Maswali yalioninyima usingizi nilipokua mtoto

Maswali yalioninyima usingizi nilipokua mtoto

Kwa nini jambazi wa kwenye video anakufa halafu nikiangalia kanda ile ile siku nyingine anakuwa hai.
 
Nilikua na anko wangu anaitwa Anord basi nilikua najua anapiga kama yule wa kwenye video.

Nikizinguliwa tu nawaambia naenda kusema kwa mjomba Anord na walikua wanaogopa kweli!
 
Nilijua ukigegeda basi mimba inatokea palepale.

Nilipokua la pili nikagegeda demu halafu nikaangalia tumbo kama mimba ishakua tayari.
 
Nakumbuka siku niliyoota vuzi nikafikiri nina cancer! sababu bibi alininunulia suruali ya mtumba nilivovaa sikuvua hadi usiku. Nilikua naambiwa vua hio suruali tufue nagoma, kufika usiku nakuta kanywele kameota! Dah! Nikajua ni madhara ya ile nguo ya mtumba!

kumbe kuota zivu ni process ya siku moja! Hongera sana.
 
1. mim nilikuwa najua sterring wa movie ni jamaa mmoja tu na anapiga dunia nzima.
2. kwa nini betrii za redio imeandikwa NATIONAL alafu wakubwa wananilazimisha kuiita NESHNO wakati hakuna S kwenye neno NATIONAL.
3. tulipofundishwa mambo ya uzazi shule ya msingi, nilijua kupiga Bao ni mtu anapopush uume wakati wa kufanya mapenzi. AKifanya mara sitini basi jamaa atakuwa kapiga mabao sitini.
4. hakuna mzungu, mwarabu, mchina wala muhindi anayeweza kumpiga au kumtoa damu mtu mweusi, eti sisi tumekomaa sana.

utoto kazi kweli kweli
 
Nilijua ukigegeda basi mimba inatokea palepale.

Nilipokua la pili nikagegeda demu halafu nikaangalia tumbo kama mimba ishakua tayari.

Wewe kweli kiboko la pili ushajua kugegeda na umefanya na majaribio. ..heheheheh ...
 
Nilikua najua haya magari madogo yanayofanya taxi yana usukani mbele na nyuma.
 
hii threads z the best....yan unajua utoton tunakuwaga na maswali kbao yanabaki kutuumiza kichwa tu.
......nakumbuka sijaanza chekechea basi naachwa nyumban na mdogo wangu mimuangalie, mama angu na dada na kaka walienda shamba.....sasa ikapita ndege inapima sijui madini au inafanya maping na kakifaa fulan kananing'ia chini...jaman nilikimbia kama kichaaa kwan nilijua ule ndo mwisho wa dunia...nikawa najiuliza hii ndege hapa kijijin imetokea wapi? afu kwa nn inaenda hadi milima ya kule inarudi hadi upande mwingne....nikajua hii inanitafta mm inazuga tu.aliniokoa baba wa jiran huko njian akanishikilia had wazazi walivorudi.

Hahahahahahahahaha!
 
  1. mimi nilikuwa nikiwaskia big boys wakizungumzia kumkojole msichana, nilikuwa nadhani mkojo huu huu wa kawaida! sasa nikawa najiuliza msichana akishakojolewa, tena kwa wingi wa mkojo, huwa unaenda wapi? matakoni ama tumboni!
  2. mimi nilikuwa naamini, tukisafiri ile miti nayo inasafiri kwa kurudi nyuma!

Kwahiyo swali no.1 umelipatia jibu lake uniambie na mimi manake hata mimi najiuliza swali kama hilo ila babo sijapata majibu yake
 
Utoto shida...!!!
Tukiona watu wamebeba maiti, Mungu wangu mbio zilikuwa mpaka uvunguni!!!!!
Wakikamata mwizi... mapema sana nyumban, & usingz hakuna.
 
hizi shule zetu za kayumba balaa. hakuna neno lililokuwa linaniumiza kichwa kama "always". madaftar yang kaka angu pale kwny date alikua ananiandikia "always change" afu shuleni "always" nafundishwa vingine. sasa ikifika usiku tunaangalia tv likapita tangazo la always (pedi) walillokua wadhamin wa muvi ya lorenzo lamas (rhino) ndo navurugika kabisaaaaa.
 
1. nlikua nkimeza mbegu ya tunda lolote sinywi maji naogopa kuimwagilia isije ikaota.
2. nlishamtia mama hasara sana kwny dagaa, nlikua nawaonea huruma sana. Bas ilikuwa akiweka kweny ungo mi nawachota naenda wamwaga kisimani ili wakue
 
Mimi kilichonipa utata ni hichi hapa na mpaka leo bado nashangaa tu.

Sensual Paradise[ edit ]
In Islam, the concept of
72 virgins (houri) refers
to an aspect of Jannah
(Paradise). This concept
is grounded in Qur'anic
text which describe a
sensual Paradise where
believing men are
rewarded by being wed
[1] to virgins with "full
grown", "swelling" or
"pears-shaped" breasts.
[2][3] Conversly, women
will be provided with
only one man, and they
"will be satisfied with
him".
 
Niliamini kuwa kitu kikipotea unatema mate kwenye kiganja cha kushoto unayachapa na vidole viwili vya kulia yatakakoelekea ndiko hicho kitu kilopo.2 Mdudu akiingia machoni unatema mate juu mara tatu au nne na mdudu anatoka,kweli utoto raha.

wewe lazima ni Mrangi wa Kolowasi
 
Neno Jesus.... Nilijua ni mtu mkatili sana coz nilisoma lilivyoandikwa ie."Jesusi".
 
Anko wangu aliwahi kuniambia kuna wakati huwa inanyesha mvua ya M. A. V. I ,Basi ikawa nikiona mawingu tu mimi mbio uvunguni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom