Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

HILI NALIUNGANISHA NA KAULI YA MH. SUGU "SERIKALI INAENDESHWA KWA MZUKA".....HAIWEZEKANI RAISI ASEME NDANI YA MIAKA MI4 NA MIEZI MI4 ATAKUWA KAHAMIA DODOMA...MARA UNAWASIKIA WASAIDIZI WAKE WOTE WANAHAMIA DODOMA NDANI YA MWEZI MMOJA.

"MZUKA AT WORKS......"
ni mizuka tuu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Maswali yako hayo mengi yanaakisi uwezo wako wa kushughulisha akili ni mdogo sana, haiwezekani uwe na maswali mengi kama hayo ambapo yote hujapata majawabu.
Any way jua tu kwamba serikali ni zaidi ya majibu ya hayo maswali, lisilowezekana akilini mwako linawezekana serikalini.
 
Binafsi mpaka sasa bado natafakali kwanini waziri mkuu wakati wa bunge la budget hakutoa taarifa ya yeye kuhamia Dodoma mapema Kama alivyosema!!!! Tafakari yangu ni kuhusu pesa za watumishi wa ofisi za waziri mkuu kuhamia huko wiki ijayo na wengine wengi watafuta, wataishi kwa pesa ipi? Imepitishwa na bunge lipi? Navyojua kuna mkusanya pesa na kuna mpanga matumizi ya hizo pesa then kuna mpitisha matumizi ya pesa zote yaani bunge.

Kuna mwaka Sumaye akiwa waziri Mkuu alitangaza kuhamia Dodoma lakini sijui nini kilitokea akarudi Dar. Ngoja tuone mwisho wa hii Sinema
 
Kwa Maoni yangu Sio lazima serikali yote ihamie dodoma namaanisha wizara...hakuna haja ya wizara inayohusika na viwanda kwenda domu wakati viwanda ving vipo dar,wizara ya madini&nishati hii ingeenda hata Mwanza ule ndo ukanda wenye madini,Wizara ya kilimo peleka hata mbeya kusini wanalima sana,Dodoma pale zingekaa wizara chache kama tamisemi/ajira na utumishi kwan ni katikati nani rahisi kufikika,Je izo nyumba za wafanyakazi zipo au ndo kwenda kukaa guest nakuingizia nchi gharama ambazo hazina msingi...
Mkuu kwahiyo unapendekeza wizara zitawanywa kulingana na eneo ambako shughuli zinafanyika huko?
 
Maswali yako hayo mengi yanaakisi uwezo wako wa kushughulisha akili ni mdogo sana, haiwezekani uwe na maswali mengi kama hayo ambapo yote hujapata majawabu.
Any way jua tu kwamba serikali ni zaidi ya majibu ya hayo maswali, lisilowezekana akilini mwako linawezekana serikalini.
Ndio maana nikaleta hapa ili wenye.uwezo mkubwa mtusaidie,mbona hujajibu hata moja sasa?
 
Magufuli yupo serious sana na ahadi zake waliombeza haiwezekani kuamia Dodoma ndio hao hao wanapoona inawezekana wanalia lia machozi.
Mkuu tunamsapoti ila kwa uharaka wa namna hii? Je hayo.maswali yanajibika.kirahisi?
 
Kwanza niseme siyo ghafla kama wengi wanavyo sema. mpango wa kuhamia Dodoma ulikuwa ni wa serikali, na ulitangazwa mwaka 1975.Kimsingi ni mpango mzuri kwani Dodoma ni katikati ya Nchi, kwahiyo mikoa mingi itapata huduma kwa urahisi.

Kuhusu nani anatakiwa kuhamia Dodoma ikiwa serikali inahamia huko, ni kwamba, Kwanza Rais lazima ahamie. maana yake ni kwamba ikulu itahamia Dodoma.Kama hivyo ndivyo, maana yake nyingine ni kwamba kikiosi cha ulinzi wa Rais kinahama.Wengine ambao lazima wahamie Dodoma kwa maana hiyo ni Usalama wa Taifa, polisi, Makao makuu ya JWTZ, na Wizara zote.

Wizara zina idara lazima zihame.ila vitengo kama ulivyo sema NECTA,NACTE,HESLEB nk siyo lazima sana wahame sasa.Ila ili kuwarahisishia watu kupata huduma muhimu sehemu moja, huko mbeleni hata vitengo hivyo vitahamia Dodoma! Ama kuhusu mikataba mbalimbali hiyo haina maana sana kwasababu ni vitu vinavyo zungumzika.Kifupi ni kwamba hakuna jambo lisilo na Changamoto zake! mwanzo mgumu lakini huko mbeleni kuna faida nyingi makao makuu ya serikali kuwa Dodoma kuliko Dar es salaam.

Mkuu ahsante sana kwa ufafanuzi.mzuri. Ila nadhani bado.maswali.ni mengi kuliko majibu. Mpango wa kuhamia ulikuwepo toka zamani.lakini ni kama ilisimama sana. Kulikuwa na ulazima gani wa kusababisha athari nyingi zisizo na ulazima?
 
Binafsi mpaka sasa bado natafakali kwanini waziri mkuu wakati wa bunge la budget hakutoa taarifa ya yeye kuhamia Dodoma mapema Kama alivyosema!!!! Tafakari yangu ni kuhusu pesa za watumishi wa ofisi za waziri mkuu kuhamia huko wiki ijayo na wengine wengi watafuta, wataishi kwa pesa ipi? Imepitishwa na bunge lipi? Navyojua kuna mkusanya pesa na kuna mpanga matumizi ya hizo pesa then kuna mpitisha matumizi ya pesa zote yaani bunge.
Mkuu hilo ni swala gumu kujibiwa. Kiuchumi matumizi ya serikali yanapaswa kufuata misingi kadhaa ikiwemo principle ya sanction, yani matumizi yoyote ya.serikali lazima yaidhinishwe.na chombo.chenye.mamlaka wakufanya hivyo kama bunge kwa serikali kuu. Sasa je matumizi.yatakayofanyika kwenye hilo zoezi yamezingatia hiyo.princie?
 
Baada ya kuhama nadhani itakuwa muda muafaka wa majengo yao kugeuzwa viwanda.
 
Mkuu ahsante sana kwa ufafanuzi.mzuri. Ila nadhani bado.maswali.ni mengi kuliko majibu. Mpango wa kuhamia ulikuwepo toka zamani.lakini ni kama ilisimama sana. Kulikuwa na ulazima gani wa kusababisha athari nyingi zisizo na ulazima?
Kimsingi hakuna wakati ambao ni very ideal! hata NIGERIA wakati wanahamisha serikali wananchi walihofu sana lakini ni uoga usio na sababu. kiusalama Dodoma is the best, kiuchumi kwa maana ya kufikika kiurahisi na watu mikoa yote Dodoma is the best.Gharama haziepukiki lakini zisitufanye kurudi nyuma.
 
Wakuu amani ya Muumba iwe juu yenu.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na mjadala kuhusu serikali kuhamia dodoma. Binafsi nadhani ni jambo jema haswa ukizingatia kuwa ni swala amablo lilishakuwepo toka kipindi kirefu nyuma.

Hata hivyo kama mtanzania wa kawaida kuna maswali najiuliza na sipati majibu hivyo nimeona nijaribu kuyaleta hapa ili kupata udadavuzi mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali

1: Neno serikali,kwa mujibu wa muktadha huu wa kuhamia dodoma ni kitu gani hasa? Yani ni wizara tu, idara tu, au wanamaanisha nini wanaposema serikali? Ili kueleweka vizuri nitatoa mfano. Wiza ya elimu ikihamia dodoma,taasisi zilizo chini yake kama vile NECTA, NACTE, TCU nk zitahama ama la?

Je zisipohama hiyo wizara huko dodoma itakuwa inafanyaje kazi ili hali taasisi zake nyingi zitakuwa darisalama? Vivyo kwenye sekta nyingine kama viwanda na biashara -tbs, nk? Hapa naomba ufafanuzi mpana kidogo, ili tujue nai anahama nani hahami.

2: Je kumetokea nini mpaka kuhama huku kuharakishwe namna hiyo?

3: Je serikali imetafakari juu ya athari ya zoezi hili kwa ughafla huu? Kuna baadhi ya taasisi za serikali zimepangisha majengo kutoka kwa wadau mablimbali, na kuna mikataba wameingia na wapangishaji hao, Je serikali imliangalia hilo na athari za kuvunja hiyo mikata?

Je serikali imeangali wazabuni katika tenda mabimbaili inazpata na kuangalia athari ya kuhamia dodoma kwa ishu za zabuni hizo? Je kampuni zenye kutoa huduma za ulinzi na usafi(mfano tu) zitakubali kuendelea kutoa huduma hizo dodoma na kwa makubaliano yapi?

4: Kwakuwa viongozi wakubwa waserikali wana makazi madogo dodoma na kwao haina athari sana kuhama, Je wamehakikisha kuwa wafanyakazi wote watapata makazi dodma maeneo pia mabayo hayataathiri ufanisi wao?

5: Binadamu anaitaji kujiandaa kisaikolojia zaidi kuliko kifedha na muda ni jambo muhimu katika kufanikisha hili, Je serikali imewaanda watumishi wake kisaikolojia juu ya wao kuhamia dodoma? Kwa muda mfupi watakaokuwa nao watuishi, serikali haini kuwa inaweza kunaweza kuwa na mtizamo mbaya wa zoezi hili kwa watumishi wake?

Je wakihama, kwa muda mfupi huu watawezaje kuacha makazi ya salama? Uimara wa familia je? Hivi serikali haioni kuwa kuna uwezekano wa watumishi kuomba ruksa za mara kwa mara kwenda kuweka mambo ya kifamialia sawa pale ambapo watahama kwa muda mfupi bila ya wao kujiandaa vizuri?

6: Hivi serikali haikuona kuwa kuweka zoezi hili ndani ya muda mfupi kunaweza sababisha gharama za maisha dodoma kuongezeka sana kwakuwa kutakuwa na ongezeko la ghafla la mahitaji bila ya kuwa na ongezeko sawa la usambazaji? Mathalani kodi katika nyumba zitapanda sana,je hilo serikali imeliangaliaje?

7: Majengo yakokuwa yanatumiwa na serikali dar yatatumika kwa utaratibu gani haswa ukizingatia kutakuwa na kuondoka kwa ghafla?

8: Kauli ya mh raisi ilikuwa kuhamia dodoma ndani ya miaka hii minne, Je kama wizara zinahama ndani ya mwezi, kulikuwa na ulazima kweli wa kufanya hivyo?

9: Kwakuwa bajeti ilishapitishwa, ni kutoka fungu gani ambalo serikali italitumia katika kufanikisha zoezi hilo?

10: Kwakuwa serikali inafanya kazi na wadau mablimbali, ni kwanamna gani imejipanga kuhakiksha kuwa kuhama kwake hasa huku kwa muda mfupi hakutaathiri ushirikishwaji wa wadau hao katika nyanja mbalimbali? Kwamfano mabalozi, taasisi na mashirika ya imataifa nk.

NB: Tafadhali tuache ushabiki na tujikite kwenye hoja. Ingependeza kama ungejibu baadhi ya hoja(kama una majibu) ama ukaongeza maswali(kama unayo pia) ili mwisho wa siku tupate uelewa mpana wa hii dhana ya serikali kuhamia dodoma. Nawasilisha
Hahaha hahaa umetisha
 
Selikali ya magufuri kuhamia dodoma
Nimeanza kuliskia hili swala toka wakati wa kikwete ila kama watu wa Tanzania tunatakiwa kuhoji jee uhamiaji wa dodoma una maslai gani kwa nchi
Je kuna kitu katika uwajibikaji kitaongezeka au twafanya maigizo
Je dodoma ndoo mharubaini wa matatizo yetu kama nchi
Je gharama za kuhamia dodoma zinatoka wapi kama ni selikalini ziliptishwa na bunge
Hili wazo limeanza siku nying jee kwa nini selikali ilikuwa inajenga baadhi ya ofisi za wizara aukuwa wakijua kuwa kuna kuhamia dodoma.
Tujadili kwa manufaa ya nchii
 
Ndo kipaumbele cha serikali awamu ya tano
 
Ni kuhamia tu sasa, mjadala baada ya zoezi hilo. HAPA KAZI TU!
 
Iweje mji mkuu wa nchi uongozwe na RC aibuu kama hutaki imekuuma sana hamia sudan
 
Selikali ya magufuri kuhamia dodoma
Nimeanza kuliskia hili swala toka wakati wa kikwete ila kama watu wa Tanzania tunatakiwa kuhoji jee uhamiaji wa dodoma una maslai gani kwa nchi
Je kuna kitu katika uwajibikaji kitaongezeka au twafanya maigizo
Je dodoma ndoo mharubaini wa matatizo yetu kama nchi
Je gharama za kuhamia dodoma zinatoka wapi kama ni selikalini ziliptishwa na bunge
Hili wazo limeanza siku nying jee kwa nini selikali ilikuwa inajenga baadhi ya ofisi za wizara aukuwa wakijua kuwa kuna kuhamia dodoma.
Tujadili kwa manufaa ya nchii

Nawaonea huruma watu wa Dar. Mlizoea kuishi kijanjajanja kwa kutumia bandari na Dili feki serikalini .... Sasa serikali imeziba mianya na inamfuata MATONYA mliyemlalamukia kuwa anawachafulia JIJI .

Je, kwa jinsi mlivyokuwa rojorojo mtasurvive kweli?????? Mnaweza kurudi kijijini mlime Kama sisi? Badilikeni na acheni kulalamika lalamika .... Mbona hujawaza kuuliza NI KWANINI SERIKALI ILIWEKWA DAR KWA MUDA MREFU JAPOKUWA MJI MKUU UNAJULIKANA KUWA NI DODOMA????

Jibu kuhusu gharama: ZINATUHUSU WEWE NA MIMI. Kaza buti tuzifidie ili tufanikishe Hilo zoezi muhimu!

NUKTA.
 
kama huna hilo buti utakaza nini?
 
Back
Top Bottom