Maswali ya wazi kwa Mh Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali ya wazi kwa Mh Zitto Kabwe

Discussion in 'Great Thinkers' started by Fitinamwiko, Sep 5, 2012.

 1. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mh Zitto naomba utufafanulie sisi wana JF, ushirikiano wako na serikali ya CCM. Tunajua siasa si uadui lakini ndani ya CCM kuna ushahidi wa kutosha kuwa siasa ni uadui. Mfano, Kuna uthibitisho wa makundi ndani ya CCM kuwekeana sumu na juzijuzi tuu imeriportiwa baadhi yao kutishiana kwa mitutu ya bunduki. Pia tumeona serikali ya CCM kwa kushirikiana na vyombo ya dola kuzuia harakati za chama chako cha CDM kuwakomboa wananchi. Tumeona jinsi maisha yakipotea ktk chaguzi mbili ndogo za Igunga na Arumeru.

  Dini yangu inanikataza kudhani, hivyo nakuomba utuwekee wazi Faida zako kisiasa binafsi na kichama (CDM) unazopata kwa kushirikiana na Serikali ya CCM. Ikizingatiwa, ndani ya CCM kuna makundi ambayo yanakigawa chama chao na kuelekea Kaburini soon or later. Pia tunajua Mh unayeambatana nae ktk safari za nje ni muhasisi wa siasa za kuchafuana (2005 Salim Ahmed na Mwandosya) na makundi ambayo yameleta matabaka ndani ya CCM kwa walionacho(Mafisadi) na wasionacho.

  Mh Zitto kama sikosei wewe ni Mbunge wa Kwanza kufukuzwa Bungeni baada ya kuibua kashfa dhidi ya serikali ya CCM. Pia Mh Zitto ni wewe uliyeanzisha mchakato wa kutaka kumuondoa madarakani Mh Pinda (vote of no confidence) ambayo ilimcost JK kuvunja Balaza lake la mawaziri. Mh Zitto umewapa serikali ya CCM ultimatum kuwataja vigogo walioficha pesa Swizz.

  Mambo haya yote si ya kupendeza ndani ya serikali ya CCM ambayo mkuu wake ndiye uliyeambatana nae kwenda Ethiopia. Wote tunajua Mheshimiwa hapendi kukosolewa na constructive criticism kweke ni uadui. Mh Zitto imekuwaje wewe umekuwa kipenzi wake, what is behind the curtain?

  Sasa tunaomba bila ya kumung'unya wala kumeza weka kila kitu wazi sisi wana JF tuelewe ukweli wa wasiwasi wetu.
   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kwa uelewa wangu mdogo wa mambo ya kisiasa na kwa jinsi ninavyomfahamu Zitto akiwa bado UDSM, sitegemei kupata jibu lolote la maswali yako. Hivyo niwaombe tu ndugu mwenye ID ya hutaki unaacha na dévil watusaidie majibu ya maswali haya, kwani siyo wewe tu ambaye muenendo wa Zitto unakupa shida, bali ni watu wengi sana hatuna imani na ndugu Zitto.
   
 3. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Mimi nadhani ukweli ni kwamba: Zitto amekuwa mwiba sana kwa serikali. Walipotaka kumpoteza kwa kumuadhibu viadhabu vya hapa na pale walijikuta ndio kwanza wanamjengea umaarufu. sasa kama wasemavyo waingeleza " I you can't fight them, join them", wameamua kummaliza kwa plan B ambayo ni kuungana naye na kumpenda sana. Nilihisi Zitto kaingia kingi lakini siku zinavyoenda na mambo yanavyokwenda nagundua kuwa Z ni mjanja sana kuliko Serikali wanavyodhani. Huo ni mtazamo tu
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tukisikia majibu yake itakuwa ni vema zaidi.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Hata weza kukufahamisha; lakini Unajua kuwa Nia yake ya kuwa Rais ilitoka IKULU ya Jakaya KIKWETE kumpambanisha ZITTO

  KABWE na Kijana wa RAIS; JANUARY MAKAMBA; Angalia Vile January alivyo na NGUVU Naibu Waziri ana NGUVU ya kuzuia

  WAPINZANI kwenda TANGA kufanya kampeni Kila mtu wa Kikwete aliye karibu na yeye ana bwata lolote na RAIS yuko KIMYA...

  INASIKITISHA sana... Naanza kuamini kweli Mwl. NYERERE alisema Kweli kuwa KIKWETE hauwezi URAIS; sasa hivi anatuacha

  akiondoka 2015; ataiacha NCHI kwenye MZIGO ambao SIJUI KAMA ataweza kutuacha Salama... atatuacha kwenye MASUALA

  yafuatayo;

  1. MATATIZO YA DINI ambayo yeye pia amechangia

  2. MATATIZO ya Ukabila yeye pia Amechangia

  3. MATATIZO ya Ardhi - Wageni Wamepewa Ardhi na Wengi ya wananchi hawana Ardhi

  4. Matabaka sasa Baadhi ya VIONGOZi wana Dai UKwao - January na TANGA

  5. UFISADI uliokufuru hadi USWISI

  6. Mtoto au watoto wa Rais na Marafiki kuwa na Mali
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ungeainisha kwanza vitu alivyofanya Zitto ambavyo umeamua kuviita kushirikiana na serikali ya CCM. Halafu ndio utake kuambiwa sababu ya vitu hivyo kufanyika.
   
 7. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,470
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180

  Zitto anatumika kwa Maslahi YAKE binafsi, na sio zaidi....! Kabla ya kuwa Mbunge, hakuwa anamiliki kiasi cha fedha alichonacho sasa. Na hata ukijumlisha tangu senti ya kwanza HALALI aliyoipata tangu aingie bungeni hadi sasa, jumla yake ni ndogo na kiasi anachomiliki. Ziada inatoka wapi?

  Zamani alikuwa hatoi ulmutm ili kutaja majina au scandle, now anaota ultmutm ili apewe chake anyamaze...!
  Tangu alipoitwa na Mkuu, na akaja na ishu kuwa serikali inunue Downs badala ya kuitaifisha na kuwasweka ndani wahujumu....nikajua ...... lol....Zito kashakuwa...Nyepesi!

  Nyepesi Zuberi Kbwe, anayo haki ya kuwania na kutangaza nia yake ya kuwa Rais.....Lakini ishu ni kuwa nia hiyo yake anaiongelea wapi? Anaiongelea lini? Kumuhonga vijisenti mwandishi wa habari ili aandike nia ya kuwa Rais ni kutaka kuleta chokochoko, huku ukijua chama ulichonacho kinazo taratibu zake...hali hii ndiyo inakikuta CCM now. Kila mtu anataka kuwa Rais, kila mtu anamwogopa mwenzie, kilichobaki ni makundi na mifarakano katika kuchafuana.

  ".......ooh, mkurugenzi kaonewa,......oooh, sheria za manunuzi hazikufuatwa kwa kuwapa tenda PUMA......" ISHU ni kuwa hata kama ni KATIBA nzima inavunjwa katika hali ya kumpa Mtanzania masikini unafuu, sio tu ivunjwe, ikibidi ichomwe moto, kwani cha msingi ni uzalendo kwanza....." Kikweli hapa ndipo nilipompa 5, bi kiroboto baada ya kumzodoa kutoingilia muhimili mwingine wa dola katika maamuzi yake...."

  Tushaona puppet wa aina hii wengi tu ulimwenguni, ambo mwisho wao huwa sio mzuri......!

  Kibanga Msese
   
 8. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aseme nini tena wakati kila kitu kipo wazi kaka...au upo bize kukatiza GOBI desert mkuu Marcopolo
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Time has come to fire him, ngoja tusubiri ripoti ya mzee Ngwilizi kama akitajwa kupokea rushwa aondoke mwenyewe! Halafu inashangaza wenzie ndani ya chama wanaeneza chama kupitia M4C lakini yeye sijawahi kusikia hata akitaja neno hilo M4C hata sijui kama anajua maana yake! CDM ichukue maamuzi magumu,.tena kunako mapema!!
   
 10. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wengi tulimtegemea na kumwamini, bt njaa haina bouncer .....
   
 11. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIMI najua huyu dogo soon atakuwa sifuri kabisa kwenye siasa kwani hajitambui na anatamaa ya kupitiliza ya kutaka kuwa RAIS,katumwa huyu mtusi watanzania tuweni macho.
   
 12. W

  WILLS Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi namjua sana uyu jamaa, nikibaraka mkubwa wa cdm, amejaribu kila njia kukibomoa cdm anashindwa maana kule kuna vichwa zaidi yake, kwa sasa umaarufu anai nje ya chama, ila ukifika kwenye vikao anakuwa mpole kama nn, uyu zitto amesha pitea kabisaaaaaa...ngumu kurudisha imani kwa watanzania, kula mwana cdm anamjua full kiburi sasa, daaa kweli zitto hana shukrani angalia picha kipindi akiwa mwanaharakati na sasa ni tofauti....
  Kama kweli anasingiziwa aje apa ajitetee..
   
 13. f

  fundimchundo Senior Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Zitto anahitaji msaada.
  Kubadilika ghafla yamkini kuna sababu.
  Ushirika na JK, Jack Zotta na Ikulu lazima una sababu.
  Zitto anasukumwa kugombea Uraisi kupitia CDM kwa kuwa ni rahisi kumuengua kwa kipengele cha URAIA.
  Mwenye masikio na asikie!
   
 14. aye

  aye JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  haka kajamaa sikaamini kabisa tena anajimaliza mwenyewe mana watu tushamshtukia
   
 15. s

  sad JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acheneni na mambo ya zito atajimaliza mwenyewe kama natumika. Ndio maana viongozi wenzake wamemwacha afanye atakavyo. Ipo siku mbichi na mbivu zitajulikana
   
 16. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  mkuu leo nadhani umekunywa chai bila kitafunio that why unaandika kitu usichokijua.
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Watusi wano mpango mzima wa kutawala nchi za maziwa makuu.hii ni ajenda yao ya siri, kama huyu naye ndiyo hivyo kwa TZ imekula kwake tutamgundua muda si mrefu maana tabia zao zinajulikana
   
 18. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Zitto ndio anazidi kwisha kama hajui hilo anazidi kujichimbia kaburi......Hata Bungeni Kijana Myika na Tundu Lissu walishaanza mfunika sasa ameamua kutumika CCM ili kuikoroga CDM
   
 19. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  duh! Sikuwa nikifahamu kuwa mh zitto ana walakini kwenye suala la uraia. Kwa hiyo inawezekana kuwa na mbunge ambaye sio raia wa tz?
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwanza unisamehe Mkuu Fitinamwiko, nina wasiwasi na hii avatar yako. Wakati tunasubiri Zitto aje kutupa majibu yako, naomba unisaidie jawabu wewe na wenzako ambao wana mawazo kama yako, "Ikiwa Zitto ni mnafiki, anatumiwa na CCM kuisambaratisha CDM, yupo kwa maslahi binafsi....hivi uongozi wa juu wa CDM hawayajui hayo? Kama unayajua, kwa nini unaendelea kubakia na mtu kama huyu ndani ya chama chao?"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...