WALE WALIOTUAMBUKIZA IBADA ZAO.. wamegeuza afrika kisiwa cha biashara .. je kiwanda cha silaha kifungwe? kama hapana soko ni wapi? kwetu sisi tuliopokea mapokeo bila kuchuja na kuendelea kupokea mapokeo bila kujali hata uhai wetu...
Hii kitu ukiwa ni msomaji sana kwenye mitandao inachanganya sana as ujuavyo kwa sasa ndiyo source ya haraka ya info mbalimbali, kuna dhahania nyingi sana ikiwemo Udini na mengineyo mengi ya kimaslahi zaidi. Ila katika yoote mi nina-conclude kwa jambo moja tu "ujinga" baasi!!
Nisingependa wale wafia dini waanze kujibizana na kutukanana nami na wala sijakariri mtandao wowote au kifungu chochote ili muanze kunidai reference!! Mi naeleza kisicholenga dini ingawa huwezi kuzungumzia ugaidi bila kugusa dini japo kidogo!!
Sometimes tusiwasingizie Wazungu!! Ni upuuzi wetu wenyewe.....!! Mfano Bagbo alipogoma kuondoka madarakani jeshi likagawanyika utamlaumu mzungu kwa mauaji yalojitokeza pale?? Hivi jeshi la Bagbo lingetoshana nguvu na jeshi la aliyekuwa amechaguliwa (Lilipata msaada kutoka kwa wazungu) si ile vita ingekuwa endelevu mpaka leo??
Utashi wetu uko wapi sasa??
Ingawa kwa udadisi mdogo niliosoma kona mbali mbali za mitandao ni kwamba baada ya marekani kuweza kumaliza vita baridi kwa kuivunja USSR ugomvi wake mkubwa ulihamia kwa rasilimali ya mafuta!! Aliona kwamba wanaotoa/kuzalisha rasilimali ya mafuta wakikaa pamoja itakuwa ni fimbo kuubwa ya kuweza kumtandika yeye na marafiki zake hasa ikizingatiwa kuwa wanaozalisha rasilimali hiyo si watu ambao angeweza kukaa nao meza moja na kupanga majambo (refer maisha na ukorofi wa Waarabu) na pia tayari walishakuwana na umoja wao (OPEC) na walishaanza kukaa pamoja na kuweka mikakati ya kupanga bei na vitu kama hivyooo!!.
Hivyo mikakati ilianza lengo likiwa ni kuweka viongozi wao ambao watatii mamlaka ya Marekani (as kinara) kama ilivyo Afrika na baadhi ya nchi za Asia na kilichotokea ndo hikiii tunachokishuhudia!! Magaidi kutoka nje ya malengo yao na pia kwenda nchi nyingine bila ya kuusoma mchezo wanaanza kuiga na kulipuana wenyewe kwa wenyewe. Hebu tujiulize swali dogo, nilisoma jinsi magaidi wa ISIL wanavyokwepa technology mpya ya drones ya kuwashoot isijue mahali walipo!! Kwa akili ipi waliyonayo kama si mbinu wamepenyezewa na hao hao waliozitengeneza??
Ingawa kwingine wanasema ni kipindi cha mpito kama ilivyopita matukio mengine mfano utawala wa Warumi, ikaja kugombania makoloni(kutawala), biashara ya utumwa, nchi nyingi kupata uhuru na baadae kukaibuka magenge makubwa sana ya dawa za kulevya!! Yale magenge kwa kiwango kikubwa yamedhibitiwa na sasa umeibuka ugaidi. Ukiangalia yote hayo yanaendana na maslahi ya wachache au mataifa fulani na pia kila kimoja kimetokea katika bara tofauti!!
Kwa Afrika ni ushamba na kuiga tu hakuna lolote la msingi!! Uafrika wetu ni mzigo sana sana yaani tunashindwa kujijua tu, mbona Asia, America ya Kusini kuna Waislam lakini hawalipuani?! Angalia Nigeria, mnataka nchi itawaliwe Kiislam then mnaenda kulipua kwenye soko katika mji wenye Waislam wengi hiyo akili au matope? Mpaka muishike hiyo nchi si mtatawala Wakristo tupu? Mwingine anaenda kujipiga picha na yeboyebo eti "tutawachinja" yaan ni upuuzi mtupu kweli Miafrika ndivyo tulivyo!!!
Ni ninavyoelewa mimi kama kuna la msingi twende kistaarabu na sihitaji habari za vifungu vya vitabu au kunilazimisha fulani ni desturi yake kuua sijui aagh!!