Maswali sahihi ya kujiuliza baada ya mauaji ya polisi, Kibiti - Pwani

Sasa mkuu, ni kweli ulitegemea mkakati rasmi wa kiusalama wa kushughurikia suala hili ubainashwe hadharani, mbele ya press au msibani? Suala hili ni nyeti na amini usiamini sio Polisi tu bali vyombo vyote vya kiusalama vya Taifa sasa hivi vimo kazini usiku na mchana ila tu tukumbuke ugumu wa kupambana na adui anayepigana nawe kwa mtindo wa HIT & RUN.
Sikukubaliana na kauli ya Nsato Marijani , haikuwa na weredi , halafu kingine ni kwamba hili si jambo la juzi tu, lilikwishatokea na tukaambiwa limeshughulikiwa , kuna komando kauawawa/ kakamatwa , mbona yanajirudia tena ?
 
6.Mabadiliko hakuna,maana wao wanaweza kuwa wanataka kuanzisha tawala zao zile kama Ninawi,mosoul,raqqa nk,kwa utawala wa kawaida ni ngumu kukaa nao zaidi ya kuwashughulikia tu
5.Maafisa wa serikali hawana makosa yyte,but adui yao namba moja ni mtu au mtumishi anaeunga mkono serikali iliyopo madarakani,kwa hiyo ni suala la kitaifa zaidi,kama wwe ni mtz wa mlengo wa kati hili linakuhusu,siadi nchi yako
4.Wanaofurahi ni wale wanaoona kuwa wanaweza Ku -exist kwenye utawala huo,ie ukiiba unakatwa mkono,ukizini unapigwa mawe mpka ufe,na mengineyo,lakini wakumbuke kabla ya kushangilia watafute taarifa hizi,je walioko Raqqa wana kitu cha maana sana wanachokipata?
3.Kama ni kweli ni hao wanaojiita wenye msimamo mkali kitu cha kuangalia,nchi ambazo walikuwepo hawa jamaa kama Syria, Iraq,Libya na kwa Jirani zetu Somalia hakuna uhakika wa watu hawa kuwepo,maana mashambulizi ya nchi za magharibi ni makubwa,lakini pia hawala zao zimeanza kupoteza nguvu hasa Mosoul,Raqqa,Ninaw,Sirte na Somalia, kwa hyo Upo uwezekano wakawa wamekimbilia huku.
2.Kuteka na kuua polisi nane si kazi ya mtu mmoja,jeshi letu si dhaifu kiasi cha kutekwa na mtu mmoja,
1.Hawa jamaa wanajipanga,swali rahisi,silaha wamechukua za nn?
Note: Tuwasaidie polisi, wakitoka kwao sisi hatuko salama!
Pumba+
 
Binafsi mimi nikimkuta askari anagombana na nyoka naua askari numuacha nyoka aende zake
 
Binafsi mimi nikimkuta askari anagombana na nyoka naua askari numuacha nyoka aende zake
Duu!
Umeweka bandiko la kiwango cha juu mno ! Nadhani huu ndio uzi pekee fikirishi tangu mauaji ya polisi wetu yatokee .

Binafsi nilivyowaona na kuwasikia viongozi wa polisi , ni kama wanataka kulipa kisasi tu , haionekani dalili ya kuja na majibu na kukomesha hali hii, wamejaa chuki na vitisho , kiukweli jambo hili linahitaji busara na weledi mkubwa sana .
 
Mleta mada umehoji mambo ya msingi sana, hiyo ndio critical thinking. Kwa kuongezea tu, Hivi mpaka sasa Polisi wanaweza kusema Dhamira hasa ya hayo mauaji ni nini?

Siyo jambo la kawaida kwa muharifu kwenda kumvamia mtu na kumuua pasipo sababu ya msingi au msukumo fulani.
 
Akili yangu mpaka sasa inanituma kuamini kuwa mara nyingi tukio la namna kama hiyo huwa ni tukio la kulipiza kisasi, au kugeukana au kuzungukana. Jambo la msingi kwa jeshi la Polisi kwa sasa ni kupeleleza na kugundua chanzo hasa ni nini kuliko kuishia kukimbizana tu kuwatafuta wauaji.
 
Kuna utata mwingi sana kutekwa kwa raia, kupambana na madawa ya kulevya, kuuwawa kwa askari polisi, mwisho usalama wetu he ukoje kwa mambo ya namna hiyo afu wanaohusika na taaluma zao ni mikwara mingi sana ufumbuzi hauonekani......
 
Response ya Jeshi la polisi so far imekuwa ya kuonyesha hasira kuliko ya kimkakati.

