Maswali kwa Mh. JPM na mawaziri wake.

frakitosho

JF-Expert Member
Dec 13, 2012
802
255
1. Wakati wa kampeni uliahidi kutowabagua watanzania kwa itikadi zao za vyama, je mbona wateule wako wote ni wakereketwa/makada wa CCM?
2. Haya majipu unayotumbua yalisababishwa na nani? Kwa nini huyo msababishaji hajachukuliwa hatua hadi sasa?
3. Je, Tanzania ni Dar es Salaam tu? Mbona mawaziri wako wanaishia vingunguti na urafiki textile tu? Huko mikoani hakuna majipu?
4. Ulisema pesa za elimu bure zitaenda moja kwa moja kwa walimu wakuu, je umeandaa magereza ya kutosha kuwahifadhi walimu wakuu watakaozitafuna? Au je, umewaandaje kisaikolojia kushika fedha nyingi kwa mara ya kwanza hususani wa vijijini?
5. Ule muongozo wa ada kwa shule binafsi umekwama wapi? Shule zinafunguliwa wiki hii, sasa je tusuburi muongozo ama tulipe ada halafu tutarudishiwa chenji pindi muongozo ukitoka?

6. Mwenye swali aongezee....
 
kwenye ada shule za binafsi waziri alisema tulipe ada tuliyolipa mwaka jana nyongeza hakuna
 
Huo utakuwa ni ubabaishaji. Watoe ada elekezi. Mamlaka ya elimu kazi yake ni nini? Hata NACTE na TCU pia wanatakiwa ku-monitor ada za vyuo na vyuo vikuu
 
Issue ya ada elekezi hapo tunaomba walitolee maelekezo maana wazazi wengi wanasubiri kauli ya serikali ndo walipe ada zinaumiza sana.
 
Walipoona wenzao wanafanya ziara za ghafla na wao wakaamua kutamka kwa ghafla tu, wala hawakua serious ma walichokiongea
So ninyi kalipeni tu afa ksma zitakavyokuwa zimepangwa na shule.
Tanzania muda si mrefu inageuka babeli.
 
1. Wakati wa kampeni uliahidi kutowabagua watanzania kwa itikadi zao za vyama, je mbona wateule wako wote ni wakereketwa/makada wa CCM?
2. Haya majipu unayotumbua yalisababishwa na nani? Kwa nini huyo msababishaji hajachukuliwa hatua hadi sasa?
3. Je, Tanzania ni Dar es Salaam tu? Mbona mawaziri wako wanaishia vingunguti na urafiki textile tu? Huko mikoani hakuna majipu?
4. Ulisema pesa za elimu bure zitaenda moja kwa moja kwa walimu wakuu, je umeandaa magereza ya kutosha kuwahifadhi walimu wakuu watakaozitafuna? Au je, umewaandaje kisaikolojia kushika fedha nyingi kwa mara ya kwanza hususani wa vijijini?
5. Ule muongozo wa ada kwa shule binafsi umekwama wapi? Shule zinafunguliwa wiki hii, sasa je tusuburi muongozo ama tulipe ada halafu tutarudishiwa chenji pindi muongozo ukitoka?

6. Mwenye swali aongezee....

7. Zile milioni 50 kila kijiji atazitoa lini?
 
Back
Top Bottom