Maswali kumi kwa David Kafulila kuhusu IPTL

shadow recruit

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Posts
1,844
Reaction score
384
Baada ya kufuatilia na kushiriki mjadala huu mpana wenye maslahi kwa taifa letu nimepata maswali kumi ambayo ndugu yangu david kafulila anaweza kunisaidia kuyajibu kuhusu iptl na escrow.

1.JE Anaijua historia ya iptl vizuri au anaifahamu kwa kupitia kusoma raia mwema na machapisho ya zitto kabwe

2.JE Anafahamu mchakato wa mauziano ya hisa ulivyofanyika kati ya mechmar corporation (malaysia)berhard kwenda pap,anajua kwamba seth aliomba kuuziwa sehemu ya hisa za iptl tanzania yaani 70% za iptl zilizokuwa chini ya mechmar lakini akakataliwa kutokana na sheria za biashara kimataifa kutoruhusu mwangalizi kununua hisa za kampuni anayoisimamia,na hivyo hisa kuuzwa kwa kampuni ya piper link,hivyo seth singh alilazimika kuomba piperlink imuuzie hisa zake ndani ya iptl tanzania,na manunuzi hayo yalifuata taratibu zote za kisheria ikiwa pamoja na kununua madeni yote ya kampuni,je analijua hili?

3.JE Kafulila anafahamu masuala yote yalioleta utata kuhusu capacity charges za kuzalisha umeme kati ya iptl na tanesko yaliamriwa na kupatiwa ufumbuzi katika mahakama ya kimataifa ya biashara,na masuala ya mgawanyo wa mapato kati ya wanahisa yaani vip na mechmar yalipatiwa ufumbuzi katika mahakama kuu tanzania chini ya jaji ukama,hukumu iliyopelekea kuanzishwa kwa akaunti ya escrow ambayo kimsingi ilikua inatunza malipo ya wanahisa yanayotokana na mauzo ya umeme wanaozalisha na kuizia taneko baada ya usuluhishi wao mahakama ya kibiashara kuhusu capacity charges.

4.JE Kafulila anafamu kuwa vip iliuza hisa zake kwa pap baada ya kufikia makubaliano ya bei ya hisa zote 30% za vip?,Na kumfanya harbinder seth singh kuwa mmiliki halali wa asilimia zote mia za iptl

5.JE Kafulila anafahamu kuwa mmiliki wa vip bwana rugemalira sio mtumishi wa umma na hivyo kama raia wengine ana haki ya kutumia fedha zake alizopata kwa njia halali ya kuuza hisa zake ndani ya kampuni anavyotaka bila kuvunja sheria,bila kuingiliwa na mtu yeyote hata kama amehonga mwanamke,ametupa jalalani,amekunywa pombe au ametoa msikitini/kanisani/shuleni/ametoa msaada kwenye kwaya/kumpa mchepuko hata bilioni mbili,maana ni zake na kafulila hatakiwi kufuatilia maisha ya mtu binafsi maana hata rugemalira afuatilii maisha ya kafulila.

6.JE Kafulila anafahamu kuwa iptl ndio kampuni pekee inayookoa fedha za watanzania kwenye nishati kwasababu ya kuwauzia umeme kwa bei nafuu kuliko kampuni anayoipigia debe na iliyomtuma kuichafua iptl yaani symbioon ambayo inaiuzia tanesco umeme unit moja kwa zaidi ya elfu moja wakati iptl inaiuzia umeme tanesco chini ya shiling mia tano kwa unit na imeanza mazungumzo kushusha umeme hadi sh 90 kwa unit,je haoni anatumika vibaya na kampuni yenye wivu wa kibiashara kuchafua iptl ambayo ni mkombozi wa tanzania

7.JE Kafulila ana majibu gani baada ya kulidanganya bunge kuhusu mmiliki wa iptl harbinder seth singh kufukuzwa na kutotakiwa kufanya biashara kenya kwa sababu ya ufisadi wakati wiki iliyopita iptl ilikabidhiwa barua na waziri wa nishati kenya kupewa tender ya kuzalisha umeme mw 2000.?

8.JE Kafulila anazungumziaje tuhuma za yeye kupokea milioni tisini kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa walioathirika na kitendo cha waziri mpya wa nishati na madini sospeter muhongo kufunga mirija ya kifisadi waliyokuwa wanatumia kujinufaisha na kuifilisi nchi (rostam,mengi,mkono) ili awachafue na kuwakomoa muhongo na katibu wake maswi?

9.JE Kafulila haoni ni muda sahihi wa yeye kuwataka radhi iptl na watanzania kwa kutumika na mafisadi ili kurudisha heshima yake kwa watanzania.

10.JE Kafulila anataka tumtambuaje baada ya haya yote,mpigaji?/Mzalendo/mtu wa kutumia fursa/au mtumikaji?

Naomba kuwasilisha ili mkuu kafulila aweze kuyajibu,karibuni kwenye mjadala

Tibaijuka yeye kagawiwa Bil 1.3 jewewe umegawiwa shilingi ngapi na hawa matapeli ili uje hapa kuuliza ujinga wako?

Tangu lini pesa isiyo ya serikali ikakaguliwa na CAG?

Hivi unatumia tumbo kufikiri?

Maswi na Muhongo wanajaribu kupigapiga miguu chini ili kujinasua lkn wizi kama huu wa kutuibia na kugawana genge lisilozidi hata watu 20 pesa nyingi zaidi ya Bil 200 ,hauvumiliki tena.

Kila siku unakuja jamii forums kupima upepo.
 
Duh mkuu punguza jaziba yaweza kuwa wewe una mengi yakutujuza juu ya maswali hayo kwa kafulila, tatizo lako unakuwa na haraka na hasira ila nakuona unayo hoja ya msingi kabisa. Hebu vuta pumuzi urejee tena utupe ukweli wa sakata hili
 
Hivi umeona wapi mahesabu ya kampuni binafsi yakakaguliwa na CAG?Mleta mada punguza kutumika au na wewe umeshamegewa zako?Mwenzako Tibaijuka keshamegewa BL 1
 
naona mnahangaika kujisafisha lakini wapi hilo limewafia kafulila hawezi kukurupuka bila kujua hayo mambo KAFULILA HOYEEEEEEE endelea hawa mafisadi wasipate usingizi kawashika pabaya na maswali yako ya kipuuzi leo mnazalau hata vyombo vya habari kisa kuujua ukweli wenu na bado.
 
Tibaijuka yeye kagawiwa Bil 1.3 jewewe umegawiwa shilingi ngapi na hawa matapeli ili uje hapa kuuliza ujinga wako?

Tangu lini pesa isiyo ya serikali ikakaguliwa na CAG?

Hivi unatumia tumbo kufikiri?

Maswi na Muhongo wanajaribu kupigapiga miguu chini ili kujinasua lkn wizi kama huu wa kutuibia na kugawana genge lisilozidi hata watu 20 pesa nyingi zaidi ya Bil 200 ,hauvumiliki tena.

Kila siku unakuja jamii forums kupima upepo.

Ukizungumzia Prof. Tibaijuka kugawiwa pesa za iptl naingiwa na hamu ya kutaka kukuelewesha, lakini kwanza rudisha ubongo wako kichwani ili unielewe. Wakati JR anataoa fedha kwa Prof. Tibaijuka hakuwa mwanahisa wa iptl,alikuwa kashauza hisa zake kwa iptl tena kwakufata sheria zote. Wasingeanzisha ukaguzi kafulila angetunga na wimbo kabisa, lipi jema kwenu? Hakuna wizi hapa akaunti ya Escrow ilifunguliwa kutokana na "Dispute" iliyotolewa na TANESCO na sasa, "Dispute" haipo, na hivyo Serikali yeyote makini haina sababu ya kuzuia fedha ambazo zipo kwenye akaunti ya Escrow kwa sababu yoyote ile.
Kilichopo hapo kuna wajinga tu walimwambia Prof. mohongo baada ya kuzibiwa mirija yao wizarani pale "UTAONA WEWE", ndio akatafutwa bwana mdogo mtoto wa mjini Kafulila akamezeshwa riwaya za Zitto akaanza kuropoka.
 
Hivi umeona wapi mahesabu ya kampuni binafsi yakakaguliwa na CAG?Mleta mada punguza kutumika au na wewe umeshamegewa zako?Mwenzako Tibaijuka keshamegewa BL 1

Mkuu unajifichia kona fupi mno CAG kazi yake ni kwenda kukagua namna fedha hizo zilivotolewa bank kuu kama zilifuata utaratibu wa kibenk nasi vinginevyo. je fedha hizo zililipwa kwa walengwa waliyoiuzia umeme Tanesco? kama ni kweli kwanini baadhi yao wanapiga kelele? akishabaini hapo CAG kwamba fedha hizo zililipwa kwa wahusika. itakuwa wale wanaolalamika watakuwa huru kwenda mahakamani kwenda kumshitaki yule wanayedaina naye
 
naona mnahangaika kujisafisha lakini wapi hilo limewafia kafulila hawezi kukurupuka bila kujua hayo mambo KAFULILA HOYEEEEEEE endelea hawa mafisadi wasipate usingizi kawashika pabaya na maswali yako ya kipuuzi leo mnazalau hata vyombo vya habari kisa kuujua ukweli wenu na bado.
Kafulila ndo kashikwa pambaya na mabosi wake akina mkono na rostam, kwenye hili hawachomoki watanzania now tunajielewa
 
Tibaijuka yeye kagawiwa Bil 1.3 jewewe umegawiwa shilingi ngapi na hawa matapeli ili uje hapa kuuliza ujinga wako?

Tangu lini pesa isiyo ya serikali ikakaguliwa na CAG?

Hivi unatumia tumbo kufikiri?

Maswi na Muhongo wanajaribu kupigapiga miguu chini ili kujinasua lkn wizi kama huu wa kutuibia na kugawana genge lisilozidi hata watu 20 pesa nyingi zaidi ya Bil 200 ,hauvumiliki tena.

Kila siku unakuja jamii forums kupima upepo.
Wewe ni wakuhurumiwa tu kichwani patupu sana, hakuna unachokijua zaidi ya kubwabwaja tu. ila ukweli jamaaq zako wanaujua wazoefu waq kutumika , kafulila hachomoki mkuu kwenye hili sakata
 
Hivi umeona wapi mahesabu ya kampuni binafsi yakakaguliwa na CAG?Mleta mada punguza kutumika au na wewe umeshamegewa zako?Mwenzako Tibaijuka keshamegewa BL 1

Nashukuru mkuu,mimi nimeleta mada tujadili sasa natumikaje hapo
 
naona mnahangaika kujisafisha lakini wapi hilo limewafia kafulila hawezi kukurupuka bila kujua hayo mambo KAFULILA HOYEEEEEEE endelea hawa mafisadi wasipate usingizi kawashika pabaya na maswali yako ya kipuuzi leo mnazalau hata vyombo vya habari kisa kuujua ukweli wenu na bado.

Kafulila ni binadamu naye pia anakosea,ndio maana alidanganya bunge kuwa seth hatakiwi kenya,wakati ni kinyume chake seth kapewa mradi kenya mkubwa kuliko wa hapa tanzania
 
Hivi umeona wapi mahesabu ya kampuni binafsi yakakaguliwa na CAG?Mleta mada punguza kutumika au na wewe umeshamegewa zako?Mwenzako Tibaijuka keshamegewa BL 1

teh teh teh teh!!! Wasinge kagua kafulila angetunga wimbo @ mfia uzi
Halafu hili la Tibaijuka iptl wenyewe wameshalitolea ufafanuzi labda kama umeamua kutoelewa maelezo yao mazuri. Ukikosa angle ya kutete upande wako usilete ramli, kwahyo kwakuwa unampinga nayeye awe namawazo kama yako unatumika.
 
Hivi umeona wapi mahesabu ya kampuni binafsi yakakaguliwa na CAG?Mleta mada punguza kutumika au na wewe umeshamegewa zako?Mwenzako Tibaijuka keshamegewa BL 1

CAG anachunguza sababu anataka kujiridhisha kama fedha ni za tanesco au zote zilikua mali ya kampuni ya IPTL
 
Back
Top Bottom