Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Huyu mkuu bado yuko mbali kweli...hivi bado tuna hoja za rais muislam na mkristu..?

germve himself
 
akitoa ufafamuzi kuhusu wake mapandre na maaakofu wanaowalawiti watoto wakiumee mnitag na mimi.
 
Umeandika vizuri,ila huwezi kuwa unahangaika kutafuta pesa ,kisha unasomesha mwanao au nduguyo wa kike kumbe yeye tamaa za mapenzi ndo ziko mbele kuliko elimu ,hakika hili jambo halikubaliki. Sisi tunaosomesha tunajua maumivu yake ,ndo maana tunawaasa sana. Ukiruhusu MTU kuzaa na kuja shule ,uneruhusu uzinifu.
Tendo la ndoa hufanywa na wanandoa,, ndo maana hakuna maadili siku hizi. Mabinti wanapewa mimba na wauza viepe (chips) na Bodaboda kisha wanawatelekeza,kisha kazi inakuwa kwako kulea mtoto wa mwanaume mwenzio,kibaya zaidi hawa mabinti wanawakinngia kifua hao waliowapa ujauzito "wakisema wanawapenda sana" tena hutishia kujiua unapomwuliza maswali mengi.

Kiufupi mambo mawili hayachanganyikani .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mavazi yake tu yanaonesha si utamaduni wake zaidi ya kuendeleza utamaduni wa wayahudi

tamaduni wetu ni kaniki na kusalia panapo miti mikubwa, vichuguu na makaburini

baba askofu anajua wazi kwamba tumeacha kuwa kumbuka mababu zetu tumebaki kuwa kumbuka na kuwaombea mababu wa kiyahudi, eti wao ndio wanafaa kukumbukwa na kuombewa

kwa ufupi amepotoka arudi kwenye misingi yetu
 
MASWALI 11 KUHUSU 'UJAMBAZI' WA BABA ASKOFU DALLU


Kupitia gazeti la Kiongozi, ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, Mhashamu Damian Dallu, amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

"Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."

Ameelezwa kushangazwa na watu wanaoongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi walio shuleni. "Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?" Alihoji.

Hata hivyo, hakuna mwanaharakati anayeongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi, kama Askofu Dallu anavyodai.

Kinachoongelewa na baadhi ya wanaharakati ni "haki ya kufanya tendo la ngono" waliyo nayo vijana ambao wamekwisha balehe, lakini bado ni matineja--vijana walio chini ya miaka 18.

Kwa hiyo, Askofu Dallu hapa ametengeneza "hoja-mwanasesere" (straw man), kuishambulia, na kujiona amefanya uenjilishaji wa uhakika, kwa kutumia mbinu halali.

Askofu Dallu anaendelea kuhoji tena, " Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena [shuleni] na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?'”

Hapa, Askofu Dullu ameuliza maswali mawili kwa mpigo. Hebu tuyatenganishe maswali ya Askofu Dallu ili yaweze kujibika vizuri, baada ya kuonyesha ulaghai wa kifalsafa anaoutumia.

Askofu Dallu, hapa ameuliza maswali mawili yafuatayo:
  1. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya kwanza aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
  2. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya pili aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
Katika namna yake ya kuuliza maswali haya mawili kwa mpigo, ametumia silaha za ujambazi wa kifalsafa kuwaburuza wasikilizaji wake. Yaani, anatumia silaha mbili za kutekeleza ujambazi wa kifalsafa--"the fallacy of loaded question" na "the fallacy of slippery slope."

Kwanza anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of loaded question." Kwa ufupi, the fallacy of loaded question assumes a particular answer to another unasked question. Mfano wake ni huu, “Umekwisha acha kumpiga mkeo?” Swali hili linaulizwa kwa kuzingatia dhahania kwamba, tayari umekwisha jibu “ndiyo” kwa swali, “Je, huwa unampiga mkeo?”, swali ambalo, kwa kweli halijaulizwa kabisa.

Anafikiri kuwa, kwa vile wanaharakati wanatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la kwanza, basi wamekwishatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la pili. Sio kweli. Hilo ni swali ambalo bado halijajibiwa na yeyote. Njadala bado unaendelea.

Na pili anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of slippery slope."
Kwa ufupi, according to the slippery-slope fallacy, if we permit a certain action, then all actions of this type, even the most extreme ones, will soon be permissible. In other words, once we start down the slope or (to vary the metaphor) get a foot in the door, there is no holding back. We commit the slippery-slope fallacy when evidence does not support this predicted outcome.

