Maswali sahihi ya kujiuliza baada ya mauaji ya polisi, Kibiti - Pwani

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
Response ya Jeshi la polisi so far imekuwa ya kuonyesha hasira kuliko ya kimkakati.

".... you don't shoot a cop, everybody wants a cop killer " .Haya ni baadhi ya maneno aliyoongea James Files, muuaji wa J. F. Kennedy baada ya kuulizwa juu ya muuaji wa afsa polisi J. Tippid. Mr. Files alimaanisha kuwa, hakuna mhalifu anayeua askari bila sababu za lazima sana kwasababu taasisi zote za kiupelelezi na kiuchunguzi zitamtafuta.

Somalia na Sudan, silaha zinauzwa bei ndogo sana inasemekana. Tena hizi bunduki kubwa ndio chee kabisa kwasababu ya ugumu wa usafirishaji ukilinganisha na bastola.

Sasa, katika mwangaza wa yote haya, ni nani na kwanini, atafute attention kubwa hivi na ugomvi karibu na taasisi zote za kiuchunguzi kwa mauaji ya polisi Kibiti ?
Hili ni moja kati ya maswali kedekede yanayoulizwa katika jukwaa hili na majukwaa mengine juu ya shambulio hili.

Ili kupata majibu sahihi na kupiga hatua kwenye hili, ni muhimu kujiuliza maswali sahihi.

MASWALI :
1. Kuna tukio lingine kama hili litakalokuja siku za usoni?
Moja kati ya wajibu wa maafisa wa usalama ni kung'amua iwapo kuna uwezekano wa tukio jingine litakalo ambatana na hili.
Kuna wakati kikundi cha kihalifu kinapanga tukio zaidi ya moja kwa kutumia wapiganaji wake waliosambaa maeneo mbalimbali.

2. Je, tukio hili linahusisha mtu mmoja, watu wachache, au utekelezaji wake unafungamana na organization yeyote kubwa?
Ni muhimu kujua kama washambuliaji ni sehemu ya network kubwa. Tukio lenyewe linaweza kuratibiwa na kutekelezwa na watu wachache, ila watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya kundi kubwa.

3. Je, kuna uhusika wowote kutoka nje ya nchi? Vyombo mbalimbali vinaweza kuhusishwa kulingana na upana wa tukio.
Ni muhimu pia kujua kama kuna taifa jingine linahusika katika tukio hili. Mara nyingi ushiriki wa taifa jingine unapuuzwa ila ukweli ni kuwa nchi jirani zinaweza kunufaika kwa namna moja au nyingine kwenye matukio kama haya.

4. Je, uhusika wa jamii kwenye tukio hili ukoje? jamii imechukia au imefurahi?
Ni mara chache matukio kama haya yanaonyesha hisia za jamii, ila hii haina maana kuwa jamii haina uhusika.

5. Je, maafisa wa serikali wamefanya makosa gani? Hii inaweza kukushangaza, ila serikali yako sio perfect. Ni kawaida kutafuta mchawi baada ya matukio kama haya japo, mara nyingi, udhifu katika kuzuia matukio kama haya huwa wa kitaasisi zaidi kuliko wa watu binafsi.

6. Je, mabadiliko gani katika mamlaka ni muhimu baada ya mtukio kama haya?
Sio kila wakati serikali inapokosea mabadiliko ni lazima.
Kila mabadiliko yanakuja na gharama mpya na uwezekano mpya wa makosa.

Pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Pole kwa jeshi la polisi.
Tunaweza kulishinda hili ndani ya misingi ya sheria.
 
Gaidi yeyote huwa anatafuta kichaka cha kujikingia.

Watakuja kufa wananchi wa kawaida,watakwambia ni haki wanatafuta.
 
Umeweka bandiko la kiwango cha juu mno ! Nadhani huu ndio uzi pekee fikirishi tangu mauaji ya polisi wetu yatokee .

Binafsi nilivyowaona na kuwasikia viongozi wa polisi , ni kama wanataka kulipa kisasi tu , haionekani dalili ya kuja na majibu na kukomesha hali hii, wamejaa chuki na vitisho , kiukweli jambo hili linahitaji busara na weledi mkubwa sana .
 
Wewe utaamini wa naona uchumi kuwa ni wanachi wa kawaida.Magaidi na majambazi wanajulikana hapa nchini.Huwa hakamatwi kusubiri ushahidi wa kuwapeleka mahakamani.Sasa kwa kuwa wameichokoza polisi,wanasakwa mmoja mmoja
 
Kwa kuwa wanaua askari na viongozi bila kuiba chochote zaidi ya silaha,huoni kuna haja ya kuwakamata wakiwa hai ili kujua lengo lao na mbinu zao?
 
Bila ya shaka wewe ni afisa usalama,tena uliebobea,
umechambua vizuri,sana,polisi wetu wanataka kulipa kisasi tu,kutokana na maneno ya kamishna wao jana kwenye media,naamini hawatofanikiwa,kwa kuwa wana jazba.
Anaetaka aamini au asiamini,hii operesheni inataka utulivu na upembuzi yakinifu.
 
Mleta mada umenena vyema. Kuongezea ni kuwa umaahari wa Jeshi la Police duniani pote ni 'Upelelezi' nusa nusa wakiitwa. Sio physical confrontation zaidi. Wako wapi wale wakiitwa 'CID' wa enzi zile. Kwenye tukio kijijini atakwenda kama mfanya biashara mchuuzi, akinywa pombe za kienyeji vilabuni. Hata mkaa at a choma. Kwa issue ya Mkurunga hata kuhamia na kupata mabint wa marafiki wangeshafanya hayo. Leo hii jibu la mauaji lingeshapatikanika. Na huenda haya yamefanyika ila hatupewi ukweli kwakuogopa kitu fulani. Haiwezekani askari na Viongozi wa mitaa wauwawe kisha Jeshi lisubiri wengine wafe ndio waendeshe operation ambayo ndani ya masaa Kadhalika wawagundue pamoja na maficho yao na kukamata Silaha..Tulisaidia nchi za kusini hadi kumshinda kaburu leo tinashindwa kumjua adui anaeua askari wetu... Noo Madetective fanyeni kazi yenu. Hili neno lugha ya ' na watu wasiojulikana' ni dongo kubwa kwenu. Vyeo mnapandaje sasa
 
Wewe utaamini wa naona uchumi kuwa ni wanachi wa kawaida.Magaidi na majambazi wanajulikana hapa nchini.Huwa hakamatwi kusubiri ushahidi wa kuwapeleka mahakamani.Sasa kwa kuwa wameichokoza polisi,wanasakwa mmoja mmoja[/QUOTE
sijakusoma ndugu yangu.
 
Wewe utaamini wa naona uchumi kuwa ni wanachi wa kawaida.Magaidi na majambazi wanajulikana hapa nchini.Huwa hakamatwi kusubiri ushahidi wa kuwapeleka mahakamani.Sasa kwa kuwa wameichokoza polisi,wanasakwa mmoja mmoja
Ndugu yangu, sijui ni hii pasaka au vipi, sijakusoma!
 
Response ya Jeshi la polisi so far imekuwa ya kuonyesha hasira kuliko ya kimkakati.

".... you don't shoot a cop, everybody wants a cop killer " .Haya ni baadhi ya maneno aliyoongea James Files, muuaji wa J. F. Kennedy baada ya kuulizwa juu ya muuaji wa afsa polisi J. Tippid. Mr. Files alimaanisha kuwa, hakuna mhalifu anayeua askari bila sababu za lazima sana kwasababu taasisi zote za kiupelelezi na kiuchunguzi zitamtafuta.

Somalia na Sudan, silaha zinauzwa bei ndogo sana inasemekana. Tena hizi bunduki kubwa ndio chee kabisa kwasababu ya ugumu wa usafirishaji ukilinganisha na bastola.

Sasa, katika mwangaza wa yote haya, ni nani na kwanini, atafute attention kubwa hivi na ugomvi karibu na taasisi zote za kiuchunguzi kwa mauaji ya polisi Kibiti ?
Hili ni moja kati ya maswali kedekede yanayoulizwa katika jukwaa hili na majukwaa mengine juu ya shambulio hili.

Ili kupata majibu sahihi na kupiga hatua kwenye hili, ni muhimu kujiuliza maswali sahihi.

MASWALI :
1. Kuna tukio lingine kama hili litakalokuja siku za usoni?
Moja kati ya wajibu wa maafisa wa usalama ni kung'amua iwapo kuna uwezekano wa tukio jingine litakalo ambatana na hili.
Kuna wakati kikundi cha kihalifu kinapanga tukio zaidi ya moja kwa kutumia wapiganaji wake waliosambaa maeneo mbalimbali.

2. Je, tukio hili linahusisha mtu mmoja, watu wachache, au utekelezaji wake unafungamana na organization yeyote kubwa?
Ni muhimu kujua kama washambuliaji ni sehemu ya network kubwa. Tukio lenyewe linaweza kuratibiwa na kutekelezwa na watu wachache, ila watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya kundi kubwa.

3. Je, kuna uhusika wowote kutoka nje ya nchi? Vyombo mbalimbali vinaweza kuhusishwa kulingana na upana wa tukio.
Ni muhimu pia kujua kama kuna taifa jingine linahusika katika tukio hili. Mara nyingi ushiriki wa taifa jingine unapuuzwa ila ukweli ni kuwa nchi jirani zinaweza kunufaika kwa namna moja au nyingine kwenye matukio kama haya.

4. Je, uhusika wa jamii kwenye tukio hili ukoje? jamii imechukia au imefurahi?
Ni mara chache matukio kama haya yanaonyesha hisia za jamii, ila hii haina maana kuwa jamii haina uhusika.

5. Je, maafisa wa serikali wamefanya makosa gani? Hii inaweza kukushangaza, ila serikali yako sio perfect. Ni kawaida kutafuta mchawi baada ya matukio kama haya japo, mara nyingi, udhifu katika kuzuia matukio kama haya huwa wa kitaasisi zaidi kuliko wa watu binafsi.

6. Je, mabadiliko gani katika mamlaka ni muhimu baada ya mtukio kama haya?
Sio kila wakati serikali inapokosea mabadiliko ni lazima.
Kila mabadiliko yanakuja na gharama mpya na uwezekano mpya wa makosa.

Pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Pole kwa jeshi la polisi.
Tunaweza kulishinda hili ndani ya misingi ya sheria.

kwa uwezo wa polisi yetu hawawezi haya, wengi wapo uku baada ya kufeli maisha na elimu zao ndio ivyo
 
Umeweka bandiko la kiwango cha juu mno ! Nadhani huu ndio uzi pekee fikirishi tangu mauaji ya polisi wetu yatokee .

Binafsi nilivyowaona na kuwasikia viongozi wa polisi , ni kama wanataka kulipa kisasi tu , haionekani dalili ya kuja na majibu na kukomesha hali hii, wamejaa chuki na vitisho , kiukweli jambo hili linahitaji busara na weledi mkubwa sana .
Asante mkuu.
 
Kwa kuwa wanaua askari na viongozi bila kuiba chochote zaidi ya silaha,huoni kuna haja ya kuwakamata wakiwa hai ili kujua lengo lao na mbinu zao?

Niongeze swali hapo juu, hao askari 8 waliokufa wana muda gani tokea waende huko kibiti na wametokea kambi zipi kufika huko na kwa nini?
 
Back
Top Bottom