Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Maswali 11 kwa Baba Askofu Dallu

Kanisa hili limepitwa na wakati. Nashangaa npaka leo watu wanaenda kusali huko.
Shida ya mtu inakiaje ihusishe kanisa zima,kusema kanisa limepitwa na wakati ni kumkashifu KRISTO,ni sawa na kusema KRISTO kapitwa na wakati,
Tuache kuropoka,tuache kukurupuka,tuache chuki,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Hiyo ni silaha nyingine ya ujambazi wa kifalsafa--fallacy of association. Tunaongelea mimba za watoto wa kike unaleta habari ya ushoga. Kwani mashoga wanabeba mimba, kama ilivyo kwa watoto wa kike? Naona umesahau kwamba Yesu alikuwa ni shoga? Zingatia haya kabla ya kupayuka:
  1. A homosexual is a person having, either a homophilic disposition or a chromosome count different from the normal count of 46 chromosomes, where in the latter case, we have an intersexed person.
  2. Jesus had a female genotype and a male phenotype, where his/her cells contained only 23 chromosomes, of the type "XX." He was an intersexed person.
  3. So, Jesus was a homosexual.
  4. And so, Jesus followers are fans of a homosexual prophet!

Kwa hiyo, ukiamua kuongelea ushoga ujiandae kueleza kwa nini wewe unamfuasa nabii shoga, kama wewe sio shoga.

Got it?
Duuuuu hapa sasa unaenda mbali hebu jaribu kubaki kwenye hoja yako ya msingi ambayo umeiwasilisha vyema

Watakuja hapa wanao muamini Yesu ambaye ni..... Kama ulivyosema hapata kalika

Umetumia neno kali sana kumfananisha nalo Yesu
 
Duuuuu hapa sasa unaenda mbali hebu jaribu kubaki kwenye hoja yako ya msingi ambayo umeiwasilisha vyema. Watakuja hapa wanao muamini Yesu ambaye ni..... Kama ulivyosema hapata kalika.
Umetumia neno kali sana kumfananisha nalo Yesu
.
Neno hilo kali liko wapi?
Naona mouse yako iliokota text isiyo yangu.
Maneno yangu yote yako shwwari.
Hebu cheki tena uone....
 
MASWALI 11 KWA BABA ASKOFU DALLU

Kupitia gazeti la Kiongozi, ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, Mhashamu Damian Dallu, amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

"Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."

Ameelezwa kushangazwa na watu wanaoongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi walio shuleni. "Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?" Alihoji.

Hata hivyo, hakuna mwanaharakati anayeongelea "haki ya tendo la ndoa" kama Askofu Dallu anavyodai. Kinachoongelewa na wanaharakati ni "haki ya tendo la ngono." Kwa hiyo, Askofu Dallu hapa ametengeneza "hoja-mwanasesere" (straw man), kuishambulia, na kujiona amefanya uenjilishaji wa uhakika, kwa kutumia mbinu halali.

Askofu Dallu anaendelea kuhoji tena, " Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena [shuleni] na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?'”

Hapa, Askofu Dullu ameuliza maswali mawili kwa mpigo. Hebu tuyatenganishe maswali ya Askofu Dallu ili yaweze kujibika vizuri, baada ya kuonyesha ulaghai wa kifalsafa anaoutumia.

Askofu Dallu, hapa ameuliza maswali mawili yafuatayo:
  1. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya kwanza aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
  2. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya pili aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
Kuna ulaghai katika namna yake ya kuuliza maswali haya mawili kwa mpigo. Yaani, anatumia silaha mbili za kutekeleza ujambazi wa kifalsafa.

Kwanza anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of loaded question." Kwa ufupi, the fallacy of loaded question assumes a particular answer to another unasked question. Mfano wake ni huu, “Umekwisha acha kumpiga mkeo?” Swali hili linaulizwa kwa kuzingatia dhahania kwamba, tayari umekwisha jibu “ndiyo” kwa swali, “Je, huwa unampiga mkeo?”, swali ambalo, kwa kweli halijaulizwa kabisa.

Anafikiri kuwa, kwa vile wanaharakati wanatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la kwanza, basi wamekwishatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la pili. Sio kweli. Hilo ni swali ambalo bado halijajibiwa na yeyote. Njadala bado unaendelea.

Na pili anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of slippery slope."
Kwa ufupi, according to the slippery-slope fallacy, if we permit a certain action, then all actions of this type, even the most extreme ones, will soon be permissible. In other words, once we start down the slope or (to vary the metaphor) get a foot in the door, there is no holding back. We commit the slippery-slope fallacy when evidence does not support this predicted outcome.

Kwa kutumia ulaghai huu, Askofu Dallu anasema bila ushahidi usiokanushika, kwamba, kama mwanafunzi aliyezaa mara moja ataruhusiwa kurudi shuleni, basi atapata sababu ya kuzaa mtoto wa pili, automatically! Kweli?

Hayo yote tisa. Kumi ni hoja ya Askofu Dallu ifuatayo, na inayopaswa kutufikirisha sana kuhusu namna baadhi ya Maaskofu wanavyotekeleza majukumu yao:

Askofu Dallu amejenga hoja ifuatayo:
  1. Kama "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] yangekuwa sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," basi yangekuwa halali.
  2. Lakini, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] sio sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," badala yake, "ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."
  3. Kwa hiyo, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo]" ni haramu.
  4. Hivyo, "hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo" ni halali.
Kwa sababu ya hoja hii, ninayo maswali kadhaa kwa Baba Askofu Dallu.

Hapa Afrika, kabla ya ujio wa wageni, tulikuwa na mfumo wa elimu isiyo rasmi, familia zikiwa ni kitovu cha utekelezaji wake. Kabla ya kuja kwa wageni, mabinti walikuwa wanabeba mimba, kama ambavyo misamiati ya kimila kuhusu uwepo wa mimba kabla ya ndoa inavyoonyesha. Kule kwetu, tunaziita "ensinjo."
  1. Kama hivyo ndivyo, kabla ya ujio wa wageni, hawa mabinti zetu walikuwa wanatupwa jalalani baada ya kupata "ensinjo"?
  2. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu elimu inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kielimu?
  3. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu ujinsia inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kijinsia?
  4. Je, sheria asilia ya maadili inasema kuwa maslahi ya kijinsia yana kipaumbele kikubwa zaidi ya maslahi ya kielimu?
  5. Je, sheria asilia ya maadili inasema nini kuhusu uchumi, afya, mazingira, siasa, na sekta nyingine za maisha ya binadamu?
  6. Mbona baadhi ya Maaskofu, nawe ukiwemo, hamsikiki kuongelea maadili katika sekta hizi baki?
  7. Neno maadili linamaanisha "maadili ya ngono" pekee?
  8. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of loaded question?"
  9. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of lslippery slope?"
  10. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ngono?
  11. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ndoa?

Mwisho, niseme tu kwamba, baadhi ya waumini makini tungependa kuwasikia Maaskofu wetu mkijadili uhusiano uliopo kati ya sheria asilia ya maadili, kwa upande mmoja, na mdororo wa uchumi, uharibifu wa mazingira, wananchi kuwekwa rumande kwa siku 7 bila kupelekwa mahalamani, kwa upande mwingine. Hatuwasikii.

Ni kama vile ajenda kuu ya Kanisa ni kusimamia maadili ya gono.
Why?

Napendekeza kuwa Maaskofu Katoliki wajitafakari juu ya utume wao, wakiongozwa na Askofu Dallu.

Najua wanafanya kazi nzuri, lakini wakati mwingine wanaangukia pua...
Hivi bado unaamini kuna viongozi wa dini siku hizi?,kwasasa ni bora kuwategemea viongozi wa kijadi hawa wa dini ni wachumia tumbo. Kama hawa wakatoliki ndio majanga wanatenda tofauti na wanavyo hubiri, wako kibao wenye wake na watoto huku mitaani ili hali ni kunyume na amri za kanisa, wala siku hizi hawajadili au kukemea maswala ya ukiukwaji wa haki za viumbe vya mungu lakini macho yao ni kodo kwenye sadaka.
 
