Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
> Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Klabu ya Barcelona akitokea Ajax Amsterdam amepost picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akionekana ndani mbuga hiyo
> Aidha, zipo taarifa pia za Mshambuliaji, Gonzalo Gerardo Higuaín anayeichezea Chelsea FC kuwepo nchini akitembelea vivutio mbalimbali
Ikiwa ni kipindi cha mapumziko ya ligi mbalimbali barani ulaya, kama ilivyokawaiada mastaa mbalimbali hutumia kipindi hicho kuambatana na familia zao kupumzika kwa kufanya utalii katika vivutio kadhaa vilivyopo ulimwenguni lengo likiwa na kuondoa uchovu wa mikimikiki ya msimu mzima.
Katika mapumziko ya msimu huu Tanzania tayari imeshapokea mastaa wawili waliokuja kutembelea vivutio mbalimbali ya utalii ikiwemo mbuga za wanyama. Wanandinga hao ni mchezaji wa timu ya Barcelona Frenkie Dejong na mpenzi wake Mikky Kiembeney itakumbukwa kuwa mchezaji huyo msimu ulioisha alijizolea umaarufu akiwa katika kilabu ya Ajax ambayo aliisaidia kufika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya " Uefa champions league". Mchezaji mwingine ni mshambuliaji wa timu ya Chelsea na raia wa Argentina Gonzalo Higuani
Kuna tetesi kuwa idadi kubwa ya wachezaji wanatarajiwa kumiminika Tanzania kwa ajili ya shughuli za utalii, itakumbukwa kwamba tangu Serikali ya awamu ya tano ichukue jitihada mahususi za kukuza utalii Nchini, Tanzania imekuwa inapokea watu mashuhuri mbalimbali kutoka tasnia tofauti wakiwemo viongozi wa kisiasa ( Obama), wanamziki (Usher Raymond), mastaa wa soka ( Beckham), mwanamitindo (Naomi Campbell).
Kongolle kwa Waziri kigwangalla kwa usimamizi na ubunifu katika wizara hiyo, ni mwelekeo mzuri ingawa jitihada zaidi zinahitajika kulifikia soko la Nchi za ulaya na Amerika bila kusahau soko la ndani ambapo Watanzania wengi pengine kutokana na hamasa ndogo wamekuwa hawana utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii.