Maswali sahihi ya kujiuliza baada ya mauaji ya polisi, Kibiti - Pwani

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa hapa jf na member Informer ni kwamba muuaji alikuwa mmoja na ndiye aliyefanya mauaji ya polisi hao hivyo kwa haraka tuseme bunduki aliyokuwa nayo ni AK47/SMG 56 na ndio maana aliweza kuwadondosha wote, na Tanzania hatuna duka linalouza assalt rifle je wauaji wanapata wapi silaha? inawezekana ni hujuma kutoka nchi jirani kama ndivyo basi maana yake ulinzi maeneo ya mipakani ni dhaifu na sera yetu kuhusu uhamiaji na kuacha watu waingie nchini kama choo cha umma ni tatizo la msingi kwa sababu silaha hazipiti airport au bandarini.
 
Kwanini Rais wa Jamhuri wa Tanzania hakwenda kwenye msiba huu wa taifa ? Hostel hazihami angepeleka hata muwakilishi lakini sio kukosa tukio hili yeye kama amiri jeshi Mkuu wa nchi
 
Hii operesheni isiishie Mkoa wa pwani tu,inawezekana hawa wahalifu wakawa wanatekelezea uhalifu pwani lakini wanakaa jirani na Mkoa wa pwani,au wako ndani ya Mkoa wa pwani,wilaya nyingine,wanafanya uhalifu halafu wanaenda mwingine kutulia.

Nadhani polisi waangalie Mkoa zaidi ya mmoja,

Kamati za ulinzi na usalama za vitongoji,vijiji,kata,tarafa zitambue wageni wasioeleweka na wenyeji waliobadilika tabia na wanaopokea wageni wasioeleweka,wanaowapokea wahojiwe
 
Kwa mujibu wa habari iliyotolewa hapa jf na member Informer ni kwamba muuaji alikuwa mmoja na ndiye aliyefanya mauaji ya polisi hao hivyo kwa haraka tuseme bunduki aliyokuwa nayo ni AK47/SMG 56 na ndio maana aliweza kuwadondosha wote, na Tanzania hatuna duka linalouza assalt rifle je wauaji wanapata wapi silaha? inawezekana ni hujuma kutoka nchi jirani kama ndivyo basi maana yake ulinzi maeneo ya mipaka ni dhaifu na sera yetu kuhusu uhamiaji na kuacha watu waingie nchini kama choo cha umma ni tatizo la msingi.
Inawezekana ikawa si nchi,ni kikundi kutoka mahali fulani, au ni watanzania wenzetu, sehemu hatarishi yenye tabia kama hizi kwa afrika mashariki ni Mombasa,
 
Kwanini Rais wa Jamhuri wa Tanzania hakwenda kwenye msiba huu wa taifa ? Hostel hazihami angepeleka hata muwakilishi lakini sio kukosa tukio hili yeye kama amiri jeshi Mkuu wa nchi
Kwake nadhani mazishi hayakuwa kipaumbele.
 
Mara nyingi hawa wanao fanya hivi huwa na sababu, huwa wanaona kuna kitu wanaonelewa na watawala "mtizamo wao " ndio hutafuta njia mbali mbali kuonesha hasira zao na mara nyingi njia ya mapigano ya kuvizia hu husika.
Mtazamo wangu serikali sababu za hao wanao waita majambazi, hakuna nchi yoyote duniani imeshawahi kushinda vita vya kuviziana tatizo hilo linawasumbua wamarekani, ulaya, na hata majirani zetu wa Kenya tusijidanganye.
 
Inawezekana ikawa si nchi,ni kikundi kutoka mahali fulani, au ni watanzania wenzetu, sehemu hatarishi yenye tabia kama hizi kwa afrika mashariki ni Mombasa,
Kwanini umewaza Mombasa na sio Mishia-Burundi au DRC ya mpkn na Kigoma.?
 
Polisi wanapaswa kutulia na kutumia akili zaidi wakati huu kwani wasipokuwa makini watawadhuru wasiohusika na kuendelea kujenga visasi. Lakini pia polisi iache kulazimisha hisia za huruma kutoka kwa wananchi.

Wengi wamesikitushwa kakini wale wachache ambao hawana hisia za uchungu kutokana na tukio hili nao waachwe ndio ubinadamu hatuwezi wote kuwa na hisia moja. Hata alipokufa Nyerere wengi tulilia lakini wapo waliokejeli na kufurahi. Hao wanafurahi au kukejeli huenda wameshaonja machungu ya polisi kama kubambikiwa kesi au kupigwa bila sababu hasa kwenye mikutano au wanapoona polisi hawahangaiki sana wanapopotea raia au kufa raia wa kawaida hivyo kwao polisi wakipata madhara hufari kama sehemu ya malipizi. Nina imani miongoni mwa polisi kuna waliosoma saikolojia watakuwa wanaekewa namna ya kukabiliana na watakaowapa pole na wale watakao wacheka.

Viongozi wa juu wa polisi eanahitaji msaada mkubwa wa kisaikolojia kwa sasa kwani hadira zao ni hatari kwa ustawi wa taifa na katika matukio haya inakuwa kama mtego wa panya.huingia waliomo na wadiokuwamo. Poleni sana wafiwa na poleni sana jeshi la polisi
 
Response ya Jeshi la polisi so far imekuwa ya kuonyesha hasira kuliko ya kimkakati.

".... you don't shoot a cop, everybody wants a cop killer " .Haya ni baadhi ya maneno aliyoongea James Files, muuaji wa J. F. Kennedy baada ya kuulizwa juu ya muuaji wa afsa polisi J. Tippid. Mr. Files alimaanisha kuwa, hakuna mhalifu anayeua askari bila sababu za lazima sana kwasababu taasisi zote za kiupelelezi na kiuchunguzi zitamtafuta.

Somalia na Sudan, silaha zinauzwa bei ndogo sana inasemekana. Tena hizi bunduki kubwa ndio chee kabisa kwasababu ya ugumu wa usafirishaji ukilinganisha na bastola.

Sasa, katika mwangaza wa yote haya, ni nani na kwanini, atafute attention kubwa hivi na ugomvi karibu na taasisi zote za kiuchunguzi kwa mauaji ya polisi Kibiti ?
Hili ni moja kati ya maswali kedekede yanayoulizwa katika jukwaa hili na majukwaa mengine juu ya shambulio hili.

Ili kupata majibu sahihi na kupiga hatua kwenye hili, ni muhimu kujiuliza maswali sahihi.

MASWALI :
1. Kuna tukio lingine kama hili litakalokuja siku za usoni?
Moja kati ya wajibu wa maafisa wa usalama ni kung'amua iwapo kuna uwezekano wa tukio jingine litakalo ambatana na hili.
Kuna wakati kikundi cha kihalifu kinapanga tukio zaidi ya moja kwa kutumia wapiganaji wake waliosambaa maeneo mbalimbali.

2. Je, tukio hili linahusisha mtu mmoja, watu wachache, au utekelezaji wake unafungamana na organization yeyote kubwa?
Ni muhimu kujua kama washambuliaji ni sehemu ya network kubwa. Tukio lenyewe linaweza kuratibiwa na kutekelezwa na watu wachache, ila watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya kundi kubwa.

3. Je, kuna uhusika wowote kutoka nje ya nchi? Vyombo mbalimbali vinaweza kuhusishwa kulingana na upana wa tukio.
Ni muhimu pia kujua kama kuna taifa jingine linahusika katika tukio hili. Mara nyingi ushiriki wa taifa jingine unapuuzwa ila ukweli ni kuwa nchi jirani zinaweza kunufaika kwa namna moja au nyingine kwenye matukio kama haya.

4. Je, uhusika wa jamii kwenye tukio hili ukoje? jamii imechukia au imefurahi?
Ni mara chache matukio kama haya yanaonyesha hisia za jamii, ila hii haina maana kuwa jamii haina uhusika.

5. Je, maafisa wa serikali wamefanya makosa gani? Hii inaweza kukushangaza, ila serikali yako sio perfect. Ni kawaida kutafuta mchawi baada ya matukio kama haya japo, mara nyingi, udhifu katika kuzuia matukio kama haya huwa wa kitaasisi zaidi kuliko wa watu binafsi.

6. Je, mabadiliko gani katika mamlaka ni muhimu baada ya mtukio kama haya?
Sio kila wakati serikali inapokosea mabadiliko ni lazima.
Kila mabadiliko yanakuja na gharama mpya na uwezekano mpya wa makosa.

Pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Pole kwa jeshi la polisi.
Tunaweza kulishinda hili ndani ya misingi ya sheria.
Vita baridi ni mbaya sana ni ukweli usiopingka kuwa jeshi letu halina mahusiano mazuri na wananchi wake huu sio ujambzi Juli swala lina sura mbili moja ni ulipaji wa kisasi lingne ugaidi baridi .we need to be extra careful kinachoendelea kwa Joseph kabila kilianza hivi hivi
 
Kwa kuwa wanaua askari na viongozi bila kuiba chochote zaidi ya silaha,huoni kuna haja ya kuwakamata wakiwa hai ili kujua lengo lao na mbinu zao?
Ni kweli kuwa uwa sio suluhisho ni sawa na kutibu malaria pasipo kujua chanzo cha malaria kwa kutbu malaria utatumia nguvu nyngi ni bora utafute chanzo cha malaria na sawli la kujiuliza hawa watu baada ya kuuwa hawachukui chochote we need to think in advance
 
N swali lingine ni kwanini wananchi hawaipi ushirikiano polisi kwa nini wawe upande wa wauaji?
Waache hao wananchi wasiotaka kutoa ushirikiano kwa polisi ili baadae waisome namba. Kwani unazani hao wanaokusanya silaha wanataka kuzitumia dhidi ya nani kama sio wao wananchi. Kuna mambo ya kushabikia lakini sio mauwaji ya askari.
 
Umeweka bandiko la kiwango cha juu mno ! Nadhani huu ndio uzi pekee fikirishi tangu mauaji ya polisi wetu yatokee .

Binafsi nilivyowaona na kuwasikia viongozi wa polisi , ni kama wanataka kulipa kisasi tu , haionekani dalili ya kuja na majibu na kukomesha hali hii, wamejaa chuki na vitisho , kiukweli jambo hili linahitaji busara na weledi mkubwa sana .
Sasa mkuu, ni kweli ulitegemea mkakati rasmi wa kiusalama wa kushughurikia suala hili ubainashwe hadharani, mbele ya press au msibani? Suala hili ni nyeti na amini usiamini sio Polisi tu bali vyombo vyote vya kiusalama vya Taifa sasa hivi vimo kazini usiku na mchana ila tu tukumbuke ugumu wa kupambana na adui anayepigana nawe kwa mtindo wa HIT & RUN.
 
6.Mabadiliko hakuna,maana wao wanaweza kuwa wanataka kuanzisha tawala zao zile kama Ninawi,mosoul,raqqa nk,kwa utawala wa kawaida ni ngumu kukaa nao zaidi ya kuwashughulikia tu
5.Maafisa wa serikali hawana makosa yyte,but adui yao namba moja ni mtu au mtumishi anaeunga mkono serikali iliyopo madarakani,kwa hiyo ni suala la kitaifa zaidi,kama wwe ni mtz wa mlengo wa kati hili linakuhusu,siadi nchi yako
4.Wanaofurahi ni wale wanaoona kuwa wanaweza Ku -exist kwenye utawala huo,ie ukiiba unakatwa mkono,ukizini unapigwa mawe mpka ufe,na mengineyo,lakini wakumbuke kabla ya kushangilia watafute taarifa hizi,je walioko Raqqa wana kitu cha maana sana wanachokipata?
3.Kama ni kweli ni hao wanaojiita wenye msimamo mkali kitu cha kuangalia,nchi ambazo walikuwepo hawa jamaa kama Syria, Iraq,Libya na kwa Jirani zetu Somalia hakuna uhakika wa watu hawa kuwepo,maana mashambulizi ya nchi za magharibi ni makubwa,lakini pia hawala zao zimeanza kupoteza nguvu hasa Mosoul,Raqqa,Ninaw,Sirte na Somalia, kwa hyo Upo uwezekano wakawa wamekimbilia huku.
2.Kuteka na kuua polisi nane si kazi ya mtu mmoja,jeshi letu si dhaifu kiasi cha kutekwa na mtu mmoja,
1.Hawa jamaa wanajipanga,swali rahisi,silaha wamechukua za nn?
Note: Tuwasaidie polisi, wakitoka kwao sisi hatuko salama!
 
Back
Top Bottom