Master Jay achukizwa na wanaopiga picha misibani

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mtayarishaji mkongwe wa muziki, Master Jay awavaa baadhi ya watu wenye tabia ya kwenda misibani na kuanza kupiga picha na ku-shoot videos kisha ku-post kwenye mitandao yao ya kijamii.

Kupitia andiko lake ameonesha kutofurahishwa na tabia hiyo kwa kuhoji; "Hivi mnaoenda kwenye misiba na kuanza kupiga picha na kushuti videos ili mposti kwenye mitandao mnajiona mko sawa??!! Kama kweli unawajali waliofiwa utaenda ukiwa na lengo moja tu, kuwafariji".

"Hayo mengine nadhani tuwaachie waandishi wa habari. let’s be respectful jamani, asanteni".

Screenshot_20240212-142341.jpg
 
Huyu nae amezidi gubu siku hizi. Kila siku anakosea na kulalamika yeye tu.
Lakini ujumbe wake una maana!

Watanzania wengi ni kama vile wana kichaa, kila anapokuwa anahakikisha watu wote wanajua alipo. Kwanini ukapige picha msibani? Kwani wewe ni muandishi wa habari? Tena kuna wengine hata wanataka kupiga picha mwili wa marehemu!

Watanzania waache viherehere na kila mtu abaki kwenye kazi yake. Kumiliki simu yenye camera haikufanyi uwe mtoa habari.

Mitandao ya kijamii imeharibu sana akili za watanzania. Kila mtu anataka kuwa mhabarishaji.
 
Master Jay bado hajapona stress za kugongewa mke wake, bado anaumwa akili. Kupiga picha msibani sio jambo baya tena siku hizi kuna mpaka kamati ya picha na videos kwenye misiba mpaka miziki inapigwa.
Lini iyo aligongewa? Na aligongewa na nani?

Funguka mkuu
 
Mtayarishaji mkongwe wa muziki, Master Jay awavaa baadhi ya watu wenye tabia ya kwenda misibani na kuanza kupiga picha na ku-shoot videos kisha ku-post kwenye mitandao yao ya kijamii.

Kupitia andiko lake ameonesha kutofurahishwa na tabia hiyo kwa kuhoji; "Hivi mnaoenda kwenye misiba na kuanza kupiga picha na kushuti videos ili mposti kwenye mitandao mnajiona mko sawa??!! Kama kweli unawajali waliofiwa utaenda ukiwa na lengo moja tu, kuwafariji".

"Hayo mengine nadhani tuwaachie waandishi wa habari. let’s be respectful jamani, asanteni".

Yani msiba wa Mzee Lowassa, kipenzi cha watu, alipo tupo, tusione hata picha Cadet ana hali gani?

Vipi kama wanafanya hivyo kwa idhini ya wafiwa kutengeneza memories za familia?

Kuna dada mmoja alifariki viunga vya Washington DC, akazikwa huko huko.

Ndugu zake baadhi walikuja kumzika kutoka Tanzania na Europe.

Zilipigwa picha mpaka video za kuungwa kwenye internet.

Kuna mdogo wake mmoja hapo Dar alishindwa kuja kuzika, lakini alisema kwamba ameshukuru sana kushirikishwa kwenye kuona mazishi live kupitia mtandao, na yeye amejiona kama kamzika dada yake ingawa alikuwa mbali.

Sasa Master Jay haoni kuwa haya ni matumizi ya teknolojia tu na kama waliofiwa wametoa idhini hakuna shida?
 
Master Jay mbona anajifanya kutoa ushauri tu kwa kila kitu? Yeye alivyomuacha mke wa ndoa na kutembea na msanii kwenye lebo yake kuna mtu alimsema? Alimdiss Kondea hajui kuimba BSS lakini akatoboa na kumzidi hadi pesa.
 
Master Jay bado hajapona stress za kugongewa mke wake, bado anaumwa akili. Kupiga picha msibani sio jambo baya tena siku hizi kuna mpaka kamati ya picha na videos kwenye misiba mpaka miziki inapigwa.
Wewe chawa wa WCB lazima umponde Master J coz alimpiga kwenye mshono Boss wenu,
So,kaa kwa kutulia,kumponda hapa hakuwezi kubadilisha alichokisema kuhusu Boss wenu.
 
Siku hizi amekuwa mzee wa ushauri. Asimalize ushauri wote mwingine aweke akiba kwa ajili ya BSS.
 
Master Jay bado hajapona stress za kugongewa mke wake, bado anaumwa akili. Kupiga picha msibani sio jambo baya tena siku hizi kuna mpaka kamati ya picha na videos kwenye misiba mpaka miziki inapigwa.
beat maker wako yule mchele mchele, anaingia studio akiwa na diaper anyonge beat kumshinda MJ kweli ? huku anavuja uharo ?
em fikiria tena
 
Back
Top Bottom