Hatimae tumemsikia na kumshuhudia aliekuwa Chief of Defense Forces kupitia media na mtu ambae inaonekana ndie alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa siku zote Marehemu JPM akiwa anapigania uhai wake na hatimae kuondoka Duniani!
Lakini maelezo yake yameongeza sintofahamu zaidi kuliko alivyotarajia. Na kwa wengine hasa mimi binafsi,
Kwa kusahihisha tu Karma lazima ianzie kwa Ben Saanane , Azori Gwanda , Leopold Lwajabe na wengineo wengi waliokumbana na mkono wa chuma wa dikteta.
"karma". Muda mfupi baadae mtoto wa kiume wa Mabeyo aliekuwa Pilot pale Coastal Aviation alianguka na ndege uwanja wa Seronera akiwa yeye na rubani mwanafunzi wa vitendo (trainee) na wote walifariki Dunia.
Hili kwa sasa sintaliongelea sana ila nimeliweka hapa ili kuonyesha ukuu wa Mungu na Malipo yake kwa wale anaotaka kuwapa majibu ya matendo yao wakiwa bado hai.
Na wakati mjadala ukiendelea kuhusu mambo kadhaa ya kisiasa kutoka na hotuba ya Mstaafu Mabeyo!
Sisi wengine tunajiuliza wwali muhimu:
Magufuli ndio alianzisha tabia ya kuficha vitu na uongo ndio aliwapa kina Kabudi ndege wakaenda Madagascar wakaleta juice wakisema rais kule anagawa mwenyewe wakaishia kunywa wao wakapiga mapicha wengine wakaambiwa hawatokunywa hadi iende maabara ya NIMR haijawahi kuletwa majibu ya tafiti za NIMR hatujui hata kama Magufuli mwenyewe aliyetoa ndege alikunywa ile juice au lah!
Ni kwa nini walituficha ugonjwa wa mpendwa Rais wetu JPM?
Tunajiuliza:
Dr Janabi alikuwepo pale JKCI muda tu hatukutokea nje ya nchi siku Magufuli analazwa labda hii ingeleta clue kidogo na senior specialist wa cardiology pale so kuwepo kwake pale sio tatizo .
Dk Janabi alikuwa pale muda wote akifanya nini ilhali yeye hakuwahi kuwa Daktari wa JPM, bali alikuwa ni Daktari wa familia ya Kikwete na pia swahiba ya JK?
Tunajiuliza
Mzena ameenda Mkapa na imekuwepo muda pale , Mkapa kafia pale ,Binti Nyerere , na Magufuli mwenyewe sasa Mwinyi sasa sijui kufichwa huko ni kupi
...ni kwa nini walikwenda kumficha pale Mzena badala ya kumpeleka kwenye hospitali nyingine yenye hadhi ikiwezekana hata nje ya nchi?
Nje ya nchi Magufuli ndio alikuwa akisema hapataki wangempeleka akafia huko si mngepiga kelele za kutosha kuwa "mabeberu " walimuua ila pia Magufuli alizuia vibali vya watumishi wa umma kusafiri nje na akasema anaboresha hospitali watu watatibiwa hapo hapo hakuna sababu ya kwenda nje.
Tunajiuliza. Kama waziri mkuu alituficha. Makamu wa Rais alituficha!
Ni nani au kikundi gani kilikuwa kinaratibu haya mambo?
Madaktari ndio wanaamua mgonjwa aruhusiwe au lah , huko alikotaka kwenda kulikuwa na huduma bobezi za kitabibu ?
ex-CDF angedictate hii na akafia Chato si mngesema Mabeyo amesuka mkakati , pia kwa wimbi lile la UVIKO la pili mtu atatolewaje hospitali arudi nyumbani akiwambukiza wa nyumbani wote hujiulizi kwanini familia yake haikuwepo hospitali ?
Tunajiuliza: Kama Mkuu wa majeshi aliambiwa na JPM awali kwamba wamrudishe nyumbani akafie huko.Ni kwa nini aligoma kutimiza takwa la Marehemu? Na kwa nini hakuwashirikisha wengine ili wachukuwe maamuzi sahihi?
Ukweli usemwe Magufuli alikuwa mgonjwa wa muda mrefu na dalili za kuchoka zilishaanza kuonekana mosi angalia kampeni za "uchafuzi" mkuu 2020 alikuwa anapiga kampeni leo anapumzika siku 8 , kila Magufuli alipokuwa akisimama kulikuwa na "air cooler " nyuma yake hii kwa wachache tuliona sio dalili nzuri hasa kwa open space kama ile na hewa ni ya kutosha air cooler ni ya nini?
Pia baada ya wimbi la kwanza kwa kuwa alikuwa "prone " kuambukizwa UVIKO alifuata ushauri vizuri alichimbia Chato kuanzia March 2020 hadi May mwishoni 2020 , Baada ya Mahiga kufariki hata Mwigulu aliapishwa Chato maana yake ni nini Chato waliifanya kama ngome ya kumficha na kumfanyia 'isolation' maana wimbi lile lingeweza kumfyeka kama asingekuwa makini ila awamu ya pili akapuuza wimbi likiwa limechachamaa February 2021 akatoka kwenda kuzindua soko la Kingalu Morogoro, Kijazi interchange na stendi ya mbezi huko kote alijiingiza kwenye mikusanyiko isiyo na sababu wakati yeye yuko kwenye yale makundi "prone" kupata UVIKO na kupelekea matatizo makubwa kutokana na complications za kupumua.
Je, Magufuli aliugua ugonjwa gani huo ambao madaktari walikaa pembeni wakimshuhudia akipigania uhai wake akiwa kama mateka?
Utawala wa Magufuli chain of command haikuwa sawasawa ndio maana hata Sabaya alisema yeye anampigia Magufuli simu hata saa 8 usiku na anapokea na yeye anaripoti kwa Magufuli moja kwa moja asiulizwe na mtu yoyote je hii ni sawa?
Polepole alikuwa anapigia mawaziri simu kwenye kipindi cha TV na kuwauliza maswali live wakati ofisi zipo na miongozo na muda wa kazi upo , yani mtu yupo kwake kapumzika saa 2 usiku apigiwe simu kisa mwenezi ana kipindi hapo kuna work-life balance kweli?
Magufuli alitengeneza magenge ya watu waaminifu na tiifu kwake aliowaamini bila kufuata chain of command maana tulishuhudia Makonda akimbeza Spika wa bunge live wakati spika wa bunge ni mkuu wa mhimili kabisa .
Pia waliohoji Magufuli yupo wapi walitishiwa , kuambiwa hawaitakii mema Tanzania na wengine kukamatwa haya aliyasema Kasim Majaliwa akiwa msikitini Iringa , March 12 2021
Anasema alipofariki wao wakuu wa vyombo ndio waliwajulisha viongozi kama PM, CS na baadae makamu wa rais, ena wote hawakuwepo eneo la tukio.
Hawa hata wangekuwepo wangefanya nini?
Bashiru Ali aliteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi kinyume na katiba , katiba inasema katibu mkuu kiongozi atatakiwa kuwa mtumishi wa umma je Bashiru Ali alikuwa ni mtumishi wa umma bado baada ya kutoka UDSM?
Hatuoni mahala makamo wa Rais, mwanasheria mkuu, Wala jaji mkuu au spika wakiwa na maamuzi yeyote. Kila kitu kilipangwa na jeshi. Huyu Mabeyo ameongea, iko siku na wengine wataanza kuongea. Damu ya mtu huwa haipotei bure.
Samia alitengwa na kundi la Magufuli ambalo ndio wahuni hao waliotaka kumsimika mtu wao ili waendeleze maslahi yao waliyoyapata Magufuli akiwa madarakani hivyo waliona akishaondoka kuna namna watapwaya na ndio uhalisia leo hii 99% ya wafuasi tiifu wa Magufuli wametulia kama maji mtungini
Kama kuna jambo lilipangwa na kufanywa na kikundi fulani,kinyume na tulivyoamishwa sisi wananchi. Na kwa jinsi siku ya Jana ilivyopita bila hata serikali ya Saa100 kujishughulisha na lolote kuhusu kumbukumbu hii muhimu nchini.
Tukiwa tunaendelea kusubiri shuhuda tunahitaji kupata taarifa za alipo Ben Saanane, Azori Gwanda.
Nani walikuwa nyuma ya tukio la kutekwa kwa Mohamed Dewji ,Roma Mkatoliki na wengineo wengi.
Nani alikuwa nyuma ya shambulizi la risasi kwa Tundu Lissu September 7 ,2017
Tutashuhudia taraatiiibu!
R.I.P Jemedari JPM!
Wameanza kuropoka huku!