".... you don't shoot a cop, everybody wants a cop killer " .Haya ni baadhi ya maneno aliyoongea James Files, muuaji wa J. F. Kennedy baada ya kuulizwa juu ya muuaji wa afsa polisi J. Tippid. Mr. Files alimaanisha kuwa, hakuna mhalifu anayeua askari bila sababu za lazima sana kwasababu taasisi zote za kiupelelezi na kiuchunguzi zitamtafuta.

Somalia na Sudan, silaha zinauzwa bei ndogo sana inasemekana. Tena hizi bunduki kubwa ndio chee kabisa kwasababu ya ugumu wa usafirishaji ukilinganisha na bastola.

Sasa, katika mwangaza wa yote haya, ni nani na kwanini, atafute attention kubwa hivi na ugomvi karibu na taasisi zote za kiuchunguzi kwa mauaji ya polisi Kibiti ?
Hili ni moja kati ya maswali kedekede yanayoulizwa katika jukwaa hili na majukwaa mengine juu ya shambulio hili.

Ili kupata majibu sahihi na kupiga hatua kwenye hili, ni muhimu kujiuliza maswali sahihi.

MASWALI :
1. Kuna tukio lingine kama hili litakalokuja siku za usoni?
Moja kati ya wajibu wa maafisa wa usalama ni kung'amua iwapo kuna uwezekano wa tukio jingine litakalo ambatana na hili.
Kuna wakati kikundi cha kihalifu kinapanga tukio zaidi ya moja kwa kutumia wapiganaji wake waliosambaa maeneo mbalimbali.

2. Je, tukio hili linahusisha mtu mmoja, watu wachache, au utekelezaji wake unafungamana na organization yeyote kubwa?
Ni muhimu kujua kama washambuliaji ni sehemu ya network kubwa. Tukio lenyewe linaweza kuratibiwa na kutekelezwa na watu wachache, ila watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya kundi kubwa.

3. Je, kuna uhusika wowote kutoka nje ya nchi? Vyombo mbalimbali vinaweza kuhusishwa kulingana na upana wa tukio.
Ni muhimu pia kujua kama kuna taifa jingine linahusika katika tukio hili. Mara nyingi ushiriki wa taifa jingine unapuuzwa ila ukweli ni kuwa nchi jirani zinaweza kunufaika kwa namna moja au nyingine kwenye matukio kama haya.

4. Je, uhusika wa jamii kwenye tukio hili ukoje? jamii imechukia au imefurahi?
Ni mara chache matukio kama haya yanaonyesha hisia za jamii, ila hii haina maana kuwa jamii haina uhusika.

5. Je, maafisa wa serikali wamefanya makosa gani? Hii inaweza kukushangaza, ila serikali yako sio perfect. Ni kawaida kutafuta mchawi baada ya matukio kama haya japo, mara nyingi, udhifu katika kuzuia matukio kama haya huwa wa kitaasisi zaidi kuliko wa watu binafsi.

6. Je, mabadiliko gani katika mamlaka ni muhimu baada ya mtukio kama haya?
Sio kila wakati serikali inapokosea mabadiliko ni lazima.
Kila mabadiliko yanakuja na gharama mpya na uwezekano mpya wa makosa.

Pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Pole kwa jeshi la polisi.
Tunaweza kulishinda hili ndani ya misingi ya sheria.
 
Bado nasisitiza , weledi na mtazamo sahihi vinaitajika kuinusuru kibiti na uonevu unaoendelea leo.
Ni ngumu kuamini ila ndio Tanzania imeingia kwenye utaratibu wa road side justice.
 
Kuna swali la msingi sana ambalo Watu wengi wanakisahau! Wale wananchi waliouwawa na majambazi wanaokaribia 20 huko pwani wakiwemo wenyeviti na watendaji ni baada ya wao kutoa taarifa za Siri kwa polisi kuhusu majambazi.

Hivi hao majambazi walijuaje kua hao ndio waliotoa Taarifa kwenye jeshi la polisi? Hivi kuna uwezekano kukawa ndani ya polisi pwani ushirikiano mkubwa na majambazi? Kwanini polisi pwani isichunguzwe? Ili kubaini wasaliti?
 
Juzi nimesoma kwenye gazeti la MWANANCHI,,,kuna mgambo wa huko kibiti ameuliwa na majambazi walimfuata kwake wakampiga risasi ya shingo
 
Mimi niliwaonea huruma sana polisi ,ila hii operesheni yao feki wamepora Mali zangu dukani natamani wauliwe woooote tuwafundishe kazi polisi wapya watakaokuwa wema
 
Yanayoendelea Kibiti yanakwambia kuwa ukiuliza wrong questions utapata wrong answers! alwayz
R.I.P viongozi wa ccm kibiti
 
Back
Top Bottom