BASATA: Msijirekodi video zisizo na maadili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
1695069984631.png
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema hivi karibuni kumetokea wimbi la Wasanii kuwa na tabia ya kupiga picha, kujirekodi au ku-rekodiwa video zenye maudhui kinyume na maadili ya Kitanzania kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii kinyume na sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini.

“Baraza linatoa onyo kali kwa Wasanii wote kuacha tabia ya kujirekodi au ku-rekodiwa na kusambaza picha au video zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa na maadili ya Kitanzania”

“Baraza halitasita kuchukua hatua Kali ikiwemo kufutiwa leseni na kibali cha kujishughulisha na kazi ya sanaa kwa wote watakaoenda kinyume na tamko hili kwani itatafsiriwa kuwa ni uvunjaji wa sheria”
 
Nguvu kubwa mnaitumia kwa wasanii

Mfano wa kina Ney...ila wale wanaohamasisha ushg kwenye miziki

Yao mnawaachia

Ova
 
Hivi wale mabinti wanaotwa video model hawana baba na kaka? Inakuaje wanavaa nusu uchi, wanashikwashikwa kimahaba/kimapenzi na wanamuziki wa kiume/wacheza sinema wa kiume na picha hizo kutazamwa na ndugu zao wa kiume? Yaani unamtazama dada yako/binti yako/mama yako akitomaswa na kushikwashikwa mwili mzima bila aibu unajisikiaje?

Mara ananyonywa denda huku akirembua macho ya kimahaba, aibu gani hii? Wengine huwa hatuna uvumilivu huu ni lazima tutoe adhabu kwa binti na huyo jamaa yake aliyerokodi naye, hatujui kuwa hiyo ilikuwa kazi anayolipwa. Kazi gani hiyo ya kudhalilisha familia?
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema hivi karibuni kumetokea wimbi la Wasanii kuwa na tabia ya kupiga picha, kujirekodi au ku-rekodiwa video zenye maudhui kinyume na maadili ya Kitanzania kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii kinyume na sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini.

“Baraza linatoa onyo kali kwa Wasanii wote kuacha tabia ya kujirekodi au ku-rekodiwa na kusambaza picha au video zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa na maadili ya Kitanzania”

“Baraza halitasita kuchukua hatua Kali ikiwemo kufutiwa leseni na kibali cha kujishughulisha na kazi ya sanaa kwa wote watakaoenda kinyume na tamko hili kwani itatafsiriwa kuwa ni uvunjaji wa sheria”
"Msijirekodi." Inafikirisha sana. Kwahiyo kina zuchu na wenzie, ruksa kurekodiwa zisizo na maadili. Muhimu wasijirekodi wenyewe, awepo cameraman
 
Back
Top Bottom