Kwa kutumia ulaghai huu, Askofu Dallu anasema bila ushahidi usiokanushika, kwamba, kama mwanafunzi aliyezaa mara moja ataruhusiwa kurudi shuleni, basi atapata sababu ya kuzaa mtoto wa pili, automatically! Kweli?

Hayo yote tisa. Kumi ni hoja ya Askofu Dallu ifuatayo, na inayopaswa kutufikirisha sana kuhusu namna baadhi ya Maaskofu wanavyotekeleza majukumu yao:

Askofu Dallu amejenga hoja ifuatayo:
  1. Kama "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] yangekuwa sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," basi yangekuwa halali.
  2. Lakini, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] sio sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," badala yake, "ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."
  3. Kwa hiyo, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo]" ni haramu.
  4. Hivyo, "hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo" ni halali.
Kimuundo, hoja hii iko sawa. Lakini kimaudhui ni hoja mbaya. Yaani, baadhi ya madokezo yake sio ya kweli hata kidogo.

Kwa sababu ya ubovu wa kimaudhui katika hoja hii, ninayo maswali kadhaa kwa Baba Askofu Dallu.

Hapa Afrika, kabla ya ujio wa wageni, tulikuwa na mfumo wa elimu isiyo rasmi, familia zikiwa ni kitovu cha utekelezaji wake. Kabla ya kuja kwa wageni, mabinti walikuwa wanabeba mimba, kama ambavyo misamiati ya kimila kuhusu uwepo wa mimba kabla ya ndoa inavyoonyesha. Kule kwetu, tunaziita "ensinjo."
  1. Kama hivyo ndivyo, kabla ya ujio wa wageni, hawa mabinti zetu walikuwa wanatupwa jalalani baada ya kupata "mimba ya utotoni" tena kabla ya ndoa?
  2. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu elimu inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kielimu?
  3. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu ujinsia inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kijinsia?
  4. Je, sheria asilia ya maadili inasema kuwa maslahi ya kijinsia yana kipaumbele kikubwa zaidi ya maslahi ya kielimu?
  5. Je, sheria asilia ya maadili inasema nini kuhusu uchumi, afya, mazingira, siasa, na sekta nyingine za maisha ya binadamu?
  6. Mbona baadhi ya Maaskofu, nawe ukiwemo, hamsikiki kuongelea maadili katika sekta hizi baki?
  7. Neno maadili linamaanisha "maadili ya ngono" pekee?
  8. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of loaded question?"
  9. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of slippery slope?"
  10. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ngono?
  11. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ndoa?

Mwisho, niseme tu kwamba, baadhi ya waumini makini tungependa kuwasikia Maaskofu wetu mkijadili uhusiano uliopo kati ya sheria asilia ya maadili, kwa upande mmoja, na mdororo wa uchumi, uharibifu wa mazingira, wananchi kuwekwa rumande kwa siku 7 bila kupelekwa mahakamani, kwa upande mwingine. Hatuwasikii.

Ni kama vile ajenda kuu ya Kanisa ni kusimamia maadili ya gono.
Why?

Napendekeza kuwa Maaskofu Katoliki wajitafakari juu ya utume wao, wakiongozwa na Askofu Dallu.

Najua wanafanya kazi nzuri, lakini wakati mwingine wanaangukia pua...

RtbKazoba--Retired Bishop Kazoba

Hiki ni kipindi ambacho Kanisa kwa ujumla wake limekuwa na kigugumizi tangu Tanzania kupata uhuru.
Dhana ya utamaduni wa mwafrika nadhani ni ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia, nasema hivo kwa sababu hata hili kanisa analo liongoza yeye halikuwa utamaduni wa kiafrika. Kama kweli Askofu anaamini katika utamaduni wa kiafrika kwanza yeye atoe rozari alovaa shingoni, kwani siyo utamaduni wetu. Zama za mababu zetu kihistoria walivaa shanga, pembe, manyoa ya wanyama nk.

Ikiwa baba askofu anataka tufuate utamaduni kanisa analongooza liliruhusu mapadri kuoa kwani kutokuoa haukuwa utamaduni wa kiafrika, waafrika waliruhusiwa kuoa tena zaidi ya mke mmoja, Utamaduni wa mwafrika ni upi anaongelea askofu?

Utamaduni wa afrika ni kina dada kutokuolewa na kuruhusiwa kuzaa kwa misingi ya usista? Utamaduni wa mwafrika ni upi?

