Maswali Magumu Yanayowatatiza Wahubili

Maswali Magumu Yanayowatatiza Wahubili

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
894
Reaction score
777
👉Wahubili wengi wanashindwa kueleza kwa uhakika kwanini watu waovu wengine wanaishi maisha mazuri huku waadilifu wakiteseka kila siku.

👉Swali la kwanini maombi ya baadhi ya waumini hayajibiwi licha ya kufunga na kuomba kwa muda mrefu linaendelea kuwachanganya wengi.

👉Tofauti kubwa za mafundisho kati ya dini moja na nyingine huwafanya wahubili kushindwa kutoa majibu yanayowaunganisha waumini wote.

👉Kuwepo kwa matajiri wakubwa ndani ya dini huku waumini wengi wakiendelea kuwa maskini ni jambo linaloibua maswali magumu kila siku.

👉Wahubili wengi hutatanishwa na swali la kwanini dunia inaendelea kushuhudia vita, njaa na mateso licha ya watu wengi kumuomba Kwa bidii.

👉Baadhi ya wahubili hushindwa kueleza kwa ufasaha siri ya maisha baada ya kifo na nini hasa hutokea kwa mwanadamu.

👉Migogoro ya kisayansi kuhusu uumbaji wa dunia na binadamu imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa mafundisho ya kidini✍️
 
Swali la kwanini maombi ya baadhi ya waumini hayajibiwi licha ya kufunga na kuomba kwa muda mrefu linaendelea kuwachanganya wengi.
Sio baadhi, hakuna anayejibiwa hata mmoja, mtu akiona jambo kimetokea anaaamini limekuwa wakati sio kweli
 
Wahubili wengi hutatanishwa na swali la kwanini dunia inaendelea kushuhudia vita, njaa na mateso licha ya watu wengi kumuomba Kwa bidii.
Mungu Hasikiizi, haoni wala hajali mambo ya duniani, amepumzika zake huko Mbinguni
 
Back
Top Bottom