Kutakuwa na kufanana kwa imani hizi za utotoni kutoka sehemu moja hadi nyingine, nikiwa mdogo nilikuwa naamini watoto wananunuliwa dukani na pia niliambiwa Shetani anaishi mtoni kwenye migomba flani ambayo haitoi ndizi na kwenye magimbi basi nikawa naogopa kupita maeneo hayo kwa kumwogopa Shetani, nilikuwa naambiwa kwamba MVUA ikiwa inanyesha na RADI inapiga huku JUA likiwaka basi hapo Shetani anampiga mke wake mateke nikaamini hivyo mpaka darasa la tatu, nikawa naona watu wengi wakipiga wake zao mara kwa mara huku nikishuhudia kwa nadra hili suala la Mvua, Radi na Jua nikawa najiuliza, mbona Shetani anapiga mke wake mara moja moja lakini majirani zetu wanapiga wake zao karibia kila siku? Na huku naambiwa Shetani ni mbaya? Tena nilikuwa naamini Shetani ni jitu jeusi halafu Mungu ni mzungu kumbe ni utoto na mafundisho potofu kutoka kwa jamii inayonizunguka, lakini leo siangalii hata hizi filamu zinazoitwa za Yesu maana ni fiksi tu na brainwash