Maswali kuhusu COVID 19 Tanzania

SheriaE

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
606
446
Habari ya wakati huu!

Poleni na mapambano dhidi ya COVID 19.

Mimi kuna maswali kadhaa kuhusu COVID 19, Na mambo yanavyoendelea Tanzania hasa kwenye Social media. Yako kama hivi.

1. Kuna watu wanasema kwamba idadi halisi inafichwa ya waathirika wa COVID 19. Sasa swali liko hivi kama ni kweli idadi inafichwa ni kwa ajili ya nani au nini? Na wanaoficha wanalengo gani? Kwa faida ya nani? Na ili iweje? Naombeni ufafanuzi kwa wenye majibu sahihi niweze kufunguliwa ufahamu ni kwa nini mambo yanakwenda hivi. Just why?

2. Alafu kuna wengine wanasema watu wanaumwa wako hospitali lakini ni muda mrefu wamekaa huko bila kuchukuliwa vipimo. Katika hili kuna ukweli kiasi? Na kama ni kweli kwa nini iko hivyo? Ina maana hakuna pesa ya kutosha kununua vipimo?

3. Na kuna wati wengine wanataka serikali ichukue baadhi ya hatua. Lakini ikijaribu kufanya hivyo kuna wengine wanajaribu kusema serikali eti iwape msaada wati wakati wao wenyewe ndio walidai uko kitu, maana tayari walikuwa tayari wamejiandaa sasa kwanini watake msaada tena? Tanzania tunataka nini?

4. Halafu na hawa wa mitandaoni wanaotoa taarifa kuhusu COVID 19 wana lengo gani? Ni kutisha watu au ndio nini?

Mwisho ningependa kutoa mapendekezo au ushauri kwa serikali ya JMT.
1. Naona mpaka sasa hakuna jinsi ni bora lockdown ikahusika tena ile ya total sio partial huenda ikasaidia kwa sababu watu wameachiwa lakini bado kuna vitu havina ulazima still vinafanyika.

2. Pia kama ikiwapendaza serikali itoe pesa kidogo kwa kila kaya, wasiojiweza kuanzia laki moja mpaka tatu. Lakini isiwe lazima.

Tuendelee kuchukua tahadhari.
Kama huna mishe ya msingi kaa home.


Please be on your limit.
 
Africa mambo mengi tunapenda yabaki mafumbo au yaonekane ni miujiza. Bado akili za watu wengi pamoja na viongozi wetu wengi hazikubali ukweli wa kisayansi. Wakati Uingereza waziri mkuu na mwana mfalme wakijitangaza kwamba wameathirika na corona, kwetu waliougua ni siri yao. Mpaka akili za watu zitakapokuwa scientific ndio tutajikwamua na changamoto zetu.
 
Inawezekana ni kweli kabisa data zinafichwa Na hata Maneno yake Mh waziri yanaleta ukakasi yamkini wamekua wakificha taarifa tangu hapo awali

“Mnaona kuona nimetoa takwimu kubwa lakini tunaamua tuseme ukweli kwa sababu Watanzania lazima waelewe kwamba changamoto hii ipo na kila mtu sasa kwa nafasi yake, kama kulikuwa na mtu anadhani tunatania ni wakati wa kuchukua hatua”- Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Sasa kwenye upande wa kwanini wanaficha, Me nadhani ni katika kushikiria tuu msimamo wao wa kuuchukulia Covid-19 kama kagonjwa kadogo kamafua kagonjwa ka-shetani kama wasemavyo hivyo wanaona kutoa idadi ya kweli pengine italeta taharuhi kwa wananchi ikawafanya waogope. So hivyo Lengo lao kubwa ni kuto wapa hofu Wananchi kitu ambach Si Sawa Maana kuongopa haizui Covid-19 kuspread bali kuiwekea Mazingira mazuri Covid-19 ili itafune vizuri
 
Ushaambiwa kuna corona,inatosha wewe chukua hatua kama ni kuji-lockdown,au kuji-self isolate vyovyote vile ..unataka kusikia watu wengi wameambukizwa ili iweje??? unataka kujua watu wengi wamekufa ili iweje?..wewe si daktari,hiyo ni kazi ya mamlaka!.kitu usichokijua ni kwamba serikali nyingi zimeficha takwimu halisi za athari za virusi hivi vya corona,kuna watu watakufa na wengine watapona,kisha dunia itaendelea kama kawaida,cha msingi jitahidi kujilinda ili uwe mmoja wa watakaoendelea na dunia
 
Sawa
Ushaambiwa kuna corona,inatosha wewe chukua hatua kama ni kuji-lockdown,au kuji-self isolate vyovyote vile ..unataka kusikia watu wengi wameambukizwa ili iweje??? unataka kujua watu wengi wamekufa ili iweje?..wewe si daktari,hiyo ni kazi ya mamlaka!.kitu usichokijua ni kwamba serikali nyingi zimeficha takwimu halisi za athari za virusi hivi vya corona,kuna watu watakufa na wengine watapona,kisha dunia itaendelea kama kawaida,cha msingi jitahidi kujilinda ili uwe mmoja wa watakaoendelea na dunia
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom