Maswali mengine yanaboa kwa kweli

Maswali mengine yanaboa kwa kweli

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
62,099
Reaction score
127,838
Aisee sijui ni kipaji au kupenda tu kusumbua....kuna watu wanapenda kuuliza maswali usifanye utani....
Wapo wale ambao huwa hawapendi kushughulisha bongo zao/miili yao...wao madam yupo mtu wa kumuuliza watauliza tu..... Utasikia anauliza 'maji yanatoka bombani'? Wakati huo wote mpo karibu na bomba..ni kiasi cha kusogea tu na kufungua bomba apate jibu au anauliza 'baba yupo hapo nje'? Wakati ni kiasi cha kusogea dirishani tu na kuchungulia au mtu amekuomba urafiki let's say facebook...kwenye profile yako umeandika wazi kabisa..lives in mwanza,home town singida....anakuja inbonx anaanza kuuliza 'vipi,pande za wapi? Hom wapi? Khaaa...why dont u view my profile...mwingine utasikia sina muda wa kuangalia profile za watu.....ila muda wa kuuliza maswali ndo unao?......wananiboa sana.

Wapo wale ambao hawajuagi kujiongeza......yani yeye anapenda aulize swali ajibiwe...ndo raha yake.
Pengine unauza mashati let's assume (ni mfano tu) anakuja mtu anauliza 'ee bwana una mashati ya rangi gani hapa kwako'? Unamjibu nina rangi mbili tu...nyekundu na nyeusi....utasikia 'nyeupe huna'?...khaaa...! Na usipomjibu atauliza hata mara tatu shida yake umjibu tu 'rangi nyeupe sina dada' ndo anaridhika.... Au anakuona umebeba jembe anakuuliza unaenda shamba? Namwambia no...naenda kanisani af nione kama atanibishia.....

Kundi lingine ni wale wanauliza maswali mfululizo utasema umekutana na afande Mwita.....anauliza maswali nane mfululizo..hivi huwa hawajishtukii? Mtu kama umekutana nae leo na mahusiano yenu yakaendelea utayajua mambo yake taratibu af utayajua automaticale bila hata kuuliza. Mi nikikutana na mtu wa hivyo maswali matatu ya mwanzo naweza kujibu ukweli au karibu na ukweli....yanayoendelea mbele yote nadanganya tu kwani shngapi...tunadaiana kwani?
Yangu ni hayo tu...kama nimekukera pita tu....
 
Khantwe umenifanya nicheke pekeangu, hilo kundi lapili ndio watu ninaoishi nao. Anaweza akauliza kitu ukanyoosha sentensi mpaka ukajua kabisa hapa hakuna swali lingine, aaa atakuliza tu tena kwa mfano kama ulioutoa
 
Last edited by a moderator:

Hahahaa utafiti umeona eeh? Mtu anakuuliza leo unaenda wapi? Utamjibu naenda kariakoo then mchana ntaenda mbagala...utaulizwa posta huendi? Ebo..! Sasa ningekuwa naenda si ningeitaja nayo?
 
Last edited by a moderator:
Hao maboifrendi wanauliza maswali hayo unawatoa wapi?
 
Mbona kama unanisema mimi?Na nikikuuliza swali nakua najibu langu kichwani ole wako unijibu tofauti yani maneno yake eeeeeh....lol.
 
Mbona kama unanisema mimi?Na nikikuuliza swali nakua najibu langu kichwani ole wako unijibu tofauti yani maneno yake eeeeeh....lol.

Hahahaa wii kama ndo hivyo mi na wewe tutakuwa tunagombana kila siku
 
Hahahaa utafiti umeona eeh? Mtu anakuuliza leo unaenda wapi? Utamjibu naenda kariakoo then mchana ntaenda mbagala...utaulizwa posta huendi? Ebo..! Sasa ningekuwa naenda si ningeitaja nayo?

Wewe sio yule kweli...? Sipendagi kuangalia profile za....
 
Last edited by a moderator:
Naww unapenda sana maswali kitendo cha kusoma tu ujue kuwa ni mm ndio nmeongelea maboifrendi unauliza tena.

Sio nakuuliza nipate jibu.....nakushangaa unaleta kitu ambacho mimi sijakiongelea
 
Back
Top Bottom