Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,539
Salaam,
Nimemuonea huruma dada yangu Christina Mughway Lissu na kupata msukumo wa kumshauri jambo!
'Kwa kuwa sina ushahidi wowote kwamba alikuwa anazuga; Binafsi namchukulia kama mtu aliekuwa na nia njema huku akisukumwa na uzalendo kutoka ndani ya nafsi yake!.'
Ni leo mchana wakati akichangia Bajeti ya wizara ya fedha: Dada yetu mpendwa ndugu Christiana Maghway Lissu alimtaka waziri wa fedha kufafanua kwamba ni kwa sababu gani serikali inanunua magari ya/kwa bei ya juu sana 'Mashangingi?' na wakati bajeti ya nchi ni finyu.Dada yetu huyu aliongeza kwa kusema thamani ya magari hayo ni sawa na dispensary!.
Dada Christina Lissu; Haukuwahi kupata taarifa kwamba suala la kupinga ununuzi wa mashangingi kwa kodi za wananchi badala ya kununua magari ya bei ya kati lilikuwa ni suala la muda mrefu, au umesahau tu?Haukupata habari kwamba hoja ilitolewa kwamba tatizo ilikuwa ni serikali ya ccm na wabunge wake na hivyo ni wapinzani ambao walitakiwa kuhakikisha wanasukumu hoja hiyo?, au pengine umesahau?Haukusikia kwamba wapinzani walikubaliana kugomea magari hayo ili kushinikiza hoja hiyo, au pengine umesahau tu dada yangu mpendwa.
Dada yangu Lissu Christina: Historia inaonesha kwamba baada ya kambi ya upinzani kukubaliana kugomea magari hayo ili kuishinikiza serikali kutoendelea kuyanunua na hivyo kutumia kodi vibaya, Kiongozi wa kambi aliliacha gari na baadae kulichukua kimiani,Haukupata kuisikia historia hiyo dada christina?Kama hukuipata au umesahau; ningependa kukumbusha ili twende pamoja Dada Christina!.Unadhani ni nini ilikuwa mantiki na msingi wa jambo hilo? je! unaamini bado kwamba msingi wa tatizo hilo uko ndani ya CCM tena CCM peke yake kama chama? Tafadhali dada christina! hebu tutafakari pamoja.
Dada Christina, kama utakuwa na kumbukumbu kidogo,utakumbuka kwamba suala hili la kupinga ununuzi wa mashangingi kwa bei ya juu, lilikuwa linaenda pamoja na kupinga posho za "kupasha viti moto".Sijui kama unakumbuka kwamba waliojaribu kutekeleza hayo kwa vitendo waliitwa wasaliti na kushughulikiwa
vibaya!
Hivi dada yangu unaweza kukumbuka hata kama ni kwa mbaali, kwamba ni kina nani waliokuwa wamekwamisha issue hii? na ushawahi kufikiri katika hali ya utulivu kwamba waliojaribu kuyasimamia hayo seriosly wako katika hali gani leo kisiasa? je! nawe ungependa kuelekea huko?
Dada Cristina! Binafsi nimejifunza kutokana na historia.Kuna baadhi ya mambo katika siasa, hata uwe na nia nzuri kiasi gani, hauwezi kufanikisha mwenyewe kama wenzako hawaungi mkono kile unachokitetea kwa dhati yake naili upate watu wanaofikiri katika utaratibu fulani, unatakiwa kuanzia mbali.Mambo ya namna hiyo yanahitaji mpango madhubuti kweli kweli ili kuweza kufanikiwa zaidi ya kuongea simple tu bungeni mbele ya watu wanaoona hoja yako kama kituko moyoni wakipiga makofi mezani.
Dada lissu Christina; Suala la posho zisizo za lazima, Mashangingi na mambo mengine kama hayo, ni suala linalowachukiza wananchi wengi ila kwa bahati mbaya suala hilo ni pana zaidi ya CCM na serikali hii unayoiona.Hivi wakati unatoa hoja yako, uliangalia ni nani yu nyuma yako,kushoto kwako na kulia kwako?.Nikuulize tu kaswali ka kizushi; Hivi mfano waziri wakati anajibu akaamua kusema "Sasa seerikali itanunua Landrover tu, hakuna mchezo hapa!" hivi ni kina nani watakaopitisha hilo? Tehe! nakutania tu dada yangu Christina! lakini hivi unadhani tatizo ni waziri?
Dada Cristina, nakushauri; kama mambo haya yanakukera kweli kwa dhati ya moyo wako kama ambavyo nimeamini, basi mambo haya yanataka mkakati zaidi ya kuchangia bungeni.Tutafakari pamoja.Je! ni mkakati wa siri au wa wazi! tehe! tehe! tehe!. Any way ambacho nina uhakika nacho ni kwamba unahitajika mkakati.