Mastaa wa soka kutoka ulaya Frenkie De Jong, Gonzalo Higuani na Moussa Sissoko watembelea mbuga ya Serengeti

View attachment 1130501

> Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Klabu ya Barcelona akitokea Ajax Amsterdam amepost picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akionekana ndani mbuga hiyo

> Aidha, zipo taarifa pia za Mshambuliaji, Gonzalo Gerardo Higuaín anayeichezea Chelsea FC kuwepo nchini akitembelea vivutio mbalimbali

Ikiwa ni kipindi cha mapumziko ya ligi mbalimbali barani ulaya, kama ilivyokawaiada mastaa mbalimbali hutumia kipindi hicho kuambatana na familia zao kupumzika kwa kufanya utalii katika vivutio kadhaa vilivyopo ulimwenguni lengo likiwa na kuondoa uchovu wa mikimikiki ya msimu mzima.

Katika mapumziko ya msimu huu Tanzania tayari imeshapokea mastaa wawili waliokuja kutembelea vivutio mbalimbali ya utalii ikiwemo mbuga za wanyama. Wanandinga hao ni mchezaji wa timu ya Barcelona Frenkie Dejong na mpenzi wake Mikky Kiembeney itakumbukwa kuwa mchezaji huyo msimu ulioisha alijizolea umaarufu akiwa katika kilabu ya Ajax ambayo aliisaidia kufika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya " Uefa champions league". Mchezaji mwingine ni mshambuliaji wa timu ya Chelsea na raia wa Argentina Gonzalo Higuani

Kuna tetesi kuwa idadi kubwa ya wachezaji wanatarajiwa kumiminika Tanzania kwa ajili ya shughuli za utalii, itakumbukwa kwamba tangu Serikali ya awamu ya tano ichukue jitihada mahususi za kukuza utalii Nchini, Tanzania imekuwa inapokea watu mashuhuri mbalimbali kutoka tasnia tofauti wakiwemo viongozi wa kisiasa ( Obama), wanamziki (Usher Raymond), mastaa wa soka ( Beckham), mwanamitindo (Naomi Campbell).

Kongolle kwa Waziri kigwangalla kwa usimamizi na ubunifu katika wizara hiyo, ni mwelekeo mzuri ingawa jitihada zaidi zinahitajika kulifikia soko la Nchi za ulaya na Amerika bila kusahau soko la ndani ambapo Watanzania wengi pengine kutokana na hamasa ndogo wamekuwa hawana utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii.

View attachment 1130759View attachment 1130760View attachment 1130763I

View attachment 1130771
Cheki guu hilo la Dear Jong
 
Serengeti imetwaa tuzo ya mwaka 2019 kwa vivutio vya utalii africa...

Wageni takribani 300 kama sio 600 waliingia toka china kwa mkupuo... Na sasa tunaenda ktk high season kwa maana ndio msimu Wa utalii sasa

Watalii wanafulika msimu huu huko serengeti, ngorongoro, tarangire...
Mkuu umeisoma mada lakini? 😂
Maana hii ya kwako ni mada Mpya..
 
Back
Top Bottom