Maswali sahihi ya kujiuliza baada ya mauaji ya polisi, Kibiti - Pwani

Nimekuwa nikiwaza tu juu ya mauaji ya mtu mmoja mmoja na mfano wa Police walio uwawa maeneo Yale ya Kibiti, Hivi serikali haiwezi anzisha kambi kama tatu za mafuzo ya Jkt kule, maana kigeografia naona kama panaruhusu sana maeneo Yale majeshi yetu kufanyia mafunzo kule na serkali ikawalipa baadhi ya Raia watakao hamishwa maeneo hayo.

Najua hali ulivyo imewanyima watu uhuru na mazoea yao ya maisha ya kawaida.

Mfono nikiwa Shule nilikuwa nasikia tu uzalendo wa Mwalimu Kambarage kuwa alikuwa akisikia mahari pana madini na mali nyingi kwenye hilo eneo alikuwa anaazisha kambi ya Jkt kwaajili ya mafunzo.

Maana nikiwaza ugumu wa sasa wa pesa na ukiwa kwenye mizunguko huku unawaza usalama wa familia yako hii ngumu sana.

Ok ni Mtazamo tu.
 
Habari zilizotufikia zinaeleza kwamba Nurdin Kisinga ambaye ni askari mgambo, amepigwa risasi katika Pori la Gomboroni, Ikwiriri majira ya saa tisa mchana wa leo (June 7, 2017).
Tukio hilo limetokea saa chache baada ya IGP Simon Sirro kuzuru ukanda huo unaoongoza kwa mauaji ya raia yenye utata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha mtu huyo kupigwa risasi lakini akasema anayeweza kuthibitisha kama amekufa au laa, ni daktari lakini taarifa alizonazo yeye ni kwamba amejeruhiwa kwa risasi.
Mtu mwingine, Eric Mwarabu ambaye alikuwa ni askari mgambo, jana usiku alipigwa risasi na kuuawa akiwa nyumbani kwake. Mwenye taarifa zaidi azidi kutujuza.
 
Rais anaongelea issue ya kibiti kama kuna watu anawakomoa ila kinachotrinspire on the ground ni kitu kingine kabisa.

Kupeleka high profile figures kibiti ili kuwapa watu matumaini sio mkakati mzuri maana matukio yakitokea huku viongozi wapo huko ndio confidence inapotea kabisa kwa watu.

Hao wauaji wanataka kutoa statement na kuwapelekea high profile targets ni kuwasaidia kukamilisha mkakati wao. Mimi sioni hili suala la kibiti likiisha kesho au keshokutwa. I see it as the beginning of a long bloody conflict!
 
Response ya Jeshi la polisi so far imekuwa ya kuonyesha hasira kuliko ya kimkakati.

".... you don't shoot a cop, everybody wants a cop killer " .Haya ni baadhi ya maneno aliyoongea James Files, muuaji wa J. F. Kennedy baada ya kuulizwa juu ya muuaji wa afsa polisi J. Tippid. Mr. Files alimaanisha kuwa, hakuna mhalifu anayeua askari bila sababu za lazima sana kwasababu taasisi zote za kiupelelezi na kiuchunguzi zitamtafuta.

Somalia na Sudan, silaha zinauzwa bei ndogo sana inasemekana. Tena hizi bunduki kubwa ndio chee kabisa kwasababu ya ugumu wa usafirishaji ukilinganisha na bastola.

Sasa, katika mwangaza wa yote haya, ni nani na kwanini, atafute attention kubwa hivi na ugomvi karibu na taasisi zote za kiuchunguzi kwa mauaji ya polisi Kibiti ?
Hili ni moja kati ya maswali kedekede yanayoulizwa katika jukwaa hili na majukwaa mengine juu ya shambulio hili.

Ili kupata majibu sahihi na kupiga hatua kwenye hili, ni muhimu kujiuliza maswali sahihi.

MASWALI :
1. Kuna tukio lingine kama hili litakalokuja siku za usoni?
Moja kati ya wajibu wa maafisa wa usalama ni kung'amua iwapo kuna uwezekano wa tukio jingine litakalo ambatana na hili.
Kuna wakati kikundi cha kihalifu kinapanga tukio zaidi ya moja kwa kutumia wapiganaji wake waliosambaa maeneo mbalimbali.

2. Je, tukio hili linahusisha mtu mmoja, watu wachache, au utekelezaji wake unafungamana na organization yeyote kubwa?
Ni muhimu kujua kama washambuliaji ni sehemu ya network kubwa. Tukio lenyewe linaweza kuratibiwa na kutekelezwa na watu wachache, ila watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya kundi kubwa.

3. Je, kuna uhusika wowote kutoka nje ya nchi? Vyombo mbalimbali vinaweza kuhusishwa kulingana na upana wa tukio.
Ni muhimu pia kujua kama kuna taifa jingine linahusika katika tukio hili. Mara nyingi ushiriki wa taifa jingine unapuuzwa ila ukweli ni kuwa nchi jirani zinaweza kunufaika kwa namna moja au nyingine kwenye matukio kama haya.

4. Je, uhusika wa jamii kwenye tukio hili ukoje? jamii imechukia au imefurahi?
Ni mara chache matukio kama haya yanaonyesha hisia za jamii, ila hii haina maana kuwa jamii haina uhusika.

5. Je, maafisa wa serikali wamefanya makosa gani? Hii inaweza kukushangaza, ila serikali yako sio perfect. Ni kawaida kutafuta mchawi baada ya matukio kama haya japo, mara nyingi, udhifu katika kuzuia matukio kama haya huwa wa kitaasisi zaidi kuliko wa watu binafsi.

6. Je, mabadiliko gani katika mamlaka ni muhimu baada ya mtukio kama haya?
Sio kila wakati serikali inapokosea mabadiliko ni lazima.
Kila mabadiliko yanakuja na gharama mpya na uwezekano mpya wa makosa.

Pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Pole kwa jeshi la polisi.
Tunaweza kulishinda hili ndani ya misingi ya sheria.
Ashakum si matusi, sikuhizi Polisi wanatofautiana kidooooogo sana na mbwa.
Mkuu wa wilaya:- kamata yuree!!!
Mkuu wa waganga wa kienyeji:- kamat yureee!!

Wala hatuoni wanachokifundishwa CCP.
Maana nina uhakika hawakufundishwa kuwapiga walemavu.

Usitegemee kukuta think-tank zenye viwango huko geshini!!

Only scrambling for title
 
Mleta huu uzi nimekuelewa vizuri saaana ni lazima wajitambue
Kwa mtazamo wangu mimi unaporafuta mbinu ama plan ya kupambana na Adui wako lazma na yeye umfkirie kua kajiandaaje
Lkn ukienda PUPA,HASIRA au PANIC hapo utacheemka
La pili hawa wauwaji lazma wanasabab yao muhim mnoo hadi wafkie hatua kama hii ya kuua maaskari tu,na mpaka wameamua kufanya hivo ujue na wao wamejipanga na kuna wazoefu hapo wapo ma SPECIAL SNIPPERS wapo WENYEJI WA MSITU
wapo WATEGAJI WAZOEFU kwa SILAHA ZA KIENYEJI KTK MACHAKA na wengineo
Kwahivo ni lazma ya kujitambua kwanza ww ulivo kabla ya kupambana na adui wako
 
Mleta huu uzi nimekuelewa vizuri saaana ni lazima wajitambue
Kwa mtazamo wangu mimi unaporafuta mbinu ama plan ya kupambana na Adui wako lazma na yeye umfkirie kua kajiandaaje
Lkn ukienda PUPA,HASIRA au PANIC hapo utacheemka
La pili hawa wauwaji lazma wanasabab yao muhim mnoo hadi wafkie hatua kama hii ya kuua maaskari tu,na mpaka wameamua kufanya hivo ujue na wao wamejipanga na kuna wazoefu hapo wapo ma SPECIAL SNIPPERS wapo WENYEJI WA MSITU
wapo WATEGAJI WAZOEFU kwa SILAHA ZA KIENYEJI KTK MACHAKA na wengineo
Kwahivo ni lazma ya kujitambua kwanza ww ulivo kabla ya kupambana na adui wako
Sasa hii hoja yako ndio Nsato Marijani hataki hata kuisikia , yeye ni vitisho mwanzo mwisho .
 
Ashakum si matusi, sikuhizi Polisi wanatofautiana kidooooogo sana na mbwa.
Mkuu wa wilaya:- kamata yuree!!!
Mkuu wa waganga wa kienyeji:- kamat yureee!!

Wala hatuoni wanachokifundishwa CCP.
Maana nina uhakika hawakufundishwa kuwapiga walemavu.

Usitegemee kukuta think-tank zenye viwango huko geshini!!

Only scrambling for title
Jesus Christ!! Unazo akili zilizotimia kabisa au umebebwa na mahaba ya kisiasa huko na ukosefu wa dili mwilini mwako? hebu tujuze
 
Jesus Christ!! Unazo akili zilizotimia kabisa au umebebwa na mahaba ya kisiasa huko na ukosefu wa dili mwilini mwako? hebu tujuze
Naona umeanza kwa kizungu, mambo yakipamba moto kidogo utahamia kwenye kiswahili yakiharibika kabisa beyond repair utatamka kwa kikwenu like "baba nishoshage kunzengo kwa ng'waguuku"
 
Naona umeanza kwa kizungu, mambo yakipamba moto kidogo utahamia kwenye kiswahili yakiharibika kabisa beyond repair utatamka kwa kikwenu like "baba nishoshage kunzengo kwa ng'waguuku"

Jamii forum humu kuna machizi wengi kweli
 
Kwa kuwa wanaua askari na viongozi bila kuiba chochote zaidi ya silaha,huoni kuna haja ya kuwakamata wakiwa hai ili kujua lengo lao na mbinu zao?
Wauawe tu kwa maana wameua Askari hakuna haja ya ushahidi maana wakiachwa watasumbua. Hii ni mfano kwa wenzao na wenye mawazo kama yao.
 
Back
Top Bottom