Hata sielewi kilichowavutia ktk master plan ya Singapore kwasababu kwenye dunia ya kwanza hicho ni kitu cha kawaida yaani safari zote mnazochoma pesa za walala hoi kwa kutembea kundi kubwa mmejifunza master plan! Hivi hatuna architecture engineer tanzania? Nafikiri tatizo ni serikali isiyokuwa na mipango, ufisadi na uvivu wa kujituma, nchi inazalisha wasomi kibao kwenye kilimo Lakini watu wanakufa njaa hili nalo tunataka watu waje kutufundisha kulima! Ni kitu gani tunachoweza Kama watanzania? Gossip na ngonjera, tanzania itajengwa na sisi watanzania, Hakuna nchi duniani iliyojengwa na wageni.
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?
Umesema kupanga ni kuchagua. Tanzania ina zaidi ya wakaazi milioni 45. Zaidi ya milioni 20 kati ya hao wanaishi mijini, au pembezoni mwa miji na kati ya hao, zaidi ya 90% wanaishi maeneo ambayo hayana mipango miji wala makazi yao hayajapimwa.
Ni aibu kwa nchi yenye viongozi na wasomi kuwa wanaongelea Kigamboni miaka nenda rudi, eneo ambalo halitaishi zaidi ya watu laki tano. Hivi inagharimu bilioni ngapi kutengeza karamani kama hako ulikoweka kwenye picha?
Ramani ya Kigambini ipo, na hata kama haitajengwa leo, tunajua kuwa itajengwa tu, hata miaka 50 ijayo.
Mh Waziri nakuomba kwa heshima na taadhima, angalau kwa muda uliobaki nao kuongoza wizara hiyo, tutengenezee mipango miji ya miji hata 20 tu hapa Tanzania. Najua hii nchi ina zaidi ya 'miji' 100, lakini naomba angalau target miji 20. Hizo ramani ziwepo mahali fulani, ili hata baadae wakija viongozi wengine wakute kuna "kazi" ya kufanya. Hii nchi hadi sasa haina dira, na kila kiongozi akija anafanya anavyojisikia kwa sababu haina master plans.
Kwenye hizi nchi zilizoendelea, si ajabu ukakutana na 'pori', kumbe sio pori, ni mji mkubwa tu 'uliojengwa' miaka 40 iliyopita, ila ujenzi wake bado upo katika stage ya kwenye 'karatasi'. Hapo hata aje kiongozi 'nabii', hawezi kubadilisha; ama anajenga, au anapaacha palivyo.
Ingawa kwa sasa pengine hatuna hela za kujenga, lakini hata za kupanga na kuchora hatuna?!!!
WanaJF
Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.
Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.
Mama Tibaijuka
Umenena vyema. Katika hiyo miji ishirini Lindi isikosekane. Hata bahari kama ya kigamboni ipo
Mkuu niliona master plan ya CCM na vitega uchumi kibao huku wakiwa hawana mpango wa kuhamishia makao makuu ya Srikali Dodoma.Kikija chama kingine natumai wanaweza kuifanya kazi hii ndani ya miaka miwili tu kama nia ipo.Daha napata wakati mgumu kukujibu kwani hata mimi sijui hatima ya hii kitu kinaitwa makao makuu ya Nchii inamaana kikija chama kingine kinaweza kikaamua makao makuu yawe LINDI!
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?
Ili tuondokane na miji holela
lazima kuwepo na nyumba za bei nafuu
watu wawe discouraged kujenga wawe encouraged kununua au kukopeshwa cheap houses..
na serikali iache kupimia watu viwanja,badala yake ipimie makampuni maeneo yajenge nyumba kwa wingi...
Makes a lot of sense "real estate developers".
Itafanya hata "quality" na "standard" za nyumba na miundo mbinu ziwe bora.