Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,071
Mimi ninapomsikia Kiongozi wa dini anapokuja Kujenga hoja yake, na kuishia kujikita tu kwa kusema kitu fulani sio 'utamaduni' wetu, huwa mara zote najiuliza maswali haya...
1/Toka lini Ukristo na uislamu vikawa ni utamaduni wa Mwafrika?
2/Toka lini Uvaaji wa nguo kufunika miili yetu na kutusitiri vyema miili yetu vikawa utamaduni wa mwafrika?
3/Toka lini kwenda hospitali kutibiwa kwa sindano, vidonge, chanjo, operesheni nk vikawa utamaduni wa mwafrika?
4/Kwanini utamaduni wa asili wa mwamfrika wa kutambika, kuroga, kuagua tunaupiga vita sasa? (Kwa sasa viongozi wa dini wanasema tuache hayo ili tutumie Dua, sala na maombi tu)
5/Kwanini utamaduni wa asili wa jamii nyingi za kiafrika wa kukeketa wanawake tunaupiga vita?
6/Toka lini kwenda shule na vyuo vikawa ni utamaduni wa mwafrika?
7/Kwanini tamaduni za kiafrika za kurithi mke wa marehemu tunazipiga vita sasa?
8/Kwanini tamaduni za kiafrika za kuwaangamiza watoto wenye aina fulani hivi za kasoro za kimaumbile(Kama ulemavu) tunazipiga vita?
9/Tangu lini ushenzi wa kujamiiana(Ubakaji, Ulawiti, Ushoga, Usagaji) leo hii umekuwa utamaduni wa kigeni wakati huo uchafu umekuwepo kwenye jamii na tamaduni za kiafrika toka enzi na enzi na hakuonekana kama ni tatizo kwao?
10/Kwanini utamaduni wa Kuendekeza ujinga na uchafu uliokuwepo kwenye maisha ya kila siku ya mwafrika tunapambana kuupiga vita sasa? (Leo hii tunahimizwa tuwe na vyoo visafi na vya kisasa wakati utamaduni wa mwafrika ulikuwa ni kujisaidia vichakani tu ili kuongeza rutuba mashambani!!)
11/Hivi utamaduni wa kusafiria Pikipiki, Magari, Ndege nk. tumeutoa wapi wakati utamaduni wa mwafrika ni kutembea kwa miguu au kupanda Punda nk.
12/Hivi utamaduni wa Kula kwa vijiko, kunawa mikono kabla ya kula, Kutumia simu za mkononi, Tv, Radio, Mitandao hivi waafrika tumeuiga wapi?