Masoud Kipanya: Mtazamo wa Kisiasa na Falsafa ya Maisha

willpower

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
404
2,271
Masoud Kipanya, wengi tulianza kumfahamu miaka ya mwishoni mwa 1990 na miaka ya mwanzoni mwa 2000.

Kadiri miaka ilivyokwenda ndipo Masoud Kipanya aliendelea kuwa maarufu na kujulikana katika mambo mbalimbali, vijana wengi kumbukumbu yao kwa Masoud Kipanya ni kipindi cha Chuchu ambacho alikifanya akiwa na Amina Chifupa na Kaka Bonda.

Baadaye akaja na KP Clothing Wear na miaka ya baadaye ikaja Maisha Plus.

Kwahiyo Masoud ni mtangazaji wa redio na TV, mtayarishaji wa vipindi, mchoraji na mfanyabiashara.

Leo nataka tutazame Masoud Kipanya wa wakati huu hasa kupitia Katuni zake za Kipanya.

Umaarufu wa katuni za kipanya umejengwa katika mambo mawili,
moja zinaakisi wakati uliopo, mara nyingi Masoud amekuwa akichora katuni zenye ujumbe wa mambo yanayotokea katika kipindi hicho.

Mbili, siasa katika katuni bila kuwepo kwa ujumbe wa wazi.

Umaarufu huu wa katuni za Masoud hauishii tu magazetini na kwenye mitandao bali hata katika viunga vya taaluma. Wanachuo kadhaa wamefanya tafiti na kuandika juu ya Katuni za Masoud Kipanya kwa mfano

Language and media: A case of lexical features of Masoud Kipanya’s cartoons in meaning presentation ya Lupenza, Harison Meshack


Nilipita Twitter kuona namna ambavyo watu huwa wanajitahidi kutaka kutafsiri katuni za Masoud Kipanya, bila kujali kama walikua sahihi ama la lakini hawa walinivutia kwa tafsiri zao za katuni.

Je wewe umewahi kuchukua muda kutaka kujua tafsiri katika katuni za Masoud Kipanya? View attachment 1942142View attachment 1942145View attachment 1942144View attachment 1942141View attachment 1942143View attachment 1942146View attachment 1942147View attachment 1942148
Screenshot_20210914-100419.jpg
 
Huyo kavua suruali hadharani kisha anawalaumu waliomuona akiwa uchi. Eti walio juu walikosea wasisemwe
 
Ispekta wa polisi mstaafu, Mahita aliwahi kusema hata kaa amsahau Masudi kipanya kwa jinsi alivyokuwa akimchora. Haswa wakati ule wa uchaguzi wa marudi jimbo la Temeke baada ya Kihiyo kujiuzulu baada ya Wakili lamwai kumbada sana mahakamani.
 
Back
Top Bottom