Maslahi duni katika sekta nyingi ni chanzo kikubwa cha uchawa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,641
46,289
Pamoja na malalamiko makubwa sana kuhusu mfumo mpya wa maisha ulioshika kasi siku za hivi karibuni ni vyema kufahamu pia chanzo kikubwa cha mambo haya.

Ukweli ni kwamba katika nchi yetu maslahi sio mazuri katika sekta au tasnia nyingi. Na ushahidi ni mwingi sana, mfano angalia watu maarufu na wenye majina makubwa wanapopatwa na mogonjwa makubwa wanavyoangaika kuomba michango ya kutibiwa.

Unaweza kuona Mwanamuziki, Mchezaji mpira, muigiza filamu na hata wanasiasa maarufu sana na wanaonekana wanaojiweza, lakini acha waugue moyo, figo au ugonjwa mwingine tu mkubwa hata kwa kipindi kifupi sana. Hapo ndipo utaona mahangaiko makubwa ya uhitaji fedha.

Udini wa maslahi ni kwa karibia sekta zote, iwe vyombo vya habari, watumishi wa serikali na hata wengi katika sekta binafsi. Kuna watumishi maisha yao yote wanaishi kwa vimikopo vya matumizi ya kawaida ya kujenga, kupeleka watoto shule, kununua gari, mafuta n.k

Hali inasababisha hofu kubwa kwa maisha ya mbeleni na kupelekea watu kujiegeuza chawa tu ilimradi maisha yaende vizuri au kwa matumaini hayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom