Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

Hili la kuhamia Dodoma lilihitaji mtu mwenye msimamo kwakuwa bunge lipo Dodoma alafu serikali ipo Dar hata ukipiga gharama ya usafiri toka enzi ya NYERERE mpaka leo gharama iliyotumika ni kubwa sana bado mahitaji mengine kama malazi na chakula,tuache kubeza hata mambo ambayo hata yasipoleta faida kwetu yataleta kwenye vizazi vijavyo.
 
Anatekeleza ombi la watumishi kupitia TUCTA walilolitoa kwa jpm kwny Mei mosi
 
WAKATI watumishi wa umma wakikuna vichwa, kuhusu maagizo yaliyokwishatolewa na yanayoendelea kutolewa ya kutakiwa kuhamia Dodoma mara moja, taarifa zinaonesha kuwa gharama za kuhamia na kuishi, si kubwa kama inavyodhaniwa.

Tathmini ya awali ya gazeti hili imeonesha kuwa hofu kubwa ya watumishi hao ni gharama za kuanza makazi mapya hasa nyumba na huduma za starehe na mapumziko baada ya kazi na wakati wa mwisho wa juma.

Pia imebainika gharama nyingine ni mazoea tu, kwa kuwa huduma nyingi zikiwemo za chakula na usafiri, vimeonesha kuwa ni nafuu kwa mkoa huo, ikilinganishwa na mkoani Dar es Salaam.

Takwimu za Gharama za Maisha (CPI) za Juni mwaka huu, zinaonesha kuwa sehemu kubwa ya kipato cha Watanzania sawa na asilimia 38, hutumika katika chakula huku hoteli na migahawa ambayo hutoa huduma hizo pia, pamoja na nyinginezo ikichukua asilimia 4.2 ya kipato cha Watanzania na kwa Dodoma huduma hizo ni rahisi kuliko Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizopo katika tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), usafiri na usafirishaji ndio huduma ya pili kwa kuchukua sehemu kubwa ya kipato cha Watanzania sawa na asilimia 12, lakini haihofiwi katika kuhamia Dodoma.

Usafiri umefuatiwa na huduma za nyumba na makazi pamoja na huduma ambatanishi za maji, umeme, gesi na nishati nyingine, ambazo huchukua asilimia 11.6 ya kipato hicho, ingawa ndio vinavyohofiwa zaidi na wanaosubiri maagizo ya kuhamia Dodoma.

Kutokana na uhalisia huo wa asilimia 60 ya kipato cha Watanzania kutumika katika chakula, usafiri na usafirishaji na nyumba, tathmini ya gazeti hili imefanikiwa kupata taarifa kuhusu namna mtumishi anavyoweza kupata huduma hizo kwa urahisi akiwa Dodoma.

Nyumba

Ingawa jambo la kwanza ambalo watumishi wengi wanaotarajiwa kwenda Dodoma, hasa wanaomiliki nyumba zao jijini Dar es Salaam, wana hofu kubwa ni gharama za nyumba, tathmini ya gazeti hili imebaini zipo nyumba za bei rahisi kuliko za Dar es Salaam.

Tathmini hiyo imeonesha kuwa eneo lenye nyumba za gharama ya chini kabisa ni Mlimwa C, ambako huduma ni za vyumba badala ya nyumba nzima. Katika eneo hilo la Mlimwa C, kuna nyumba za bei ya chini kabisa lakini za tope, ambazo hata hivyo zimeezekwa kwa bati na zina umeme. Kodi ya chumba kimoja ni Sh 15,000.

Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Prosper Ganyala, alisema mbali na urahisi huo wa kodi, kutoka eneo hilo kwenda mjini ni kilometa tano tu.

Kwa mujibu wa Ganyala, pia kuna nyumba za matofali ya saruji, ambayo kodi ya chumba kimoja ni Sh 25,000 na anayetaka chumba na sebule, kodi ni Sh 35,000 lakini choo na maliwato viko nje ni vya kushirikiana wapangaji wote.

Eneo lingine lenye makazi ya bei nafuu, ni Area A ambako kodi ya chumba kimoja kwa nyumba ya kawaida, imetajwa kuwa ni Sh 30,000 kwa mwezi hadi 50,000 kulingana na hadhi ya nyumba.

Mkazi wa Area A, Nazael Mkuse amesema kodi hizo hutegemea aina ya nyumba na idadi ya vyumba vilivyo katika nyumba hiyo na kama mteja atataka nyumba nzima, atahesabiwa idadi ya vyumba vilivyopo.

