FaizaFoxy - Jf senior expert member Hapo Zittoanaongelea Tax, tena ya Capital gain.
Zitto anaelewa sana kuhusu Tax evasion na Tax avoidance lakini hilo anajifanyakama halijui. Ananshangaza!
Hapo jamaa hawakufanya Tax evasion hapo ni simply Tax avoidance, kisheria.
Hakuna ujanja hapo, kama hawakufanya evasion ni halali kabisa.
Zitto anachoshindwa kueleza ni kuwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni yaKitanzania, kaingia Singasinga kaiona opportunity na kajuwa vipi atatatuwa huomgogoro, kaongea nao wamekubalina kawanunua kawalipa, kavuta fedha walizokuwawalipwe wao.
Kinachofata hapo ni uhalali wa tx na ndio anauongelea Zitto, kachimbuwa kakutahakuna tzx evasion kuna tax avoidance ambayo kisheria ni halali.
Sijui msichokielewa anachoongelea Zitto zaidi ya hicho ni nini?
Nadhani, Zitto angekuwa kidogo mjanja asingeongelea hilo la kampuni kuuzwamillion 6, unless anajuwa anachokifanya ila anataka ku divert msimamo, kunakila uwezekano na yeye kavuta au anataka kuvuta kwa singa na IPTL nahuyoMtanzania mwingine ambae hatajwi sana humu, lakini yeye ndio master-mind wahuu mkorogano.
Hapo sasa hivi kuna kila mtu kutaka kuvuta kwa Singa kwa kupiga makelele.
My Take:
Nasema huyo Mtanzania ni mastemind kwa sababu yeye alifikiri akiwabana sanaIPTL watakubali yaishe wachukuwe fedha wagawane halafu mitambo yote atabakinayo yeye aanze kuchuma peke yake kiulaini.
Bahati nzuri au mbaya, Singa kaliona hilo akaingia kati na kuna kila sababukakubaliana na IPTL kuwa wataumizwa, yeye ana njia mbadala watakuwa ni win winsituation, pesa watapata na mitambo haitopotea na wamuamini yeye, na ndichokilichofanyika.
Hapo aliyeumia ni Mtanzania mwenzetu, tena si kaumia kwa kuwa hajapata faida yabure, la hasha, faida kapata ya bure tena kubwa sana, kwani yeye hajatia fedhayake katika hili sakata, yeye alikuwa kama godfather tu waku facilitate mambondani ya Tanzania. Ndiyo norm kwa biashara zote kubwa duniani.
Alichoumia ni pale alipotaka kubana moaka mitambo yote ibaki kwake. Kataka kulakiharamu zaidi, ndipo Singa alipoingia na ku rescue.
Sasa, Mbnde kuona hivyo ni lazima apigane, kwani kwa sasa fedha ya kuwalishawapayukaji hovyo kama akina Tumbili anayo, na afanye nini zaidi? anachofanyakama kukosa tukose wote, lakini amechelewa jamvini karamu imeshaliwa.
Mwisho wa siku, kisheria ataibuka Singa kidedea, labda afanyiwe umafia. NaSinga si mdogo huyo, Tanzania anaijuwa juu chini, kaishi sana pande za Iringa,kama kuna mtu anaikumbuka RCC Iringa, basi ni hao akina Singa si wageni kabisaTanzania hii.
Mengine yote ni kubwabwaja, porojo na kuhororoja, kuna mshiko wa watukunyamazishwa na ndiyo maana unasikia kelele.
Hakuna wizi hapo wa mali ya umma kisheria, kuna "opportunity" naWatanzania kama ujuavyo ni ma "opportunists" kama fisi wanavyongojamifupa au makopangola wanavyoona mzoga, hawachelewi! ndicho kilichopo.