Anasema kanisa litakuwa na masisita wa aina gani? Je anataka kutuaminisha kuwa wote waliosoma hizo shule anazoongelea ni masisita leo? Hapana askofu huu siyo utamaduni wa kiafrika unaohubiri yeye. Ingekuwa vizuri kama ungeongelea maadili zaidi, Umejiuliza hawa wanaopata mimba mashuleni ni watoto wa familia za uwezo gani wa kipato zaidi?

Baba askofu asingetaja utamaduni ningemwelewa. Kama kanisa mungejaribu kutafuta changamoto kwa nini watoto wanapata mimba mashuleni na jinsi ya kusaidia.

Baba askofu mbona kanisa lako ndo linaongoza kwa kwesi za kudharirisha watoto kote duniani? au unataka tuwafungie ndani kama ilivokuwa utamaduni wa kanisa kuwafungia wasichana wote wanaopata ujauzito na hatimaye wakaishiakuolewa na walinzi na madereva wenu maaskofu.

Askofu rudi katika magoti tafakari na Mungu wako kuhusu hili tamko lako. Yesu asingekufa msalabani kama kusingekuwa na msamaha wa dhambi, lakini pia biblia ama maandiko yanatuzuia tusihukumu tusijehukumiwa.
 
mavazi yake tu yanaonesha si utamaduni wake zaidi ya kuendeleza utamaduni wa wayahudi

tamaduni wetu ni kaniki na kusalia panapo miti mikubwa, vichuguu na makaburini

baba askofu anajua wazi kwamba tumeacha kuwa kumbuka mababu zetu tumebaki kuwa kumbuka na kuwaombea mababu wa kiyahudi, eti wao ndio wanafaa kukumbukwa na kuombewa

kwa ufupi amepotoka arudi kwenye misingi yetu

Unadhani njia sahihi ya kudhibiti tamaa ni kumzuia kwenda shule? Unatoka kusema wewe hukuwahi kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa? Hii sheria ilikuwepo toka zamani je imeshazuia mimba kwa kiasi gani? hebu lete takwimu. Ni rahisi sana kuongea hapa mtandaoni na kujinasibu eti wewe unasomesha, hebu sasa fikiria tayari amezaa na ametelekezwa hapo kwako asipomrudisha shule ina maana yeye ataendeelea kuwa jobless na mtoto wake pia ni jobless, maanake utaendelea kulea binti yako na mjukuu. Ni vema ukamsaidia huyo binti ili baadae aweze kusimama. Tofauti na hapo ni mzigo wako mpaka siku unaenda kaburini.
 
Ukweli in za ghali yaani wanasoma wenye nazo tuu...ila uache uongo seminary nyingi zimejengwa na wafadhili sio waamini

germve himself
Kwa mtazamo wako shule za Kanisa ni seminary tu, si ndiyo eeh?
 
Awamu ya mkatoliki mwenzao, ingekuwa awamu ya muislam Kikwete wangepishana kutoa matamko.
 
Wanaharakati wetu mara nyingi wanashangaza sana! Hivi sasa wanapambana mabinti waliopata mimba waruhusiwe kuendelea na masomo wakati huohuo wanapinga ndoa za utotoni! Sasa vipi kupata mimba nje ya ndoa iwe sawa na binti aonewe huruma na kuruhusiwa kurudi shule ilhali akiolewa iwe tabu?! Leo hii ukioa binti aliyemaliza shule ya msingi hivi karibuni na hakubahatika kuendelea na elimu ya sekondari jamii nzima inakugeukia lakini wale wanaowatandika hawa mabinti nje ya ndoa wanaonekana sawa tu! Wala huwezi kuwasikia wanaharakati wetu wakikemea vitendo vya ukahaba vinavyofanywa na mabinti wadogo kabisa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar. Kwao wao shida ni pale binti anapoolewa lakini anapozini hakuna shida. Tuache unafiki na huu ushetani.
Nimekuelewa sana, yah man

Jamii Forums mobile app
 
Wanatamani dunia ingekuwa yao peke yao

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli. Wanaipupia sana dunia kiasi kwamba wapo tayari kuua au kuwaharibia wenzao maisha ili mradi tu dunia yao ipatikane utadhani wataishi milele! Hawana budi kutanabahi kuwa duniani tunapita tu na watakutana na Mola wao watake wasitake.
 
Back
Top Bottom