Uchawa ni ajira kwa sasa inayodharirisha watu kwa kulipwa

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,035
Hakina mambo yamebadilika. Kutokana na kutokuwa na Ajira kundi kubwa la vijana hasa Wasomi wamewaza sana na kufikia Uamuzi kuwa wawe machawa.

Uchawa ni hali ya kujitoa ufahamu Aibu Haya Hasira Upofu na Ukiziwi. Ukiwa na Sifa hizo basi UCHAWA utauweza.

Uchawa pia una watu wenye Umri mkubwa waliokwama kimaisha nao Wameamua kuwa MACHAWA hivyo UCHAWA hauna umri rasmi. Hizo ndio Sifa za uchawa.

Kutokana na Ukosefu wa Ajira Serikalini Watu wengi Wameamua kuwa MACHAWA wa watu Mbalimbali wenye Uwezo wao wa kifedha au nadaraka ili mradi wawe na uwezo wa kuwalipa hao machawa. Bahati nzuri hao wenye Fedha au Madaraka ili Mambo yao Yasikike na yaende vizuri Wanataka yatangazwe hivyo huwatumia machawa kuyatangaza vizuri hata kama ni mabaya.

Pia kwa wale wanaotafuta madaraka au vyeo huwatumia machawa kumchafua Mtu ili apoteze Madaraka yake na nafasi hiyo aichukue yeye.

Machawa wamekuwa wakilipwa fedha nyingi kufanya kazi hizo nao wao hujiita Wameajiriwa. Mfano mzuri wa Kazi za machawa ni kama tulivyoshuhudia Kiongozi mmoja mkubwa ndani ya Chama alivyodharirishwa sana na machawa kupitia Mitandao na kupelekea kuandika Barua ya kujiuzulu nafasi yake.

Silaha kubwa wanayotumia machawa katika kutimiza majukumu yao ya ni mitandao ya kijamii, redio na TV.

MACHAWA pia Wamekuwa Wakiwalenga watu mashuhuri na maarufu.
 
Mada hii na aione Lucas Mwashambwa
Yaani ningeweza kumfahamu, ningempa mawazo ya kuweza kujiiwezesha mwenyewe na akalinda dignity yake, maana kutwa humu na mada za aina ile ile ni upumbavu wa hali ya juu, ni vema akaelewa kuwa always kuna two sides of story, yeye kakaazana na moja tu
 
Huyu ni mjane kafiwa na mume wake anatafuta namna ya kuishi
 
R na L bado ni tatizo kwako halafu mbona hata paragraph hamna?

Inatia kinyaa kusoma
 
Hakina mambo yamebadilika. Kutokana na kutokuwa na Ajira kundi kubwa la vijana hasa Wasomi wamewaza sana na kufikia Uamuzi kuwa wawe machawa.

Uchawa ni hali ya kujitoa ufahamu Aibu Haya Hasira Upofu na Ukiziwi. Ukiwa na Sifa hizo basi UCHAWA utauweza.

Uchawa pia una watu wenye Umri mkubwa waliokwama kimaisha nao Wameamua kuwa MACHAWA hivyo UCHAWA hauna umri rasmi. Hizo ndio Sifa za uchawa.

Kutokana na Ukosefu wa Ajira Serikalini Watu wengi Wameamua kuwa MACHAWA wa watu Mbalimbali wenye Uwezo wao wa kifedha au nadaraka ili mradi wawe na uwezo wa kuwalipa hao machawa. Bahati nzuri hao wenye Fedha au Madaraka ili Mambo yao Yasikike na yaende vizuri Wanataka yatangazwe hivyo huwatumia machawa kuyatangaza vizuri hata kama ni mabaya.

Pia kwa wale wanaotafuta madaraka au vyeo huwatumia machawa kumchafua Mtu ili apoteze Madaraka yake na nafasi hiyo aichukue yeye.

Machawa wamekuwa wakilipwa fedha nyingi kufanya kazi hizo nao wao hujiita Wameajiriwa. Mfano mzuri wa Kazi za machawa ni kama tulivyoshuhudia Kiongozi mmoja mkubwa ndani ya Chama alivyodharirishwa sana na machawa kupitia Mitandao na kupelekea kuandika Barua ya kujiuzulu nafasi yake.

Silaha kubwa wanayotumia machawa katika kutimiza majukumu yao ya ni mitandao ya kijamii, redio na TV.

MACHAWA pia Wamekuwa Wakiwalenga watu mashuhuri na maarufu.
Tena mizee ndiyo michawa ya waziwazi kuliko hata hawa vijana wenye njaa na tamaa. Unasemaje kuhusu wale waliokuwa wakimuita Rais, mh. Mungu? Je, hawakuwa na ajira? Wenye ajira na wateule ndiyo machawa wakubwa, Kuna wakati wanakubaliana na mambo na kuyabariki lakini mioyoni mwao dhamira zinawasuta.

Uchawa umetengenezwa na mfumo wa serikali ya CCM hasa kuanzia kipindi cha Mwendazake. Ajira na teuzi ktk sekta ya umma vimefanywa mali ya CCM.
 
Inabidi Kuwe na Shule ya Uchawa nchini, maana inaonekana kazi hiyo inalipa sana.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom