Maswali ya Mwanangu kwa Mama yake yamenishtua!

Rabboni

JF-Expert Member
Apr 6, 2015
1,085
1,564
Wakuu haya mambo ya DNA najua yatakuwa yamewagusa wanaume wengi!

Nina mwanangu mdogo ndiyo atauanza mwaka wa nne hapa duniani muda sio mrefu ni wakike.
Nina uhakika ni wakwangu kwasababu tunafanana kwa kiasi kikubwa.

Sikuwepo nyumbani kwa takribani siku 6. Nilitoka kikazi kidogo, nilirejea jana jioni! Niliwakuta wako poa.
Nimefika wife kanipokea vizuri, na binti yangu pia, stori mbili tatu, nikaenda Bafuni wife alikwisha andaa utaratibu huo, wao wakawa sebleni.
Wakati narejea kujiunga nao kabla sijaingia pale niliyasikia vizuri mazungumzo yao!!
Mwanangu alikuwa anamuuliza mama yake maswali
"Mama mi nimefurahi Baba alivyokuja, je, wewe?"
akajibu hata mimi.
"Mama afu si utamtandikia baba zile shuka nzuri kuliko zote?" akajibiwa ndiyo.

Hayo maswali hayakunipa shida sana kwasababu dogo wangu anaongea sana namfahamu,
Swali hili hapa.."Mama unampenda baba?" ndiyo lilinifanya nirejelee maswali mawili ya mwanzo kwa haraka ili kubaini lengo lake lilikuwa ni lipi kuhoji hayo maswali! ofcoz sikuweza kusikia wife alijibu nini, kwani mahojiano yao yaliisha nilivyowa join story zikawa ni nyingine.

Nimekaa sana na mwanangu natamani nimuulize kwanini alimhoji mama yake aina ile ya maswali,
Sema haiji akilini akijua kama niliwasikia anaweza akadhania tofauti nikaamua ku mute!!

Who can help me here, to describe the facts of my daughter's questions to her Mom?
 
Atakuwa ndio kwanza anajifunza kuhusu upendo. Na amegundua kuwa baba hupewa vitu vizuri na spesheli kiaina. Na pengine alishasikia kwenye simu ukiambiwa i love you.

Kuna siku mtoto wa 4 yrs hivi wakati tunaangalia movie alisema 'she is pregnant'. Baba yake akamuuliza what is pregnant in swahili? Akasema 'mzuri!'. Nilijifunza kuwa positive na watoto kwa sababu ya mtizamo wa baba yule.
 
Watoto wa umri kama mwanao ni wadadisi hivyo ni hulka yao kuuliza maswali ya kudadisi mambo. Kitu cha kuhofia ni kwanini adadisi mapenzi badala ya ulimwengu unaomzunguka. Mfano anaweza kukuuliza kama kuku ana meno au hana. Hapa naona mtoto kama kawa exposed sana katika mambo ya malavidavi. Pitia vipindi vya tv, au cd anazopenda kuangalia haswa za bongo movie
 
She is just a little girl who try to learn something in a new world especially in that age..period

Ila hiyo doubt yako speaks a millions words

Sijaweka wasiwasi sana.
Dogo huwa anamaswali mengi mno. Asante kwa ushauri.
 
Atakuwa ndio kwanza anajifunza kuhusu upendo. Na amegundua kuwa baba hupewa vitu vizuri na spesheli kiaina. Na pengine alishasikia kwenye simu ukiambiwa i love you.

Kuna siku mtoto wa 4 yrs hivi wakati tunaangalia movie alisema 'she is pregnant'. Baba yake akamuuliza what is pregnant in swahili? Akasema 'mzuri!'. Nilijifunza kuwa positive na watoto kwa sababu ya mtizamo wa baba yule.

Good sana, umenifundisha kitu.
 
Acha hofu. . . .. Mtoto wa umri huo anaweza sema mambo meengi tu vile ubongo wake unamuelekeza. . . Kaa naye kwa ukaribu na mapenzi muulize maswali naye atakuuliza yake utamuelewa tu
 
Back
Top Bottom