Tumsamehe Bure Baba Askofu Hajui Alitendalo Maana Ukitazama Vizuri Tunaye Baba Askofu Wa Escrow Wa Jimbo La Rulenge Ngara Tunangoja Kuona Hatua Atakazochukuliwa Hivi Punde
Ha ha ha maana nadhani kwenye maadili yao sidhani kama wanaruhusiwa kupokea mgao kama ule ....but hutasikia kuwa kafukuzwa upadri hata akimpa mtu mimba wala hutasikia kafukuzwa sana sana wataficha ficha wee
Kama nakumbuka 6yrs nyuma kuna.padri alikamatwa usiku mitaa ya chuo udsm akimlawiti mtoto wa kiume kwenye gari...yule mtoto akasema ni kawaida yule padri kumfanyia hvy..but kanisa iilipiga danadana weeee wakaipotezea
Ila kwa magu aah kila kitu twende
Sasa wewe kamuulize padri vipi ukandamizaji wa demokrasia na mtu kushikiliwa hadi siku 7 bila kupelekwa mahakamani kinyume na sheria za nchi...akikupa jibu lazina ukaee chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Mcdad, ni hivi:

Mosi, hakuna sheria ya Bunge inayomkataza mwanafunzi mwenye rika ya utu uzima kufanya ngono, hata kama yuko shule ya msingi. Mwanafunzi wa aina hiyo anabanwa na sheria za shule tu, sheria ambazo uhai wake unakomea kwenye uzio wa shule. Hata hivyo, kuna sheri ya Bunge inayomkataza mwanafunzi huyo kubeba mimba.

Pili, kuna sheria ya Bunge inayokataza mtoto yeyote kufanya/kufanyishwa tendo la ngono, kwani jambo hilo ni sawa na ubakazi. Mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18.

Tatu, sheria za maadili ya kidini zinakataza uasherati, lakini sheria za Bunge hazikatazi.

Nne, sheria za maadili ya kidini zinakataza uzinzi, sio kama kosa la jinai, bali kama kosa la kimadai.

Na tano, zingatia haya kuhusu maneno "tendo la ngono (sexual act)":
  1. Tendo la ngono ni tendo la kusisimua jenitalia kwa makusudi, kwa kutumia njia yoyote ile, kwa lengo la kutafuta mshindo (sexual act).
  2. Tendo la ngono linalofanyika kwa kuingiza uume uliodisa katika uke na kufikicha mpaka uume unapolegea linaitwa tendo la kutomba (vaginal-penile sexual act).
  3. Tendo la ndoa ni tendo la ngono kati ya mwamamke na mwanamume waliooana, yaani tendo la ngono kati yakati ya mume na mke (marital act/conjugal act).
  4. Tendo la ngono kati ya mwamamke na mwanamume ambapo, kila mmoja hajaolewa, na hao wawili hawajaoana, ni uasherati (fornication).
  5. Tendo la ngono kati ya mwamamke na mwanamume ambapo, hao wawili hawajaona, na angalau mmojawapo ameolewa na mtu mwingine, ni uzinzi (adultery).
  6. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa jenitalia ya kiume kwa kutumia mikono linaitwa punyeto (manual-penile sex au manual-penile masturbation)
  7. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa jenitalia ya kike kwa kutumia mikono linaitwa punyeto (manual-vaginal sex au manual-vaginal masturbation)
  8. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa jenitalia ya kiume kwa kutumia mdomo linaitwa felasio (oral-penile sex au felatio)
  9. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa jenitalia ya kike kwa kutumia mdomo linaitwa kanilingusi (cunnilingus)
  10. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa jenitalia ya kiume kwa kutumia mapaja au miguu linaitwa mapenzi ya mapaja (inter-crural sex)
  11. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa tezi-dume (male prostate gland) au tezi-jike (female prostate gland) kwa kutumia uume na kupitia kwenye rektamu linaitwa ulawiti (anal -penile sex)
  12. Tendo la ngono linalohusisha uchuaji wa tezi-dume (male prostate gland) au tezi-jike (female prostate gland) kwa kutumia kidole na kupitia kwenye rektamu linaitwa uchuaji wa tezi dume kwa kutumia kidole (manual prostate gland massage). Saluni nyingi za kuchua mwili zinatoa huduma hii--Tazama picha.
View attachment 548637

