Maswali 3 au 4 ya Ugomvi: Kwa Wanaomlilia Maalim Seif...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Swali la Ijumaa: Nimeona na kusikia kundi la wabunge wakiimba "Maalim Seif, Maalim Seif". Na nimesoma hoja nyingi za kutaka Seif atangazwe mshindi. Hadi hivi sasa sijapata majibu ya kuridhisha na naomba mwenye nayo atusaidie:
1. Wanajuaje Seif kashinda Uchaguzi wa Zanzibar?
2. Kwanini Wanaamini hiyo sababu ya kuwa Seif kashinda?
3. Kwanini wanafikiri ukomo wa Rais wa Zanzibar ni siku yake ya kuapishwa (yaani miaka mitano kamili tangu alipoapishwa)?
4. Kwanini hawakumlilia Lowassa mbele ya Magufuli ambaye naye inadaiwa amepora ushindi na badala yake wamemlilia Seif mbele ya Shein wakati Shein hajatangazwa mshindi au kudai kushinda? Walimfanyia Kikwete kwa sababu waliamini kapora ushindi wa Slaa. Siyo kwamba kwa kutomlilia Lowassa mbele ya Magufuli wamethibitisha kuwa wanamtambua kuwa ni mshindi halali na madai ya Lowassa kuwa ni mshindi hayakuwa na msingi wowote katika ukweli?
 
labda wewe utusaidie ukomo wa rais ni miaka mingapi? kama sio mitano basi tutangaze tu uchifu huko zanzibar
 
Labda swali la kizushi pia.
Tume bado haijatangaza mshindi. Kwa jinsi tume inavyishinikizwa ikitokea ikafaanya maamuzi kulingana na jinsi wanavyoshinikizwa na kumtangaza Dr Shein, nini kitatokea? . Kwa sababu wote hatujui inawezekana kabisa kura za Dr zikawa nyingi kuliko za Maalim Seif. Na tume ikishatangaza basi huwezi kupeleka malaalamiko popote. Labda washabiki wakae wafikirie mara mbili mbili
 
Duuuuh!Kweeli wewe jamaa umeishiwa namna hii?
Siamini kama mtu anayejipambanua kuwa si mnufaika wala mfaidikaji wa mfumo wa elimu mfu ya ccm iliyokuwa na lengo la kuwafanya watanzania mambulula kuwa anaweza uliza maswali ya namna hii!Wengine wanatoka Misri kuelekea Kanaani,wewe ndio unaelekea kurudi Misri,pole sana.
 
Mwanakijiji alikuwa anamsifia JK mwaka 2005-2006. Baadaye akamgeuka baada ya kuona ameachwa kwenye mataa. Ndivyo alivyo.
 
kweli wahenga walisema akili nyingi huondoa maarifa,Mzee Mwanakijiji MAHABA YAMEKUFANYA UWE WA HOVYO SANA KULIKO HATA KULIKO HATA JINGALAO
 
Swali la Ijumaa: Nimeona na kusikia kundi la wabunge wakiimba "Maalim Seif, Maalim Seif". Na nimesoma hoja nyingi za kutaka Seif atangazwe mshindi. Hadi hivi sasa sijapata majibu ya kuridhisha na naomba mwenye nayo atusaidie:
1. Wanajuaje Seif kashinda Uchaguzi wa Zanzibar?
2. Kwanini Wanaamini hiyo sababu ya kuwa Seif kashinda?
3. Kwanini wanafikiri ukomo wa Rais wa Zanzibar ni siku yake ya kuapishwa (yaani miaka mitano kamili tangu alipoapishwa)?
4. Kwanini hawakumlilia Lowassa mbele ya Magufuli ambaye naye inadaiwa amepora ushindi na badala yake wamemlilia Seif mbele ya Shein wakati Shein hajatangazwa mshindi au kudai kushinda? Walimfanyia Kikwete kwa sababu waliamini kapora ushindi wa Slaa. Siyo kwamba kwa kutomlilia Lowassa mbele ya Magufuli wamethibitisha kuwa wanamtambua kuwa ni mshindi halali na madai ya Lowassa kuwa ni mshindi hayakuwa na msingi wowote katika ukweli?

Wewe ni Mwanakijiji ninae soma mabandiko yake humu JF au ni mwingine ametumia jina lako maana sidhani Mzee Mwanakijiji nilie mzoea anaweza uliza maswali ya hi yo..!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom