Maswali ambayo utayasikia tena na tena maishani

Malunkwi

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
339
79
1. Mdada anaingia kwenye daladala na viatu vimechongoka anakukanyaga, halafu anakuuliza ‘Samahani umeumia?’

2. Kwenye msiba utakuta watu wanalia,’Kwanini kafa yeye? Jamani kwanini kafa yeye?

3. Mtu anaingia kwenye mgahawa halafu anamuuliza weita,’Biriani yenu nzuri?’

4. Shangazi yako ambaye hamjaonana siku nyingi lazima atatoa, ‘He jamani umekuwa mkubwa’

5. Binti akiwaeleza ndugu zake kapata mchumba wa kumuoa lazima ndugu moja atauliza,’Mtu mwenyewe mzuri?

6. Ukipigiwa simu saa 7 ya usiku tegemea swali,’Vipi nimekuamsha?’

7. Madaktari wa meno wakati wanakuchokonoa meno na vyuma vyao utasikia,’Nambie kama unaumia’

8. Umekaa unaburudika na sigara yako anatokea **** anakuuliza,’Kwa hiyo siku hizi unavuta?’
 
8,,5 ndo bado,,,,,
sigara sivuti,then mi ni male
3 nimewah kusikia nikiwa napata huduma kwenye mamalishe za uswahilin kwangu
 
Yuko ambaye alinipigia usiku...kama saa 7 hivi...akaniambia vp nimekuamsha usingizini..nikamwambia hapana nilikuwa nje naota jua..akakata simu!!
 
mi nlivyopata mchumba hata sikuulizwa kama mchumba angu mzuri, ingawa ni kweli nimeona hlo kwa baadh ya watu
 
# 6 Ukipigiwa simu saa 7 ya usiku tegemea swali,'Vipi nimekuamsha?'

hii huwa inaboa kinoma!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom