Masogange atimuliwa South Africa

Masogange atimuliwa South Africa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,213
Reaction score
18,455
masogange1.jpg
Agnes Gerald (Masogange).

HABARI ikufikie kuwa muuza nyago wa video za wasanii wa Bongo Fleva (video queen), Agness Gerald ‘Masogange' anadaiwa kutimuliwa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi' na sasa amekuwa akionekana Bongo akirandaranda mitaani.

TUJIUNGE JOHANNESBURG
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho Masogange ni rafiki yake aliyeko maeneo ya Midland jijini Johannesburg, Sauzi, staa huyo alitimuliwa na mwenye nyumba baada ya kodi ya pango kwisha na kutakiwa kulipa jambo ambalo lilimshinda.

Ilisemekana kwamba mwanaume aliyekuwa akimpa jeuri aliyetajwa kwa jina maarufu la Said 2010 ambaye ni mfanyabiashara, Mbongo aishie jijini humo alimtosa hivyo bidada akarejea Bongo kinyemela.

KUMBE CHANZO NI TUNDA
Habari nzito zilidai kwamba chanzo cha jamaa huyo ‘kumfungia vioo' Masogange ni baada ya kunasa kwenye penzi la muuza nyago mwingine wa video za wasanii wa Kibongo aliyetajwa kwa jina maarufu la Tunda.

Ilidaiwa kwamba zile mbwembwe za Masogange za kujitundika mitandaoni zilifika mwisho baada ya Said kuhamia kwa Tunda, mtoto mweupe mwenye sura ya mvuto ambaye anaonekana kwenye video za nyimbo za akina Matonya, TID ‘Mnyama', Christian Bella na wengine wengi.Ilizidi kunyetishwa kwamba, awali, Tunda alikuwa Bongo lakini jamaa huyo alimtumia tiketi ya ndege na sasa anatanua naye Bondeni kwa Madiba.

UGOMVI
Ubuyu uliendelea kumwagwa kwamba, hivi karibuni Masogange na Tunda waliingia kwenye ugomvi mkubwa huku wakitukanana mitandaoni bila kuanika sababu ya bifu lao.

"Kama ulikuwa unamfuatilia Masogange wiki mbili hivi zilizopita, utagundua kuna mtu alikuwa anagombana naye. Si mwingine ni huyo Tunda ambaye amemdatisha jamaa hadi akasahau kama kuna Masogange.

"Wewe fikiria, Masogange siyo mtu wa kutua Bongo kimyakimya bila kutupia picha kwenye Instagram ili kuwarusha roho wenzake. Siyo kwamba hawezi, sasa hivi yupo juu ya mawe ndiyo maana anajificha," kilisema chanzo hicho.

SUALA LA URAIA
Chanzo hicho kilipotonywa kuwa mwaka jana Masogange alitamba kuukwaa uraia wa Sauzi na kuukana wa Bongo kilisema:"Mimi nimeishi hapa South Africa (Sauzi) zaidi ya miaka mitano. Nilishaomba uraia miaka kibao sijapata hadi leo, huyo Masogange ni nani wampe uraia kwa siku mbili? Hizo fiksi tu. Kama aliomba sawa lakini hawezi kupewa uraia kirahisirahisi. Kuna process (taratibu) ndefu hadi mtu apate uraia."

MASOGANGE ATAKWENDA TENA SAUZI?
Chanzo hicho kilizidi kudadavua kuwa siyo kwamba Masogange hatakwenda tena Sauzi kwa sababu ana watu na marafiki kibao nchini humo lakini kwa sasa hana maskani ya kufikia baada ya kutimuliwa."Anaweza kwenda any time (muda wowote) lakini mpaka awe na uhakika na pa kufikia," kiliongeza chanzo hicho.

Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Masogange, alipopatikana alisomewa kila kitu ‘eituzedi' ambapo aliomba chondechonde isiandikwe kwamba ametimuliwa bali yupo Bongo kwa ajili ya mapumziko.

"Jamani si kweli, waambie wahariri nipo huku (Bongo) kwa ajili ya mapumziko tu," alisema Masogange kwa kifupi.

Chanzo: GPL
 
Maskini anatia huruma, mbwe mbwe zote zile unaambulia kurudi bongo na iphone 6 na vibikini vyake, kumbe ata uraia huna nfyuuu umalaya tu ukome, angekutoa jicho kwanz ushukur mungu kufukuzwa ukiwa hai
 
Kweli warumi sasa nimeona umuhimu wa ushauri uliompa huyu Agnes juzi kati hapa.Ona sasa anaaibika (kama ni kweli maana Shigongo haaminiki aisee)
 
Last edited by a moderator:
Ndio mana mnaabiwa mwende shule mkasome,sijui nani aliwambia K ndio mtaji,sasa hiyooooooo umebaki nayo hashue na majisifu umebakia kujifungia ndani kama mwari wa zamani,unaanza kutafuta mabwana wa shoga zako sasa...
 
Kweli warumi sasa nimeona umuhimu wa ushauri uliompa huyu Agnes juzi kati hapa.Ona sasa anaaibika (kama ni kweli maana Shigongo haaminiki aisee)

Yupo bongo ,nasikia ni kweli katimuliwa south, sasa ivi anahangaika kutafuta chumba mbezi beach, ila nilimpa ushauri hakuufanyia kazi, angesoma ata mambo cosmetics kama zari, ona sasa anarud bongo kichwan patupu, lugha yenyewe hajui basi kazi tupu, yan bor unyimwe tako upewe akili, kapata bahat kapangiwa nyumba nzuri yeye anawaza kufanya umalaya
 
Last edited by a moderator:
Zero kabisa.Yeye anadhani atabaki mzuri milele? Ona sasa bado msichana lakini kapigwa kibuti kachakuliwa mwenzie.Akianza kuchoka je?

Imebaki historia tu, yeye alishindwa ata kufanya biashara uko akalipa kodi mpaka anafukuzwa? Mmh aibu sana huy mrembo akili hana, kapata bahati kachezea
 
Rummy kala 0713 mpaka kajichokea sasa hivi ana mtoto chocolate CBC warumi Madame B

Mmh!! Yule rummy na yeye kiboko, kajitu kafupi ila kanafumua watoto wa watu balaa, na sijui kama mzima yule.

Huyo demu wake ndo anamuita kiboko yake? Mzuri kiasi ila anaonekana mkubwa
 
Last edited by a moderator:
Imebaki historia tu, yeye alishindwa ata kufanya biashara uko akalipa kodi mpaka anafukuzwa? Mmh aibu sana huy mrembo akili hana, kapata bahati kachezea

Hahahaaa,itabidi sasa tubadili usemi tuseme kua "usililie uzuri lilia akili" maana unaweza ukapata bahati ukashindwa kuitumia lakini akili utaitumia katika kutafuta pesa.
 
Huyu dada niliishi nae jiran Sinza,mama yake akiwa housegirl wa Jamaa flani mwenye nazo kidogo,hana mishe ya mcng zaid ya kuuza "asali yake",..
 
Yupo bongo ,nasikia ni kweli katimuliwa south, sasa ivi anahangaika kutafuta chumba mbezi beach, ila nilimpa ushauri hakuufanyia kazi, angesoma ata mambo cosmetics kama zari, ona sasa anarud bongo kichwan patupu, lugha yenyewe hajui basi kazi tupu, yan bor unyimwe tako upewe akili, kapata bahat kapangiwa nyumba nzuri yeye anawaza kufanya umalaya

Atajua mwenyewe ngoja ayaone sasa.Au aende kwa shoga yake chagga bibi wakajiuze wote maana hua naona tambo zao huko insta.
 
Hahahaaa,itabidi sasa tubadili usemi tuseme kua "usililie uzuri lilia akili" maana unaweza ukapata bahati ukashindwa kuitumia lakini akili utaitumia katika kutafuta pesa.

Mmmh kashindwa ata kusomea course fupi jaman ata ya hotel, ye kutwa kupost ..... * wake insta, yani kweli siku izi mlilie akili sio bahat, maana wengine wana bahati ila akili hawana
 
Back
Top Bottom