Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo ametembelea Kiwanda cha Magari kinachomilikiwa na Masoud Kipanya, aahidi kumsaidia mwekezaji huyu wa ndani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,804
Katibu mkuu wa CCM komredi Chongollo ametembelea Kiwanda cha kisasa cha kutengeneza magari kinachomilikiwa na mwekezaji wa kitanzania mh Masoud Kipanya.

Kiwanda cha Kipanya kinatengeneza magari ya kisasa yanatembea kwa kutumia nguvu ya umeme wa betri maalumu.

Komredi Chongollo amefurahishwa sana na ubunifu wa Kipanya na ameahidi kumsaidia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM wa kuinua vipaji na kuongeza ajira.

Kipanya ambaye ndiye Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo pekee ya magari ya kisasa nchini amemshukuru sana KM Chongollo na kusema anaamini ziara hiyo ina baraka za mwenyekiti wa CCM.

Source: ITV habari
 
TAARIFA KWA UMMA

KATIBU MKUU WA CCM NDG. DANIEL CHONGOLO ATEMBELEA NA KUKAGUA MAENDELEO YA KARAKANA YA MASOUD KIPANYA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo, ametoa siku saba kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kufika katika Karakana ya kutengeneza magari ya Alli Masoud maarufu Masoud Kipanya ili kufanya ukaguzi na kutoa vibali vinavyohitajika ili kuruhusu uzalishaji.

Akiwa katika karakana hiyo ameahidi ndani ya siku 14 atarudi akiwa na taasisi zote zinazohusika na udhibiti wa ubora, ili kuharakisha mchakato wa kiwanda hicho kuendelea.

Akizungumza leo tarehe 12 Aprili, 2022 Vingunguti jijini Dar es Salaam alipotembelea na kukagua maendeleo ya kiwanda hicho Katibu Mkuu ameeleza kuwa,

Ilani ya CCM kurasa za 151-4 imeahidi na imeendelea kuweka msukumo katika ubunifu, hivyo akiwa Mtendaji Mkuu wa Chama atahakikisha wanathamini mchango wa wazalishaji wa ndani kikiwemo kiwanda hicho, hivyo uwezeshaji wa kiwanda hiki ni muhimu ili kuongeza ajira kwa wananchi, kukuza teknolojia na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

Baada ya kupokea taarifa kupitia kwa Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Ndg Alli Masoud, Katibu Mkuu ameilekeza TBS kuhakikisha ndani ya siku saba wanakitembelea kiwanda hicho na kukapatia ithibati ili utaratubu mwingine uendelee,

“Naiagiza TBS ndani ya siku saba ije hapa ili kukamilisha taratibu za usajili na kukipatia kiwanda hati za ithibati, kwetu hili sio dogo kwa kuwa Ilani imeelekeza na kutoa msukumo katika kukuza ubunifu, nikuahidi nitakushika mkono na kufanya harambee ili wadau waunge mkono juhudi hizi ili kukujengea uwezo wa kifedha katika kukiimarisha kiwanda hiki".

Katibu Mkuu amemsihi Ndg. Masoud kuendeleza ubunifu huo na asivunjike moyo kwani Chama na Serikali vipo pamoja naye wakati wote.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa kiwanda hicho Ndg. Kipanya pamoja na mambo mengine, amesema wazo la uzalishaji wa kiwanda hicho ni mchakato ulioanza mwaka 2013, ambapo alifanya usajili na kuanza uzalishaji wa kwanza mwaka 2020.

USSR
 
Katibu mkuu wa CCM komredi Chongollo ametembelea Kiwanda cha kisasa cha kutengeneza magari kinachomilikiwa na mwekezaji wa kitanzania mh Masoud Kipanya.

Kiwanda cha Kipanya kinatengeneza magari ya kisasa yanatembea kwa kutumia nguvu ya umeme wa betri maalumu.

Komredi Chongollo amefurahishwa sana na ubunifu wa Kipanya na ameahidi kumsaidia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM wa kuinua vipaji na kuongeza ajira.

Kipanya ambaye ndiye Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo pekee ya magari ya kisasa nchini amemshukuru sana KM Chongollo na kusema anaamini ziara hiyo ina baraka za mwenyekiti wa CCM.

Source: ITV habari
😍👍👍
 
Kiwanda hakina jina, wala mahali kiwanda kilipo hapana jina, aina ya magari yanayotengenezwa haijulikani.
 
Katibu mkuu wa CCM komredi Chongollo ametembelea Kiwanda cha kisasa cha kutengeneza magari kinachomilikiwa na mwekezaji wa kitanzania mh Masoud Kipanya.

Kiwanda cha Kipanya kinatengeneza magari ya kisasa yanatembea kwa kutumia nguvu ya umeme wa betri maalumu.

Komredi Chongollo amefurahishwa sana na ubunifu wa Kipanya na ameahidi kumsaidia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM wa kuinua vipaji na kuongeza ajira.

Kipanya ambaye ndiye Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo pekee ya magari ya kisasa nchini amemshukuru sana KM Chongollo na kusema anaamini ziara hiyo ina baraka za mwenyekiti wa CCM.

Source: ITV habari
Acheni kukuza mambo kuliko uhalisia! Hili jambo linaweza kuwa sawa na ile propaganda ya Jafo ya viwanda mia moja kila mkoa!
 
Ilani ya CCM kurasa za 151-4 imeahidi na imeendelea kuweka msukumo katika ubunifu, hivyo akiwa Mtendaji Mkuu wa Chama atahakikisha wanathamini mchango wa wazalishaji wa ndani kikiwemo kiwanda hicho, hivyo uwezeshaji wa kiwanda hiki ni muhimu ili kuongeza ajira kwa wananchi, kukuza teknolojia na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.
2025 ajiandae kuimarisha chama
 
Back
Top Bottom