Nadhani taarifa hii itasaidia kidogo.
nashukuru ndugu kwa kunielewesha vizuri sana ndo mana nikataka kujua km kuna sheria ya shule sio ya nchi inayoruhusu mwanafunzi kujihusisha na ngono... Na vipi nasikia neno analotamka rais w nchi linatafsiriwa km ni sheria kamili lina ukweli swala hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nashukuru ndugu kwa kunielewesha vizuri sana ndo mana nikataka kujua km kuna sheria ya shule sio ya nchi inayoruhusu mwanafunzi kujihusisha na ngono... Na vipi nasikia neno analotamka rais w nchi linatafsiriwa km ni sheria kamili lina ukweli swala hilo?
.
Kwa ujumla, mfumo wa sheria una ngazi tano:
  1. Sheria asilia ya maadili
  2. Sheria za nchi/Bunge
  3. Matamko ya watawala.
Hivyo basi, vipaumbele vya utii viko hivi:
  1. Sheria asilia ya maadili ina nguvu kuliko Sheria za nchi
  2. Sheria za nchi/Bunge zina nguvu kuliko Matamko ya watawala
 
Wanaharakati wetu mara nyingi wanashangaza sana! Hivi sasa wanapambana mabinti waliopata mimba waruhusiwe kuendelea na masomo wakati huohuo wanapinga ndoa za utotoni! Sasa vipi kupata mimba nje ya ndoa iwe sawa na binti aonewe huruma na kuruhusiwa kurudi shule ilhali akiolewa iwe tabu?! Leo hii ukioa binti aliyemaliza shule ya msingi hivi karibuni na hakubahatika kuendelea na elimu ya sekondari jamii nzima inakugeukia lakini wale wanaowatandika hawa mabinti nje ya ndoa wanaonekana sawa tu! Wala huwezi kuwasikia wanaharakati wetu wakikemea vitendo vya ukahaba vinavyofanywa na mabinti wadogo kabisa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar. Kwao wao shida ni pale binti anapoolewa lakini anapozini hakuna shida. Tuache unafiki na huu ushetani.
 
Aisee...
Hivi hakuna mtu mwenye uwezo wa kujibu hoja kama hivi, ili amjibu Lissu.
For the first time naona mtu anajibu HOJA na anapinga kwa HOJA ndani ya JF.
Hakuna mihemko wala personal interests.
kula 5 mkuu.
 
Kazoba, muulize Dallu, katika Kanisa/dini/mafundisho, kuna dhana ya kusameeana? Tunafundishwa kusamehe, sasa yeye anatufundisha nini? Yesu anasema msamehe mwenzako “…hata saba mara sabini” Matayo 18:22.
“Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi” Waefese 4:31-32.

mapadri wangapi wanazini, wanalawiti, wanalewa na bado wanaendelea na utume chini ya msamaha wa Askofu?

Mwisho nimuulize Dallu, Ukatoliki ni utamaduni wa Mwafrika? Bukoba ukatoliki umeletwa lini? Walikuwa na utamaduni wa Ukatoliki kabla ya kuja hao wazungu na dini?
MWISHO NIKUSHUKURU KWA SOMO LA FALSAFA.
Asante Mtumishi wa Mungu Baba Askofu Kazoba kwa kutokua mnafiki, wengi tulitegemea Baraza la Maaskofu Katoliki kutoa tamko la kujitenga na msimamo binafsi wa Askofu Dallu
 
Kanisa hili limepitwa na wakati. Nashangaa npaka leo watu wanaenda kusali huko.
We unaenda wapi mkuu...na hilo unaloenda lita expire lini...halafu utaenda lipi tena....

germve himself
 
MASWALI 11 KUHUSU 'UJAMBAZI' WA BABA ASKOFU DALLU

Kupitia gazeti la Kiongozi, ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, Mhashamu Damian Dallu, amesema kuwa anaunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

"Hayo mambo siyo sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika, ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."

Ameelezwa kushangazwa na watu wanaoongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi walio shuleni. "Nawashangaa eti wanapigania haki ya tendo la ndoa, haki ya wapi hiyo?" Alihoji.

Hata hivyo, hakuna mwanaharakati anayeongelea "haki ya tendo la ndoa" miongoni mwa wanafunzi, kama Askofu Dallu anavyodai.

Kinachoongelewa na baadhi ya wanaharakati ni "haki ya kufanya tendo la ngono" waliyo nayo vijana ambao wamekwisha balehe, lakini bado ni matineja--vijana walio chini ya miaka 18.

Kwa hiyo, Askofu Dallu hapa ametengeneza "hoja-mwanasesere" (straw man), kuishambulia, na kujiona amefanya uenjilishaji wa uhakika, kwa kutumia mbinu halali.

Askofu Dallu anaendelea kuhoji tena, " Tutakuwa na shule za namna gani zinazoruhusu mwanafunzi kwenda kulea mtoto kisha arudi tena [shuleni] na akipata mimba nyingine aende tena nyumbani?'”

Hapa, Askofu Dullu ameuliza maswali mawili kwa mpigo. Hebu tuyatenganishe maswali ya Askofu Dallu ili yaweze kujibika vizuri, baada ya kuonyesha ulaghai wa kifalsafa anaoutumia.

Askofu Dallu, hapa ameuliza maswali mawili yafuatayo:
  1. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya kwanza aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
  2. Je, mwanafunzi akibeba mimba mara ya pili aruhusiwe tena kurudi shuleni baada ya kujifungua?
Katika namna yake ya kuuliza maswali haya mawili kwa mpigo, ametumia silaha za ujambazi wa kifalsafa kuwaburuza wasikilizaji wake. Yaani, anatumia silaha mbili za kutekeleza ujambazi wa kifalsafa--"the fallacy of loaded question" na "the fallacy of slippery slope."

Kwanza anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of loaded question." Kwa ufupi, the fallacy of loaded question assumes a particular answer to another unasked question. Mfano wake ni huu, “Umekwisha acha kumpiga mkeo?” Swali hili linaulizwa kwa kuzingatia dhahania kwamba, tayari umekwisha jibu “ndiyo” kwa swali, “Je, huwa unampiga mkeo?”, swali ambalo, kwa kweli halijaulizwa kabisa.

Anafikiri kuwa, kwa vile wanaharakati wanatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la kwanza, basi wamekwishatoa jawabu la "ndiyo" kwa swali la pili. Sio kweli. Hilo ni swali ambalo bado halijajibiwa na yeyote. Njadala bado unaendelea.

Na pili anatumia mbinu iitwayo "the fallacy of slippery slope."
Kwa ufupi, according to the slippery-slope fallacy, if we permit a certain action, then all actions of this type, even the most extreme ones, will soon be permissible. In other words, once we start down the slope or (to vary the metaphor) get a foot in the door, there is no holding back. We commit the slippery-slope fallacy when evidence does not support this predicted outcome.

Kwa kutumia ulaghai huu, Askofu Dallu anasema bila ushahidi usiokanushika, kwamba, kama mwanafunzi aliyezaa mara moja ataruhusiwa kurudi shuleni, basi atapata sababu ya kuzaa mtoto wa pili, automatically! Kweli?

Hayo yote tisa. Kumi ni hoja ya Askofu Dallu ifuatayo, na inayopaswa kutufikirisha sana kuhusu namna baadhi ya Maaskofu wanavyotekeleza majukumu yao:

Askofu Dallu amejenga hoja ifuatayo:
  1. Kama "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] yangekuwa sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," basi yangekuwa halali.
  2. Lakini, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo] sio sehemu ya utamaduni wetu wa Afrika," badala yake, "ni mambo ya kigeni yanayotaka kutuchafulia utamaduni wetu."
  3. Kwa hiyo, "hayo mambo [ya kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo]" ni haramu.
  4. Hivyo, "hatua ya Rais John Magufuli kutoruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo" ni halali.
Kimuundo, hoja hii iko sawa. Lakini kimaudhui ni hoja mbaya. Yaani, baadhi ya madokezo yake sio ya kweli hata kidogo.

Kwa sababu ya ubovu wa kimaudhui katika hoja hii, ninayo maswali kadhaa kwa Baba Askofu Dallu.

Hapa Afrika, kabla ya ujio wa wageni, tulikuwa na mfumo wa elimu isiyo rasmi, familia zikiwa ni kitovu cha utekelezaji wake. Kabla ya kuja kwa wageni, mabinti walikuwa wanabeba mimba, kama ambavyo misamiati ya kimila kuhusu uwepo wa mimba kabla ya ndoa inavyoonyesha. Kule kwetu, tunaziita "ensinjo."
  1. Kama hivyo ndivyo, kabla ya ujio wa wageni, hawa mabinti zetu walikuwa wanatupwa jalalani baada ya kupata "mimba ya utotoni" tena kabla ya ndoa?
  2. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu elimu inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kielimu?
  3. Je, sheria asilia ya maadili kuhusu ujinsia inayosimamiwa na kanisa inasema nini kuhusu jukumu la serikali kukuza na kuhami maslahi ya kijinsia?
  4. Je, sheria asilia ya maadili inasema kuwa maslahi ya kijinsia yana kipaumbele kikubwa zaidi ya maslahi ya kielimu?
  5. Je, sheria asilia ya maadili inasema nini kuhusu uchumi, afya, mazingira, siasa, na sekta nyingine za maisha ya binadamu?
  6. Mbona baadhi ya Maaskofu, nawe ukiwemo, hamsikiki kuongelea maadili katika sekta hizi baki?
  7. Neno maadili linamaanisha "maadili ya ngono" pekee?
  8. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of loaded question?"
  9. Ni halali kwa Askofu kufanya uenjilishaji kwa kutumia silaha ya ujambazi wa kifalsafa iitwayo "the fallacy of slippery slope?"
  10. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ngono?
  11. Na je, kwa mujibu wa sheria asilia ya maadili, ni katika umri gani binadamu anakuwa na haki ya kufanya tendo la ndoa?

Mwisho, niseme tu kwamba, baadhi ya waumini makini tungependa kuwasikia Maaskofu wetu mkijadili uhusiano uliopo kati ya sheria asilia ya maadili, kwa upande mmoja, na mdororo wa uchumi, uharibifu wa mazingira, wananchi kuwekwa rumande kwa siku 7 bila kupelekwa mahakamani, kwa upande mwingine. Hatuwasikii.

Ni kama vile ajenda kuu ya Kanisa ni kusimamia maadili ya gono.
Why?

Napendekeza kuwa Maaskofu Katoliki wajitafakari juu ya utume wao, wakiongozwa na Askofu Dallu.

Najua wanafanya kazi nzuri, lakini wakati mwingine wanaangukia pua...

RtbKazoba--Retired Bishop Kazoba
aache unafiki mbona maaskofu, walikula hela ya escrow lakini kanisa limewasamehe???

maaskofu na mapadri wazinzi. kanisa limewasamehe waendelee na huduma

cha ajabu ni kipi? kumsamehe Binti aliyedungwa mimba na mizee kama Dallu
 
Mbaya zaidi hizo shule zilijengwa kwa sadaka za waumini masikini ambao uwezo wao hauruhusu kusomesha watoto wao kwenye hizo shule walizozijenga wenyewe.
Ukweli in za ghali yaani wanasoma wenye nazo tuu...ila uache uongo seminary nyingi zimejengwa na wafadhili sio waamini

germve himself
 
Mimi ningemuuliza swali moja tu huyo Askofu, aje hapa atuambie ni kwanini Maelfu ya Mapadri wanaowapa mimba waumini wao Kanisa Katoliki haliwafukuzi lakini linaendelea kuwalea?
Liwafukuze waende wapi...mchungaji au mwanandoa yeyote akimpa mimba mtu ambae sio mchumba au mke wake anafukiziwa wapi

germve himself
 
Back
Top Bottom