Master J na Shaa kufunga ndoa

xShaa-na-Master-Jay.jpg.pagespeed.ic.VvnVGLGX_w.webp


Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Joseph Kimario ‘Master Jay’, ameweka wazi mpango wake wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Sara Kaisi ‘Shaa’.

Master J amesema Shaa atakuwa mke bora kwake kwani tayari ameshaishi naye kwa miaka 10 bila matatizo yoyote.

“Miaka 10 niliyoishi naye nimemwelewa vizuri, anastahili kabisa kuitwa mke wa Master J hapa nafanya taratibu za kumuoa ili tuishi maisha ya mke na mume,” Master J aliliambia gazeti la Mtanzania.

Mtayarishaji huyo wa muziki alisema kwamba anampenda Shaa kwa sababu ni msichana anayejielewa, licha ya kuwa msanii hasahau jamii inayomzunguka huku akijituma sana katika kazi zake zote kwa ujumla.
Amezini miaka 10!
 
Maimartha kachezea sana kichapo toka kwa P.diddy alipokua hai. Jamaa nakumbuka alifariki ghafla, alidondoka njiani na kufariki wala hakuugua.
Yeah nasikia mlio wa honi tu pale kitega uchumi Posta uliondoa maisha yake....
 
Kweli Shaa anajua 'siri ya penzi'.
Ila kiukweli huwa naona huruma sana kumuumiza mwanamke mwenzangu aliyeolewa.
Sijui anajisikiaje kuvunja ndoa ya watu.
Labda kama waliachana kabla,ila kama yeye ndiye aliyewaachanisha...My dear Shaa...hii dhambi itakutafuna milele!
 
h, post: 16542380, member: 207619"]Kweli Shaa anajua 'siri ya penzi'.
Ila kiukweli huwa naona huruma sana kumuumiza mwanamke mwenzangu aliyeolewa.
Sijui anajisikiaje kuvunja ndoa ya watu.
Labda kama waliachana kabla,ila kama yeye ndiye aliyewaachanisha...My dear Shaa...hii dhambi itakutafuna milele![/QUOTE]

Itakua alikua na mahusiano kabla ndoa haijavunjika sababu master J tangu aachane na mkewe miaka 10 bado haijafika
 
Maimartha kachezea sana kichapo toka kwa P.diddy alipokua hai. Jamaa nakumbuka alifariki ghafla, alidondoka njiani na kufariki wala hakuugua.
Mpenzi wa Maimartha si alikuaga yule mtangazaji shoga wa EATV anapenda kutangaza Bolingo. Anavaa hereni.
 
Back
Top Bottom