“Maeneo haya chumba na sebule ni Sh 100,000 lakini vyoo huwa vya kuchangia na mitaa ya huku bado haina lami na inamlazimu mpangaji kutembea umbali wa kama robo saa hivi, ili kufika stendi ya mabasi ya kwenda mjini,” alisema.

Eneo lingine la nyumba za gharama nafuu, ni Maili Mbili, ambako imeelezwa kuwa nyumba nyingi zinapangisha vyumba badala ya nyumba nzima, ambapo chumba kisicho na dari (ceiling board), chenye sakafu ya kawaida, umeme na maji, kodi ni Sh 30,000 hadi 35,000, huduma za umeme na maji za kuchangia.

Nyumba bei juu

Akizungumza na gazeti hili wiki hii dalali wa nyumba na viwanja, Merere Yusuph, alisema nyumba za gharama za kati na juu zipo ingawa zinatofautiana kwa hadhi na bei.

“Nyumba nyingi Dodoma zina hadhi ila inategemea iko eneo gani, kukaa Kisasa, Uzunguni, Area D na Area C inategemea na hali ya mfuko wako ilivyo. “Kodi katika maeneo hayo huanzia Sh 300,000 kwa mwezi kulingana na ukubwa wa nyumba na kuendelea. Zina vyoo na maliwato ndani na nyingine zina chumba cha kulala chenye choo na maliwato ndani,” alisema.

Alitoa mfano wa nyumba za Chang’ombe Extension, kuwa zimejengwa kwa ramani na mpangilio mzuri, ambako zipo zenye uzio na zisizo na uzio na kodi huwa maelewano kati ya mwenye nyumba na mpangaji.

“Isiyo na uzio wanaanzia Sh 100,000 hadi 200,000 kwa mwezi na yenye uzio huanzia 200,000 hadi 350,000,” alisema.

Katika eneo la Kisasa, alisema kuna nyumba zenye maduka ya biashara na nyingine za ghorofa zenye huduma za starehe, ikiwemo eneo kubwa la kuegesha magari, bustani mpaka mabwawa ya kuogelea.

“Nyumba katika maeneo hayo, kodi huanzia Sh 400, 000 kwa mwezi na kuendelea na zenye mabwawa ya kuogelea bei huwa ni mapatano,” alisema.

Alipoulizwa hali ya wateja ikoje katika shughuli hiyo ya udalali wa vyumba na nyumba za kuishi, alisema tangu suala la kuhamia Dodoma lionekane halina mbadala, amekuwa akipata ofa nyingi za wakazi wa Dar es Salaam wanaotaka nyumba za kuishi na wengi wao wanataka nyumba nzima.

Usafirishaji

Huduma nyingine inayochukua sehemu kubwa ya gharama za maisha kwa Watanzania ni usafiri na usafirishaji, ambao hata hivyo watumishi wengi wa serikali hawaihofii katika suala la kuhamia Dodoma, kama wanavyoumiza kichwa kuhusu makazi.

Hata hivyo kutokana na umuhimu wake katika maisha ya watu na hasa watumishi, gazeti hili lilizungumza na madereva wa teksi na bodaboda.

Dereva teksi, Mussa Amiri alisema maeneo ambayo wamekuwa wakipata wateja kutoka mjini kwenda huko na kutoka huko kurudi mjini ni Nzuguni, Nkuhungu na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambako wanaoishi ni watu wa kipato cha kati na juu.

Kwa mujibu wa Amiri, kutoka mjini Dodoma kwenda Kisasa bei huwa ni Sh 10,000 hadi 12,000 kulingana na umbali na kwenda Nzuguni bei huwa Sh 15,000 hadi 20,000.

Alisema unapopeleka abiria katika maeneo ya Nkuhungu, bei huwa si chini ya Sh 7,000 na mtu akitaka kufika Udom, atalazimika kulipa kuanzia Sh 15,000 na kuendelea kulingana na umbali anaokwenda. “Kwenye maeneo yenye barabara za vumbi bei huongezeka,” alisema.

Taarifa zinaonesha katika maeneo ambayo gharama za makazi ziko chini kama Mlimwa C na Area A, ni nadra kupata wateja wa teksi na mara nyingi, wanaotoa huduma za usafiri ni bodaboda.

Hata hivyo, huduma hiyo ya usafiri wa pikipiki, taarifa zinaonesha kuwa zimesambaa katika maeneo mengi ya mji na bei hutegemeana na umbali wa eneo husika. Kwa maeneo yaliyo karibu bei huwa Sh 1,000 hadi Sh 2,000 na kwa maeneo ya mbali bei huwa kati ya Sh 5,000 na kuendelea.

Mmoja wa waendesha pikipiki, Yusuph Kimani alisema kupeleka abiria maeneo ya Nzuguni ni Sh 6,000 hadi 10,000; kulingana na umbali na wale wanaoenda Mkuhungu, Area C, Area D, Uzunguni bei huwa Sh 3,000 hadi Sh 4,000.

Vyakula, migahawa

Ingawa chakula na vinywaji visivyo na vilevi ndio huduma na bidhaa zinazochukua sehemu kubwa ya kipato cha Watanzania, lakini cha ajabu si miongoni mwa hofu za watumishi wa umma, katika gharama za kuhamia mkoani humo.

Akizungumza na gazeti hili mkazi wa Dodoma, Edina Mkopi alisema migahawa mingi imekuwa na bei tofauti tofauti za vyakula. Katika baadhi vyakula huanzia Sh 7,000 na mingine Sh 14,000 kwa mtu mmoja, lakini iko mingine wakiwemo mama lishe ambao vyakula huanzia Sh 1,500 hadi kati ya Sh 3,000 na 4,000.

Kuhusu upatikanaji wa vyakula kwa ajili ya kupika majumbani, taarifa zinaonesha ni mzuri na bidhaa za vyakula ni za bei nafuu kuliko Dar es Salaam kutokana na kuzungukwa na mikoa ya wakulima.

Starehe

Jambo la nne miongoni mwa mambo matatu yanayohofiwa na watumishi wa umma katika kuhamia Dodoma, mbali na nyumba, chakula na usafiri ni maeneo ya kupumzika na starehe.

Ingawa takwimu za NBS zinaonesha kuwa starehe na masuala ya utamaduni huchukua asilimia 1.6 tu ya kipato cha Watanzania na unywaji wa vilevi na utumiaji wa bidhaa za tumbaku huchukua asilimia 3.7 tu, lakini mambo hayo yanatajwa kuwa moja ya hofu kubwa za watumishi katika kuhamia Dodoma hasa vijana.

Gazeti hili lilipita maeneo ya klabu za usiku, ambako kuna matumizi makubwa ya vinywaji na starehe, ambapo ilibainika kuwa zimekuwa zikipata wateja wengi wakati wa vikao vikubwa kama Bunge na mikutano ya CCM tu.

Mkazi wa Dodoma, Emmanuel Mbaule, anayejishughulisha na biashara ya vinywaji vyenye vilevi, alisema klabu hizo huwa na watu wengi hasa kipindi cha Bunge ambapo Dodoma huwa na msongamano mkubwa wa watu, lakini baada ya Bunge wateja ni wachache.

“Sasa ukienda klabu wateja hawafiki hata 50 tena siku za mwisho wa juma kwa siku za kawaida unaweza kukuta watu hata watano,” alisema.

Hata hivyo Mbaule alisema klabu nyingi za usiku, zinahitaji marekebisho maana nyingi hazikidhi vigezo vya kisheria. Alitoa mfano wa vilabu hivyo kukosa vyumba vya kuvutia sigara na milango ya dharura, huku maeneo ya klabu yakiwa finyu.

Kuhusu baa ambazo pia zimekuwa zikitoa huduma za starehe, mapumziko na kuuza vilevi na bidhaa za tumbaku, Mbaule ambaye ni mwakilishi wa mauzo ya vinywaji hivyo Kanda ya Kati, alisema Dodoma kuna baa zaidi ya 156 lakini nyingi ziko kwenye makazi ya watu.

Maeneo ya kupumzika

Maeneo mengine ya kupumzika mbali na baa na klabu za usiku, ambayo kwa Dar es Salaam ni pamoja na katika fukwe za bahari, imeonekana kuwa mkoa huo wa Dodoma yatakuwa na changamoto kubwa.

“Dodoma haina maeneo mengi ya kupumzikia zaidi ya pale Mashujaa na Viwanja vya Nyerere, serikali ilione na hili ni kitu muhimu,” alisema mkazi wa Dodoma, Beatrice Chinyuka. Alisema maeneo hayo pia yanahitaji kuboreshwa kwa usafi maana hata viti vilivyopo ni vile vilivyojengwa kwa kutumia saruji.

Habari Leo
 
isipohamia leo itaenda lini,wanaolalamika kwamba haikujadiliwa bungeni ndio hao wanaosusuia vikao kila siku, wanataka kujadili nini,ni kwamba watu walikua hawajui kwamba serikali inapaswa kua dodoma au ni uzembe uliopitiliza kiasi kwamba mtu akifanya kitu sahihi ambacho hakijazoeleka tunaona kama tunaonewa????aliesema anahamisha serikali yake kwenda dodoma kwani hajui kwamba hela atapata wapi mpaka asemhivo?sijui hela atatoa wapi na staki kujua watu watahamaje cha msingi serikali ihamie dodoma,avunje au asivunje katiba vyote sawa tu naunga mkono maana ina manufaa.....lazima tabaka fulani likubali maumivu ili tupige hatua....hata marekani haikufika hapo ilipo kirahisi hivyo kama tunavyotaka sisi lazima maamuzi magumu yafanyike twende mbele
 
Hakuna anayepinga kuhamia dodoma. Ila watu wanapinga kukimbilia dodoma ili hali kule hakuna 'facilities' za kuwapokea wanaoenda.
Wamekurupuka.
 
Kamwe Marekani haikuwahi na haitatokea iwe na maamzi ya kimwendokasi bin kukurupuka namna hii.
Huyu mtu asipofungwa speed gavana atajikuta anapiga jaramba hadi mwishwo wa ungwe...
 
Wakuu amani ya Muumba iwe juu yenu.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na mjadala kuhusu serikali kuhamia dodoma. Binafsi nadhani ni jambo jema haswa ukizingatia kuwa ni swala amablo lilishakuwepo toka kipindi kirefu nyuma.

Hata hivyo kama mtanzania wa kawaida kuna maswali najiuliza na sipati majibu hivyo nimeona nijaribu kuyaleta hapa ili kupata udadavuzi mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali

1: Neno serikali,kwa mujibu wa muktadha huu wa kuhamia dodoma ni kitu gani hasa? Yani ni wizara tu, idara tu, au wanamaanisha nini wanaposema serikali? Ili kueleweka vizuri nitatoa mfano. Wiza ya elimu ikihamia dodoma,taasisi zilizo chini yake kama vile NECTA, NACTE, TCU nk zitahama ama la?

Je, zisipohama hiyo wizara huko dodoma itakuwa inafanyaje kazi ili hali taasisi zake nyingi zitakuwa darisalama? Vivyo kwenye sekta nyingine kama viwanda na biashara -tbs, nk? Hapa naomba ufafanuzi mpana kidogo, ili tujue nai anahama nani hahami.

2: Je, kumetokea nini mpaka kuhama huku kuharakishwe namna hiyo?

3: Je, serikali imetafakari juu ya athari ya zoezi hili kwa ughafla huu? Kuna baadhi ya taasisi za serikali zimepangisha majengo kutoka kwa wadau mablimbali, na kuna mikataba wameingia na wapangishaji hao, Je serikali imliangalia hilo na athari za kuvunja hiyo mikata?

Je, serikali imeangali wazabuni katika tenda mabimbaili inazpata na kuangalia athari ya kuhamia dodoma kwa ishu za zabuni hizo? Je kampuni zenye kutoa huduma za ulinzi na usafi(mfano tu) zitakubali kuendelea kutoa huduma hizo dodoma na kwa makubaliano yapi?

4: Kwakuwa viongozi wakubwa waserikali wana makazi madogo dodoma na kwao haina athari sana kuhama, Je wamehakikisha kuwa wafanyakazi wote watapata makazi dodma maeneo pia mabayo hayataathiri ufanisi wao?

5: Binadamu anaitaji kujiandaa kisaikolojia zaidi kuliko kifedha na muda ni jambo muhimu katika kufanikisha hili, Je serikali imewaanda watumishi wake kisaikolojia juu ya wao kuhamia dodoma? Kwa muda mfupi watakaokuwa nao watuishi, serikali haini kuwa inaweza kunaweza kuwa na mtizamo mbaya wa zoezi hili kwa watumishi wake?

Je, wakihama, kwa muda mfupi huu watawezaje kuacha makazi ya salama? Uimara wa familia je? Hivi serikali haioni kuwa kuna uwezekano wa watumishi kuomba ruksa za mara kwa mara kwenda kuweka mambo ya kifamialia sawa pale ambapo watahama kwa muda mfupi bila ya wao kujiandaa vizuri?

6: Hivi serikali haikuona kuwa kuweka zoezi hili ndani ya muda mfupi kunaweza sababisha gharama za maisha dodoma kuongezeka sana kwakuwa kutakuwa na ongezeko la ghafla la mahitaji bila ya kuwa na ongezeko sawa la usambazaji? Mathalani kodi katika nyumba zitapanda sana,je hilo serikali imeliangaliaje?

7: Majengo yakokuwa yanatumiwa na serikali dar yatatumika kwa utaratibu gani haswa ukizingatia kutakuwa na kuondoka kwa ghafla?

8: Kauli ya mh raisi ilikuwa kuhamia dodoma ndani ya miaka hii minne, Je kama wizara zinahama ndani ya mwezi, kulikuwa na ulazima kweli wa kufanya hivyo?

9: Kwakuwa bajeti ilishapitishwa, ni kutoka fungu gani ambalo serikali italitumia katika kufanikisha zoezi hilo?

10: Kwakuwa serikali inafanya kazi na wadau mablimbali, ni kwanamna gani imejipanga kuhakiksha kuwa kuhama kwake hasa huku kwa muda mfupi hakutaathiri ushirikishwaji wa wadau hao katika nyanja mbalimbali? Kwamfano mabalozi, taasisi na mashirika ya imataifa nk.

NB: Tafadhali tuache ushabiki na tujikite kwenye hoja. Ingependeza kama ungejibu baadhi ya hoja(kama una majibu) ama ukaongeza maswali(kama unayo pia) ili mwisho wa siku tupate uelewa mpana wa hii dhana ya serikali kuhamia dodoma. Nawasilisha

ONDOA HOFU BRAZA, WATAHAMA KWA UTARATIBU MARIDHAWA. KUMBUKA JP. ALISEMA SERIKALI ITAHAMA KTK KIPINDI KILOCHOBAKIA CHA MIAKA MINNE NA MIEZI MICHACHE. KWASASA NI BAADHI TU YA VITENGO NA WATUMISHI WAANDAMIZI WATATANGULIA. HIVYO FANYA ASSESSMENT YAKO MWAKA 2019 DISEMBA NDIO UTAKUWA UMEJUA HALI ILIVYO. KWASASA MJADALA HAUSADII KWANI AGIZO LISHATOKA.

HATA HIVYO MAZINGIRA YA DODOMA NI MAZURI TU, VIWANJA KWA AJILI YA OFISI ZA SERIKALI VIPO VYA KUTOSHA NA MAKAZI VITAPIMWA VINGI TU. CDA ILIANZISHWA KWA SABABU HIYO.
 
Tanzania Tanzania!

Taarifa za kuhamia Dodoma zilipotolewa ilionekana tumechelewa na niliamini ili tusizidi kuchelewa Wizara kadhaa zingekuwa tayari Dodoma. Kumbe nilikuwa najidanganya.

Naiomba Serikali iseme kuanzia lini Wizara zitaanza kuhamia Dodoma ili watanzania wajue.
 
Julius Nyerere tangu aazimie kuhamia Dodoma 1966 na kupitisha Azimio la Bunge 1973 mpaka anaondoka Madarakani 1985 hakuweza kuhamisha hata Wizara moja. Aliwahi kujaribu kuhamisha Wizara ya Mambo ya Nje lakini alipopelekewa Mchanganuo wa Bajeti yake aliufyata.
Kigezo pekee cha kupanga Dodoma kuwa Makao Makuu ilikuwa ukati kati wake pekee hawakutazama Ujangwa wala kupitiwa kwake na Bonde la Ufa ambacho ni kikwazo kikuu kwa ujenzi Mkubwa mkubwa.
Kwa Hili Magu kaharakisha kama alivyokurupuka MwlNyerere.
Angalau Mzee Mwinyi alijaribu kuukuza Mji wa Dodoma kwa kuifanya kuwa Tax havens ambapo ukiwekeza na kuzalisha Dodoma unalipa nusu ya kodi na hata utility ya Umeme na maji iliazimiwa ilipwe nusu bei japo utekelezaji wake nao haukufanikiwa.
Haikuandikwa Mbinguni kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Tanzania, ni utashi tu wa Mtu mmoja kwa tamaa zake za kumfurahisha Mgogo wake leo inaligharimu Taifa na watu wake!
Mkapa alithubutu kibusara kwa kulipeleka Bunge nako hapakuchangamka.
Jakaya alijaribu kupeleka Udom nako hapakuchangamka.
Dodoma ipo kuzalisha Omba omba tu na Wagonjwa wa Macho Nyerere kwa utashi wake kaigeuza Washington ya Tanzania ikamshinda
 
Kuhamia dodoma mchezo??? Hiyo pesa ipo...?? Walikurupika ki-mwendokasi alaf wamebuma ki-mwendokasi
 
Back
Top Bottom