Maswali 7 kwa Chadema baada ya Busanda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali 7 kwa Chadema baada ya Busanda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masatu, Jun 6, 2009.

 1. M

  Masatu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  1. Nauliza kwanini Chadema waligawa chupi na sidiria?

  2. Nauliza kwanini Chadema waligawa biskuti?

  3. Nauliza kwa nini Chadema ( wakiongozwa za Ziito Kabwe ) walichoma bendera za CCM?

  4. Nauliza pesa za kukodi chopa zimetoka wapi?

  5. Nauliza kwanini Chadema walipeleka mamluki kutoka Tarime kwenda kufanya fujo?

  6. Nauliza kwanini Chadema walinunua vijana kwenda kwenye mikutano ya CCM na kuzomea?

  7. Nauliza kwanini viongozi wa Chadema walikuwa wakitoka matamshi ya kuchochea uvunjwaji wa amani Busanda?

  Maswali haya yanatakiwa kujibiwa na wafuatao

  1. Freeman Mbowe

  2. Dr Wilbroad Slaa

  3. Zitto Kabwe
   
  Last edited by a moderator: Jun 6, 2009
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MASWALI MAZURI SANA!
  wameonyesha udhaifu mkubwa
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee Kijana,

  Naona hapo umemkoma Nyani giladi. Tatizo la padre inaelekea yuko biased, ningetegemea padre wa mungu achambue mabaya yote kutoka pande zote.

  Pia asilimia 50 ya watu kupiga kura sio jambo la ajabu kabisa. Unless ana ushahidi wa kutosha kuonyesha hao wengine walizuiwa au shahada zao zilinunuliwa, naona argument yake hii ni weak.

  Kwenye viongozi wa serikali kwenda huko, anasahau hata akina Zitto, Dr. Slaa na wengine ni wabunge wa maeneo yao, je na wenye kwenda huko walikuwa likizo sehemu zao za kazi? Kinachotakiwa ni kuwa na utaratibu ambao unaelezea namna ya gharama za waziri au mtumishi yeyote wa serikali kulipiwa anapokuwa kwenye kazi za chama chake. Hapa sio waziri tu, hata wabunge nao wanaguswa na hilo.

  Kuiba kura, kununua shahada, kufanya vurugu wakati wa kampeni, kutumia vyombo vya dola vibaya, vyama kuwa na mamluki wa kuzomea nk. haya yote ni mambo mabaya ambayo inatakiwa tuyakemee kwa nguvu zote.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu MTZ

  Wanasahau turn up ya Tarime pia ilikuwa ni below 50% lakini hakuna alie hoji, mwabaki kutukana tu sasa
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Masatu, maswali yako mazuri sana lakini haya mambo yanawezekana vipi kwa nchi inayojali utawala wa sheria na haki. Labda tukubaliane kuwa viongozi tuliowapa dhamana hiyo wameshindwa na hivyo kutoa mwanya kwa maswali kama yako. Sasa kama ni hivi, uchaguzi ni wa nini kama chama kinachounda serikali ndicho kinara wa uvunjaji wa sheria. Kumbuka Uchaguzi una sheria zake na kuna watu wanalipwa mamilioni ya pesa za walipa kodi kusimamia sheria hizo - ni hawa ndio ninawataka watuambie kwa nini walishindwa kufanya hivyo.

  Kuhusu hela za kukodi chopa, ninachojua kwa hakika ni kuwa Chadema hawakuzipata kwa wizi kama wa EPA na Kagoda.

  Mtanzania, hiyo ya bias sijui lakini inaelekea unakubaliana na Padre kuwa kuna mabaya yalifanyika. Sasa wengine tunachouliza ni kwa nini vyombo vya serikali vilivyopewa dhamana ya kuhakikisha sheria zinafuatwa zinafumbia macho vitendo hivyo - kuilinda CCM ?

  Kwanza kuna ushahidi wa kutosha kuwa shahada zilinunuliwa na mamlaka husika kupewa taarifa, je walichukua hatua gani. Pili matukio ya vitisho vya wazi wazi kwa wapiga kura yaliripotiwa, kweli huoni hili likawa moja ya sababu ya kupungua kwa idadi ya wapiga kura ? Wahusika wakuu kwenye hili walikuwa CCM lakini Tume ya Uchaguzi likiuwa kimya, kwa nini ?

  Mtanzania hapa unanimaliza kabisa - kitendo cha mawaziri wote hao si sahihi na ni endelezo la ufisadi serikalini na kama hili hulioni sina zaidi. Huko nyuma kuna chaguzi nyingi matokeo yake yalibatilishwa kutokana na vitendo vya viongozi hasa mawaziri kutumia rasilimali za serikali kwenye kampeni.

  Sheria zipo na tunachotakiwa kukikemea kwa nguvu zote ni kile cha vyombo husika kufumbia macho vitendo kama hivyo.
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mag3

  U cudnt gaet it! kwa maneno mengine ni kuwa maswali yaliyoulizwa na Padri ni mepesi mno kama pamba.

  Padri anauliza habari ya mawaziri, wakati kila mtu anajua huwezi kuwa waziri bila ya kuwa Mbunge! hivyo hao watajwa walikuwa huko kama wabunge wa CCM, wengine wa NEC nk, sawa kama alivyokwenda Zitto hatuna haja ya kumuuliza alienda kule kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mashirika ya Umma bali tunajua kaenda kama Mbunge na naibu katibu mkuu wa Chadema. Hili halihitaji rocket scientist kujua.

  Padri anataka kujua habari ya low turn out wakati hilo ni tatizo kwa almost kila chaguzi ndogo kuna watu wamehama, wengine wamekufa, wengine just cudnt care ndio demokrasia hiyo. Tatizo hili lilikuwepo hata kule Tarime mkuu mbona Karugendo hajahoji?

  Padri anauliza uhalali wa "Mafisadi" kufanya kampeni, jibu ni rahisi chombo gani cha sheria kilichowahukumu na kuwa "mafisadi" ikiwa kila mtu ataamka asubuhi na kusema fulani fisadi bila ya uhalali wowote wa kisheria na sisi tunakubali then na mimi nasema Slaa, Zitto, mbowe wote mafisadi kwanini wamefanya kampeni? na sijiu ni sheria gani inayomzuia so called "fisadi" kutofanya kampeni.

  Padri anauliza habari za waliokamatwa na shahada. Anakiri wamekamatwa that means wapo kwenye vyombo vya sheria au ana suggests wafungwe hapo hapo?

  Anauliza gharama za CCM sijui ile chopa ni ya charity?

  Aaah bwana we! maswali yenyewe ya ki kindergatten kindergatten not worth my time
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kuna mzito mmoja bongo nilimpa ujumbe mwisho wa last year, nilimtaka akipata nafasi kuchungulia chungulia JF japo kidogo, last week ameniambia kwamba sasa yeye hakosi hapa maana kuna pure ideas, maswali na majibu na huwezi pata hii elimu popote bongo.

  - Mkulu Masatu, ahsante kwa kutuwekea upande wa pili wa hii ishu, kumbe haya yalitokea hata Tarime lakini Mchungaji akawa bubu ila sasa Busanda anataka kusema, sasa imagine zamani tulipokuwa hatuna nguvu za kujua upande wa pili wa ishus as a nation si tulikuwa tunapelekwa mzobe mzobe tu! No wonder tumekwama!

  - Mkuu Masatu, darasa zito sana hili.

  Respect.

  FMEs!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Masatu,
  Hata kama waziri alienda kama mbunge kwa nini alitumia wadhifa wake kama waziri kuhakikisha FFU inawadhibiti wapinzani? Hapa Marekani jambo hilo lisingekubalika kabisa.
   
 9. M

  Masatu JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndio stahiki zao hizo kutumia magari 24/7, unazungumzia marekani sie tupo Bongo sio kila kinachofanyika marekani ni applicable hapa.
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Jasusi,

  Una uhakika na hilo? Ni wapi ambako Wapinzani walidhibitiwa na FFU kwa amri ya Masha?

  Angalia Tarime, polisi walipiga watu, waliweka watu ndani lakini CHADEMA bado wakashinda. Kilichotokea Busanda ni will of the people; they were not coreced into voting CCM. Tukilielewa hilo basi tutawasaidia Upinzani ili wajiandae na kujijenga zaidi. Playing ground is not going to change; inabidi wacheze hivyo hivyo na rafu zote lakini kama wana wachezaji imara, naamini wanaweza kuishinda CCM.

  Hii ya kusema mawaziri waliacha kazi zao kwenda Busanda naona masatu kaliandika vizuri hapo juu. You can't have your cake and eat it too! Ni sawa kwa Zitto kuacha jimbo lake la Kigoma kwenda kupiga kampeni Busanda lakini sio sawa kwa Masha ambaye ni mbunge wa huko huko mwanza kuacha kazi zake zingine kwenda kukisaidia chama chake?

  Haya mambo ukiyaangalia kwa black and white yatakuchanganya hasa.
  Mimi naona kuwe na sheria za kuhakikisha hawa viongozi wanapokuwa kwenye kufanya shughuli za vyama vyao basi wasitumie magari na resources zingine za serikali bila kujali ni wabunge au mawaziri. magari ya wabunge yamenunuliwa kwa pesa za wananchi; je wanapoyatumia kwenye kampeni za vyama vyao ni sahihi?
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Teh teh.....

  amakweli jamiiforums ni bunge tukutu..


  omarilyas
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ndio maana ukiingia mara moja tu hutoki tena, Bwa! ha! ha! ila huyu Padri aache magirini Mungu hapendi makengeza ya kuona CCM tu lakini hawezi ona the otherside, tena kwa makusudi wachungaji wa namna hii watatugawa taifa hawa tusipokuwa makini.

  FMEs!
   
 13. M

  Mkora JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi naomba kusaidia kujibu swali la nne

  Anayelipia chopa ni mtu wa RA anawekeza upande wa pili just incase

  Habari ndio hiyo
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mtanzania,
  Sikumbuki ni gazeti gani lakini ilikuwemo ripoti Masha akiwaambia FFU wafanye kazi yao. Sasa siku zote hajawaambia wafanye kazi yao na wakati wa uchaguzi ndio anawakumbusha kufanya kazi yao? Na tunajua FFU kazi yao ni kuzibiti wapinzani.
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Hapana mkuu hii style ya FFU, Mwalimu aliitoa huko East nchi kama Yugoslavia, Rumania, Chezc, na Bulgaria zote zilikuwa na hawa FFU likes, niliwahi pita na meli huko na kuwaona hawa FFU,

  - Nilipouliza kwa nini wako special sana, maana wananchi walikuwa wanawaogopa sana wakipita mitaani, nikaambiwa kwamba hao ndio hasa walindaji wa sera ya Communism, yaani watawala wa nchi hizo walikuwa wanakusanya watoto wa yatima na kuwapeleka kwenye camps maalum toka wakiwa wadogo, mbali sana na miji ya wananchi huko wanawafundisha unyama tu na kupiga wananchi, sasa siku ikitokea kasheshe ndio wanaletwa kumaliza soo,

  - Zamani bongo FFU, walikuwa na kazi mbili Mpirani na Mlimani, na ninakumbuka enzi hizo wakitokea tu manaanza wenyewe kutimka, nasikia siku hizi wanaitwa kikosi cha kuzuia ghasia, lakini FFU ilikuwa idea ya Mwalimu.

  Respect.

  FMEs!
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lakini siku hizi wanasikika tu kwenye eneo la uchaguzi. Ndio maana wengine tunasema kulikoni? At least kule Tarime enzi za Mwalimu aliwatumia kupambana na ubabe wa wizi wa ng'ombe lakini siku hizi unawasikia tu kunapokaribia uchaguzi. Na wanaong'atwa ni wapinzani.
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Bwa! ha! ha! haya Mkulu Jasusi nimekubali yaishe mkuu maana umenichana sana mbavu hapa Bwa! ha! ah!

  Respect.

  FMEs!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jun 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kama wewe hukuhoji haina maana 'hakuna aliyehoji'!
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Chadema ni political opportunists tu, hawana ajenda yoyote ya maendeleo. Wanaishi kwenye ndoto za kufika mahali fulani ili tu wapate hisia za kuwa huko zilivyo.
  Habari nzuri ni kwamba hizi chaguzi zinawawezesha waliofungua macho kuona, sasa ni juu ya kila aliyeona kama atafanya maamuzi sahihi au lah.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  and how would you describe CCM? the greatest thing to happen to Tanzania since the invention of fire?
   
Loading...