa najua ukimuona zeruzeru lazima uzae zeruzeru labda ujitemee mate kifuani. 2. Ukikojoa lazima uteme mate la sivyo unakufa
 
hii threads z the best....yan unajua utoton tunakuwaga na maswali kbao yanabaki kutuumiza kichwa tu.
......nakumbuka sijaanza chekechea basi naachwa nyumban na mdogo wangu mimuangalie, mama angu na dada na kaka walienda shamba.....sasa ikapita ndege inapima sijui madini au inafanya maping na kakifaa fulan kananing'ia chini...jaman nilikimbia kama kichaaa kwan nilijua ule ndo mwisho wa dunia...nikawa najiuliza hii ndege hapa kijijin imetokea wapi? afu kwa nn inaenda hadi milima ya kule inarudi hadi upande mwingne....nikajua hii inanitafta mm inazuga tu.aliniokoa baba wa jiran huko njian akanishikilia had wazazi walivorudi.
mh nimecheka hadi nimetoa machozi
 
Kuna baadhi ya mambo yalinifanya niumize akili enzi za uto to
1- mtu akivaa overall (kanyela mumo) anakunyaje?
2-mama akienda kujifungua, je mototo hupitia wapi kutoka tumboni?
3-baba na mama, walizalia pamoja?
4-mwalimu ndie mtu mwenye akili kuliko watu wote?
5-rais ndie mwenye nchi?

Ongezea maswali yalio kutatiza utoton

ndiyo maana africa hatuendelei, duh..sasa kwa mawazo hayo lini tutavumbua ndege, simu, gari na vifaa vingine muhimu
 
nilikuwa najua tunapotoa sadaka kanisani baadae zinapaa kwenda kwa mungu

Hata mimi msikitini nilijua hizo hela zinawekwa sehemu katika msikiti then kesho wanakuta Mungu keshachukua.
Jamani utoto!
 
Eti wakubwa walivyokuwa wakisema fulani amekula hela zangu. Nilikuwa najiuliza mtu anakulaje hela? Hazimwumizi?

Basi nabaki naishia kuumia tu moyoni
 
Nilikuwa najua ukimuona zeruzeru lazima uzae zeruzeru labda ujitemee mate kifuani. 2. Ukikojoa lazima uteme mate la sivyo unakufa

Hili la zeruzeru hata mimi lilinisumbua sana, kuna siku nilikuwa natoka shule, mbele yangu akawa anakuja zeruzeru, kilichofata hapo hadi namaliza kupishana na huyo binadamu mwenzangu, kifua chote kimelowa mate kwa ndani!!!
 
kwa nini mtu akiendesha baiskeri aangalie mbele, badala ya kuangalia chini ili ajue kinachoendelea hapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom