Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Rtbkazoba

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2016
Posts
261
Reaction score
210
MASWALI 11 KUHUSU 'UJAMBAZI' WA BABA ASKOFU DALLU

upload_2017-7-23_13-48-51.png

Kupitia gazeti la Kiongozi, ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, Mhashamu Damian Dallu, amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

"Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."

Ameelezwa kushangazwa na watu wanaoongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi walio shuleni. "Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?" Alihoji.

Hata hivyo, hakuna mwanaharakati anayeongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi, kama Askofu Dallu anavyodai.

Kinachoongelewa na baadhi ya wanaharakati ni "haki ya kufanya tendo la ngono" waliyo nayo vijana ambao wamekwisha balehe, lakini bado ni matineja--vijana walio chini ya miaka 18.

Kwa hiyo, Askofu Dallu hapa ametengeneza "hoja-mwanasesere" (straw man), kuishambulia, na kujiona amefanya uenjilishaji wa uhakika, kwa kutumia mbinu halali.

Askofu Dallu anaendelea kuhoji tena, " Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena [shuleni] na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?'”

Hapa, Askofu Dullu ameuliza maswali mawili kwa mpigo. Hebu tuyatenganishe maswali ya Askofu Dallu ili yaweze kujibika vizuri, baada ya kuonyesha ulaghai wa kifalsafa anaoutumia.

Askofu Dallu, hapa ameuliza maswali mawili yafuatayo:
  1. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya kwanza aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
  2. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya pili aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
Katika namna yake ya kuuliza maswali haya mawili kwa mpigo, ametumia silaha za ujambazi wa kifalsafa kuwaburuza wasikilizaji wake. Yaani, anatumia silaha mbili za kutekeleza ujambazi wa kifalsafa--"the fallacy of loaded question" na "the fallacy of slippery slope."

Kwanza anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of loaded question." Kwa ufupi, the fallacy of loaded question assumes a particular answer to another unasked question. Mfano wake ni huu, “Umekwisha acha kumpiga mkeo?” Swali hili linaulizwa kwa kuzingatia dhahania kwamba, tayari umekwisha jibu “ndiyo” kwa swali, “Je, huwa unampiga mkeo?”, swali ambalo, kwa kweli halijaulizwa kabisa.

Anafikiri kuwa, kwa vile wanaharakati wanatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la kwanza, basi wamekwishatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la pili. Sio kweli. Hilo ni swali ambalo bado halijajibiwa na yeyote. Njadala bado unaendelea.

Na pili anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of slippery slope."
Kwa ufupi, according to the slippery-slope fallacy, if we permit a certain action, then all actions of this type, even the most extreme ones, will soon be permissible. In other words, once we start down the slope or (to vary the metaphor) get a foot in the door, there is no holding back. We commit the slippery-slope fallacy when evidence does not support this predicted outcome.

Kwa kutumia ulaghai huu, Askofu Dallu anasema bila ushahidi usiokanushika, kwamba, kama mwanafunzi aliyezaa mara moja ataruhusiwa kurudi shuleni, basi atapata sababu ya kuzaa mtoto wa pili, automatically! Kweli?

Hayo yote tisa. Kumi ni hoja ya Askofu Dallu ifuatayo, na inayopaswa kutufikirisha sana kuhusu namna baadhi ya Maaskofu wanavyotekeleza majukumu yao:

Askofu Dallu amejenga hoja ifuatayo:
  1. Kama "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] yangekuwa sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," basi yangekuwa halali.
  2. Lakini, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] sio sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," badala yake, "ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."
  3. Kwa hiyo, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo]" ni haramu.
  4. Hivyo, "hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo" ni halali.
Kimuundo, hoja hii iko sawa. Lakini kimaudhui ni hoja mbaya. Yaani, baadhi ya madokezo yake sio ya kweli hata kidogo.

Kwa sababu ya ubovu wa kimaudhui katika hoja hii, ninayo maswali kadhaa kwa Baba Askofu Dallu.

Hapa Afrika, kabla ya ujio wa wageni, tulikuwa na mfumo wa elimu isiyo rasmi, familia zikiwa ni kitovu cha utekelezaji wake. Kabla ya kuja kwa wageni, mabinti walikuwa wanabeba mimba, kama ambavyo misamiati ya kimila kuhusu uwepo wa mimba kabla ya ndoa inavyoonyesha. Kule kwetu, tunaziita "ensinjo."
  1. Kama hivyo ndivyo, kabla ya ujio wa wageni, hawa mabinti zetu walikuwa wanatupwa jalalani baada ya kupata "mimba ya utotoni" tena kabla ya ndoa?
  2. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu elimu inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kielimu?
  3. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu ujinsia inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kijinsia?
  4. Je, sheria asilia ya maadili inasema kuwa maslahi ya kijinsia yana kipaumbele kikubwa zaidi ya maslahi ya kielimu?
  5. Je, sheria asilia ya maadili inasema nini kuhusu uchumi, afya, mazingira, siasa, na sekta nyingine za maisha ya binadamu?
  6. Mbona baadhi ya Maaskofu, nawe ukiwemo, hamsikiki kuongelea maadili katika sekta hizi baki?
  7. Neno maadili linamaanisha "maadili ya ngono" pekee?
  8. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of loaded question?"
  9. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of slippery slope?"
  10. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ngono?
  11. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ndoa?

Mwisho, niseme tu kwamba, baadhi ya waumini makini tungependa kuwasikia Maaskofu wetu mkijadili uhusiano uliopo kati ya sheria asilia ya maadili, kwa upande mmoja, na mdororo wa uchumi, uharibifu wa mazingira, wananchi kuwekwa rumande kwa siku 7 bila kupelekwa mahakamani, kwa upande mwingine. Hatuwasikii.

Ni kama vile ajenda kuu ya Kanisa ni kusimamia maadili ya gono.
Why?

Napendekeza kuwa Maaskofu Katoliki wajitafakari juu ya utume wao, wakiongozwa na Askofu Dallu.

Najua wanafanya kazi nzuri, lakini wakati mwingine wanaangukia pua...

RtbKazoba--Retired Bishop Kazoba
 
Viongozi wa dini wengi wao hawaishi kadri maandiko yao yanavyosema hususani kuhusu kutenda haki na hukumu

wanaunga mkono maneno ya watawala kwa kuwa wanakaa nao meza moja wakati wa "kumega mkate" hata wanaposea huwasikii wakiwakemea ila utawasikia tu pale masilahi yao yanapoguswa
 
Ni kawaida kwa watu waovu kuikataa mantiki siku zote na badala yake hukimbilia visingizio. Umewahi kujiuliza ni kwa nini watu wa ulaya na USA waliamini kwamba Irak inamiliki silaha za maangamizi? Silaha hizo zilipokosekana vikatafutwa visingizio kwamba Saddam Hussen alikuwa ni Dikteta hivyo ni halali kwake kupinduliwa na kuuawa!!

Hongera sana kwako Rtbkazoba kwa bandiko lako lililosheheni mantiki.
 
Usihangaike sana na Kanisa awamu hii, litaunga mkono pasipo kuhoji kila kitakachosemwa na Mkuu katika awamu hii.

Hii kauli ingekuwa ilitolewa na Rais Mwislamu basi ungeona matakamko kona zote za nchi.
Hayo ni mawazo Mgando,kutoa kauli haitegemei mkuu wa nchi ni Dini gani. Busara hupatikani kwa Uvivu na uzembe wa kujituma kufikiri kwa umakini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MASWALI 11 KWA BABA ASKOFU DALLU

image-jpeg.547182

Kupitia gazeti la Kiongozi, ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, Mhashamu Damian Dallu, amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

"Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."

Ameelezwa kushangazwa na watu wanaoongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi walio shuleni. "Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?" Alihoji.

Hata hivyo, hakuna mwanaharakati anayeongelea "haki ya tendo la ndoa" kama Askofu Dallu anavyodai. Kinachoongelewa na wanaharakati ni "haki ya tendo la ngono." Kwa hiyo, Askofu Dallu hapa ametengeneza "hoja-mwanasesere" (straw man), kuishambulia, na kujiona amefanya uenjilishaji wa uhakika, kwa kutumia mbinu halali.

Askofu Dallu anaendelea kuhoji tena, " Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena [shuleni] na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?'”

Hapa, Askofu Dullu ameuliza maswali mawili kwa mpigo. Hebu tuyatenganishe maswali ya Askofu Dallu ili yaweze kujibika vizuri, baada ya kuonyesha ulaghai wa kifalsafa anaoutumia.

Askofu Dallu, hapa ameuliza maswali mawili yafuatayo:
  1. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya kwanza aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
  2. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya pili aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
Kuna ulaghai katika namna yake ya kuuliza maswali haya mawili kwa mpigo. Yaani, anatumia silaha mbili za kutekeleza ujambazi wa kifalsafa.

Kwanza anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of loaded question." Kwa ufupi, the fallacy of loaded question assumes a particular answer to another unasked question. Mfano wake ni huu, “Umekwisha acha kumpiga mkeo?” Swali hili linaulizwa kwa kuzingatia dhahania kwamba, tayari umekwisha jibu “ndiyo” kwa swali, “Je, huwa unampiga mkeo?”, swali ambalo, kwa kweli halijaulizwa kabisa.

Anafikiri kuwa, kwa vile wanaharakati wanatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la kwanza, basi wamekwishatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la pili. Sio kweli. Hilo ni swali ambalo bado halijajibiwa na yeyote. Njadala bado unaendelea.

Na pili anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of slippery slope."
Kwa ufupi, according to the slippery-slope fallacy, if we permit a certain action, then all actions of this type, even the most extreme ones, will soon be permissible. In other words, once we start down the slope or (to vary the metaphor) get a foot in the door, there is no holding back. We commit the slippery-slope fallacy when evidence does not support this predicted outcome.

Kwa kutumia ulaghai huu, Askofu Dallu anasema bila ushahidi usiokanushika, kwamba, kama mwanafunzi aliyezaa mara moja ataruhusiwa kurudi shuleni, basi atapata sababu ya kuzaa mtoto wa pili, automatically! Kweli?

Hayo yote tisa. Kumi ni hoja ya Askofu Dallu ifuatayo, na inayopaswa kutufikirisha sana kuhusu namna baadhi ya Maaskofu wanavyotekeleza majukumu yao:

Askofu Dallu amejenga hoja ifuatayo:
  1. Kama "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] yangekuwa sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," basi yangekuwa halali.
  2. Lakini, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] sio sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," badala yake, "ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."
  3. Kwa hiyo, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo]" ni haramu.
  4. Hivyo, "hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo" ni halali.
Kwa sababu ya hoja hii, ninayo maswali kadhaa kwa Baba Askofu Dallu.

Hapa Afrika, kabla ya ujio wa wageni, tulikuwa na mfumo wa elimu isiyo rasmi, familia zikiwa ni kitovu cha utekelezaji wake. Kabla ya kuja kwa wageni, mabinti walikuwa wanabeba mimba, kama ambavyo misamiati ya kimila kuhusu uwepo wa mimba kabla ya ndoa inavyoonyesha. Kule kwetu, tunaziita "ensinjo."
  1. Kama hivyo ndivyo, kabla ya ujio wa wageni, hawa mabinti zetu walikuwa wanatupwa jalalani baada ya kupata "ensinjo"?
  2. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu elimu inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kielimu?
  3. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu ujinsia inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kijinsia?
  4. Je, sheria asilia ya maadili inasema kuwa maslahi ya kijinsia yana kipaumbele kikubwa zaidi ya maslahi ya kielimu?
  5. Je, sheria asilia ya maadili inasema nini kuhusu uchumi, afya, mazingira, siasa, na sekta nyingine za maisha ya binadamu?
  6. Mbona baadhi ya Maaskofu, nawe ukiwemo, hamsikiki kuongelea maadili katika sekta hizi baki?
  7. Neno maadili linamaanisha "maadili ya ngono" pekee?
  8. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of loaded question?"
  9. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of lslippery slope?"
  10. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ngono?
  11. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ndoa?

Mwisho, niseme tu kwamba, baadhi ya waumini makini tungependa kuwasikia Maaskofu wetu mkijadili uhusiano uliopo kati ya sheria asilia ya maadili, kwa upande mmoja, na mdororo wa uchumi, uharibifu wa mazingira, wananchi kuwekwa rumande kwa siku 7 bila kupelekwa mahalamani, kwa upande mwingine. Hatuwasikii.

Ni kama vile ajenda kuu ya Kanisa ni kusimamia maadili ya gono.
Why?

Napendekeza kuwa wajitafakari juu ya utume wao, wakiongozwa na Askofu Dallu.
Kazoba, muulize Dallu, katika Kanisa/dini/mafundisho, kuna dhana ya kusameeana? Tunafundishwa kusamehe, sasa yeye anatufundisha nini? Yesu anasema msamehe mwenzako “…hata saba mara sabini” Matayo 18:22.
“Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi” Waefese 4:31-32.

mapadri wangapi wanazini, wanalawiti, wanalewa na bado wanaendelea na utume chini ya msamaha wa Askofu?

Mwisho nimuulize Dallu, Ukatoliki ni utamaduni wa Mwafrika? Bukoba ukatoliki umeletwa lini? Walikuwa na utamaduni wa Ukatoliki kabla ya kuja hao wazungu na dini?
MWISHO NIKUSHUKURU KWA SOMO LA FALSAFA.
 
Usihangaike sana na Kanisa awamu hii, litaunga mkono pasipo kuhoji kila kitakachosemwa na Mkuu katika awamu hii.

Hii kauli ingekuwa ilitolewa na Rais Mwislamu basi ungeona matakamko kona zote za nchi.
Chuki zinakusumbua

Waambie basi Masheikh na Wanazuoni wakiislamu walipize kwa kutoa matamko juu ya Magufuli
 
MASWALI 11 KWA BABA ASKOFU DALLU

image-jpeg.547182

Kupitia gazeti la Kiongozi, ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, Mhashamu Damian Dallu, amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

"Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."

Ameelezwa kushangazwa na watu wanaoongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi walio shuleni. "Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?" Alihoji.

Hata hivyo, hakuna mwanaharakati anayeongelea "haki ya tendo la ndoa" kama Askofu Dallu anavyodai. Kinachoongelewa na wanaharakati ni "haki ya tendo la ngono." Kwa hiyo, Askofu Dallu hapa ametengeneza "hoja-mwanasesere" (straw man), kuishambulia, na kujiona amefanya uenjilishaji wa uhakika, kwa kutumia mbinu halali.

Askofu Dallu anaendelea kuhoji tena, " Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena [shuleni] na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?'”

Hapa, Askofu Dullu ameuliza maswali mawili kwa mpigo. Hebu tuyatenganishe maswali ya Askofu Dallu ili yaweze kujibika vizuri, baada ya kuonyesha ulaghai wa kifalsafa anaoutumia.

Askofu Dallu, hapa ameuliza maswali mawili yafuatayo:
  1. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya kwanza aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
  2. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya pili aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
Kuna ulaghai katika namna yake ya kuuliza maswali haya mawili kwa mpigo. Yaani, anatumia silaha mbili za kutekeleza ujambazi wa kifalsafa.

Kwanza anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of loaded question." Kwa ufupi, the fallacy of loaded question assumes a particular answer to another unasked question. Mfano wake ni huu, “Umekwisha acha kumpiga mkeo?” Swali hili linaulizwa kwa kuzingatia dhahania kwamba, tayari umekwisha jibu “ndiyo” kwa swali, “Je, huwa unampiga mkeo?”, swali ambalo, kwa kweli halijaulizwa kabisa.

Anafikiri kuwa, kwa vile wanaharakati wanatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la kwanza, basi wamekwishatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la pili. Sio kweli. Hilo ni swali ambalo bado halijajibiwa na yeyote. Njadala bado unaendelea.

Na pili anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of slippery slope."
Kwa ufupi, according to the slippery-slope fallacy, if we permit a certain action, then all actions of this type, even the most extreme ones, will soon be permissible. In other words, once we start down the slope or (to vary the metaphor) get a foot in the door, there is no holding back. We commit the slippery-slope fallacy when evidence does not support this predicted outcome.

Kwa kutumia ulaghai huu, Askofu Dallu anasema bila ushahidi usiokanushika, kwamba, kama mwanafunzi aliyezaa mara moja ataruhusiwa kurudi shuleni, basi atapata sababu ya kuzaa mtoto wa pili, automatically! Kweli?

Hayo yote tisa. Kumi ni hoja ya Askofu Dallu ifuatayo, na inayopaswa kutufikirisha sana kuhusu namna baadhi ya Maaskofu wanavyotekeleza majukumu yao:

Askofu Dallu amejenga hoja ifuatayo:
  1. Kama "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] yangekuwa sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," basi yangekuwa halali.
  2. Lakini, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] sio sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," badala yake, "ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."
  3. Kwa hiyo, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo]" ni haramu.
  4. Hivyo, "hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo" ni halali.
Kwa sababu ya hoja hii, ninayo maswali kadhaa kwa Baba Askofu Dallu.

Hapa Afrika, kabla ya ujio wa wageni, tulikuwa na mfumo wa elimu isiyo rasmi, familia zikiwa ni kitovu cha utekelezaji wake. Kabla ya kuja kwa wageni, mabinti walikuwa wanabeba mimba, kama ambavyo misamiati ya kimila kuhusu uwepo wa mimba kabla ya ndoa inavyoonyesha. Kule kwetu, tunaziita "ensinjo."
  1. Kama hivyo ndivyo, kabla ya ujio wa wageni, hawa mabinti zetu walikuwa wanatupwa jalalani baada ya kupata "ensinjo"?
  2. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu elimu inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kielimu?
  3. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu ujinsia inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kijinsia?
  4. Je, sheria asilia ya maadili inasema kuwa maslahi ya kijinsia yana kipaumbele kikubwa zaidi ya maslahi ya kielimu?
  5. Je, sheria asilia ya maadili inasema nini kuhusu uchumi, afya, mazingira, siasa, na sekta nyingine za maisha ya binadamu?
  6. Mbona baadhi ya Maaskofu, nawe ukiwemo, hamsikiki kuongelea maadili katika sekta hizi baki?
  7. Neno maadili linamaanisha "maadili ya ngono" pekee?
  8. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of loaded question?"
  9. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of lslippery slope?"
  10. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ngono?
  11. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ndoa?

Mwisho, niseme tu kwamba, baadhi ya waumini makini tungependa kuwasikia Maaskofu wetu mkijadili uhusiano uliopo kati ya sheria asilia ya maadili, kwa upande mmoja, na mdororo wa uchumi, uharibifu wa mazingira, wananchi kuwekwa rumande kwa siku 7 bila kupelekwa mahalamani, kwa upande mwingine. Hatuwasikii.

Ni kama vile ajenda kuu ya Kanisa ni kusimamia maadili ya gono.
Why?

Napendekeza kuwa wajitafakari juu ya utume wao, wakiongozwa na Askofu Dallu.
Hakuna sehemu ktk vyuo Vya ualimu nchini kwa ngazi ya astashahada au stashahada ambavyo mwalimu anafundishwa jinsi ya kumfundisha Mzazi mwenye mtoto.........yaani wanafunzi mjamzito au ana mtoto halafu aendelee kubaki shule??? Wakati keshafundishwa good manners akiwa kidato cha kwanza na akashindwa.......acheni sanaa ktk Elimu. Kama ameshindwa kusoma aangalie utaratibu mwingine wa maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumsamehe Bure Baba Askofu Hajui Alitendalo Maana Ukitazama Vizuri Tunaye Baba Askofu Wa Escrow Wa Jimbo La Rulenge Ngara Tunangoja Kuona Hatua Atakazochukuliwa Hivi Punde
 
Hawa maaskofu wanafiki sana. Hivi wao na mapadri wao wanavyotoka na wake za watu na tunawaona na kuwajua tumwambie Pope awafukuze kabisa huo uaskofu?
 
Askofu kamaliza, kasema wazi hakuna Shule ya Kanisa Katoliki itakayoruhusu mimba. Huo ndiyo msimamo; wewe unamhoji Askofu ukiwa kama nani? Kama nia yako ni kuwagurahisha CHADEMA au mashoga, go ahead. Hapa ndiyo mahala pake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom