Maswali Magumu Yanayowatatiza Wahubiri

Maswali Magumu Yanayowatatiza Wahubiri

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
730
Reaction score
657
👉Wahubili wengi wanashindwa kueleza kwa uhakika kwanini watu waovu wengine wanaishi maisha mazuri huku waadilifu wakiteseka kila siku.

👉Swali la kwanini maombi ya baadhi ya waumini hayajibiwi licha ya kufunga na kuomba kwa muda mrefu linaendelea kuwachanganya wengi.

👉Tofauti kubwa za mafundisho kati ya dini moja na nyingine huwafanya wahubili kushindwa kutoa majibu yanayowaunganisha waumini wote.

👉Kuwepo kwa matajiri wakubwa ndani ya dini huku waumini wengi wakiendelea kuwa maskini ni jambo linaloibua maswali magumu kila siku.

👉Wahubili wengi hutatanishwa na swali la kwanini dunia inaendelea kushuhudia vita, njaa na mateso licha ya watu wengi kumuomba Kwa bidii.

👉Baadhi ya wahubili hushindwa kueleza kwa ufasaha siri ya maisha baada ya kifo na nini hasa hutokea kwa mwanadamu.

👉Migogoro ya kisayansi kuhusu uumbaji wa dunia na binadamu imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa mafundisho ya kidini.

Dr. Zack ✍️
 
Watu waovu wanaishi maisha mazuri waadilifu wanateseka ,👉maisha yanaendeshwa kwa kanuni sio maombi.

Maombi kutokujibiwa👉 fuata kanuni za maisha achana na maombi

Tofauti ya DINI moja na nyingine👉Dini ni utapeli Mungu hana Dini

Matajiri ndani ya Dini alafu waumini maskini👉Dini ni chombo kilichoundwa kwa ajili ya kuteka fikra za watu wazungu walitumia akili nyingi hapa na wamefanikiwa kwahiyo waumini wataendelea kuwa maskini mpaka watakapoamua kujitambua.

Vita na njaa,👉maombi hayawezi kuzuia hayo waliosababisha wanajua wanachokifanya Dunia inaendeshwa kimaslahi hata hao wahubiri Wapo kimaslahi

Maisha baada ya kifo👉wahubiri hawawezi kukuambia kwamba ukifa unazaliwa tena au unarudi kule ulipokuwa kabla hujazaliwa watakuambia Kuna siku ya mwisho na kama huendi kanisani siku ya mwisho utachomwa moto jehanamu.

Uumbaji wa Dunia👉hapa wahubiri watakusimulia yaliyoandikwa kwenye biblia Lakini biblia ni kitabu kilichochapwa oxford na wazungu kwa kutumia lugha ya mafumbo kwa kazi maalumu Mungu hausiki katika hicho kitabu
 
Mmekuwa wengi jamani!🙌🏾 Mungu hahusiki how sure are you??
 
Maswali yote haya ukiyaleta kwenye dini na Mungu yana tengeneza logical inconsistency na logical contradictions.

Ukiondoa Dini na Mungu, Maswali yote haya yanapata majibu yenye logical consistency yasiyo na contradictions zozote.
 
Dini ni utapeli ulioletwa na wanadamu ili kuwahadaa watu. Nchi za kiislamu wana Sharia Law, ukiacha dini ya uislamu adhabu Yako ni kifo (unakatwa kichwa), Cha kushangaza kwenye hizo nchi Kuna matajiri na masikini. Kwenye masuala ya dini mnashirikiana (tena ni lazima) ila kwenye masuala ya kazi, matibabu na malazi unajipambania mwenyewe, utajua pesa utatoa wapi za kupata matibabu😃😃😃😃

Dini zingekuwa ni za kweli watu wangeenda Macca na Madina bure, Quran, Tasbihi na Kanzu ungepewa bure ila hata kanzu zinazotofautiana bei, kwenda Hija ni Moja ya nguzo za uislamu ila unatakiwa ulipe nauli mpaka Macca na pia malazi na chakula lazima ulipie ukiwa Macca au Madina

Kama Mungu ni muislamu anawapenda waislamu, si ungeona watu wenye maisha mazuri wangekuwa waislamu😃😃😃😃 Sidhani kama Allah angeruhusu wasio waislamu wawe na Mali nyingi kuliko waislamu😄😄😄😄
 
Hakuna UHALIFU MKAMILIFU, hizo hoja zako zote ni evidence za "DINI NI UTAPELI"
 
👉Wahubili wengi wanashindwa kueleza kwa uhakika kwanini watu waovu wengine wanaishi maisha mazuri huku waadilifu wakiteseka kila siku.

👉Swali la kwanini maombi ya baadhi ya waumini hayajibiwi licha ya kufunga na kuomba kwa muda mrefu linaendelea kuwachanganya wengi.

👉Tofauti kubwa za mafundisho kati ya dini moja na nyingine huwafanya wahubili kushindwa kutoa majibu yanayowaunganisha waumini wote.

👉Kuwepo kwa matajiri wakubwa ndani ya dini huku waumini wengi wakiendelea kuwa maskini ni jambo linaloibua maswali magumu kila siku.

👉Wahubili wengi hutatanishwa na swali la kwanini dunia inaendelea kushuhudia vita, njaa na mateso licha ya watu wengi kumuomba Kwa bidii.

👉Baadhi ya wahubili hushindwa kueleza kwa ufasaha siri ya maisha baada ya kifo na nini hasa hutokea kwa mwanadamu.

👉Migogoro ya kisayansi kuhusu uumbaji wa dunia na binadamu imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa mafundisho ya kidini.

Dr. Zack ✍️
Wahubiri hawatatizwi na maswali yote, kwa sababu wao huhubiri yale waliyofundishwa kuhusu imani. Tatizo linakuja pale mtu anapotaka kumuuliza fundi muashi jinsi ya kutengeneza hereni ya dhahabu. Kila mtu ana taaluma na eneo lake la uelewa.

Tatizo kubwa la wengi wetu ni kutaka mafanikio kwa njia za mkato. Lakini kila kiumbe hai kina njia yake ya kupata riziki, haijalishi ni mwema au muovu. Unaweza kupanda mihogo shambani mwako, halafu wakaingia nguruwe wakaiteketeza. Kwako hiyo ni hasara, lakini kwa nguruwe hiyo ndiyo riziki yao. Hivyo maisha yana mchakato wake, na kila jambo lina njia yake.

Ukihitaji kufanikiwa, ni lazima ufuate mchakato uliowekwa ili jambo lako lifanikiwe. Maombi ni sehemu ya imani, na kila mwanadamu ana uhuru wa kuchagua imani anayotaka kuifuata, au hata kutofuata dini yoyote. Hakuna kulazimishana katika dini.

Kilicho muhimu zaidi ni sisi wanadamu kuishi kwa kupendana, kusaidiana, na kuheshimiana. Tusijenge chuki, fujo, wala vurugu kati yetu, kwa sababu hakuna anayeishi milele duniani. Kila mmoja ana muda wake wa kuishi, na baadaye ataondoka.

Tunapokwenda baada ya maisha haya hatujui kwa uhakika, lakini watu wa imani hutupa matumaini na habari njema kwamba tukitenda mema tutapata maisha ya amani na starehe, na tukitenda maovu tutapata maisha ya dhiki na adhabu huko tuendako, sasa ukiamini na ukatenda matendo mazuri halafu huko uendako ukakutana na maisha mazuri ni vizuri kuliko kutoamini kabisa halafu ukaenda huko ukakutana na mateso.

Lakini juu ya yote ni vizuri tukaishi kwa upendo na amani na matendo mazuri hata kama ikiwa tunatofautiana kwenye imani au hata baadhi yetu hatuamini dini yoyote.
 
Back
Top Bottom