Maskini Dada Christina Maghway Lissu! Inafaa tusaidiane

Maskini Dada Christina Maghway Lissu! Inafaa tusaidiane

mkuu silalamiki na huwa sikati tamaa.Wakati wote mimi ni mtu wa kujifunza na kutafuta altenatives.Kama mtu una uhakika kwamba hauwezi kufanikiwa tena kwenye jambo fulani kwa kutumia njia fulani katika mazingira fulani, nibora ukakaa chini kwanza kutafakari na kutafuta altenative. Ni vizuri kufanya hivyo kwa kushauriana na wenzako unaodhani kwamba mna mitizamo inayoelekea kufanana.

Katika wabunge wote umeona huyu mwenye jina la Lissu ndio wa kukumbusha na kukosoa kwa mbwembe.
 
Mie ndio maana nasema uwezo wenu ni mdogo sana. Kwani kama yeye anatumia gari ya aina yeyote inahusiana nini na magari ya umma? Hapa kazungumzia magari ya Umma na gharama za kuyaendesha.
Sisi kitu binafsi hakituhusu. Hata kwa mfano Mh Ndesamburo aamue kuwa anakuja asubuhi na helcopter yake gharama hizo zitaihusu nini serekali?
Yeye kapigania maslahi ya Umma.


Sent from my iPad using JamiiForums
Wewe umeongea poin ya msingi sana.Hoja ya msingi si mtu anatumia gari gani.Suala ni gari hilo limenunuliwa na nani na kwa bei gani.Kwa mfano mtu anaweza kutembelea gari ya 8,00mil ila kanunua na hela yake, hapo hamna shida kabisa, au chama kikanunua gari ya mil400, lakini hela hiyo ikawa imetolewa na wanachama waliojitolea kwa maagizo ya kununua gari kama hilo, hiyo haina shida kabisa mkuu.
 
Kifungu hicho cha tumekilazimisha kinaafikiwa!! kina Bethlehem naLusinde ndiyoooooo, hoja imepita, katibuuuu.........
 
Katika wabunge wote umeona huyu mwenye jina la Lissu ndio wa kukumbusha na kukosoa kwa mbwembe.
kama kuna wengine, basi washauri na wewe maana jukwaa hili ni huru nawe ni mtu huru.Au kwani ni lazima nishauri wote! mimi nimempenda Christina! sasa sijui shida iko wapi.
 
ACT Tanzania tukiingia madarakani hatutotumia magari bali tutatumia bajaj kwa rais na pikipiki ya Boxer 150 kwa waziri mkuu, tutanunua na kalandinga kwa ajili ya wabunge wakiwa wanaelekea vikaoni Dodoma, Asanteni

Imetolewa na
ACT-Tanzania Uenezi
Dotto C. Rangimoto
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nilimshangaa sana huyu Christina Lissu. Sijui na yeye anatumia gari gani. Ningemuona yupo sahihi kama angekuwa anatumia magari aina ya Starlet, Vitz au Ist
Lizaboni unamshangaa nini Christina wakati bado magari ya bei mbaya yananunuliwa eti kwa mgongo wa vibali maalum!!! Tunaposhana na STL za nguvu barabarani zinapishana kwa mbwembwe!!
 
Sasa haudhani kwamba pengine utaahira wangu ndio unanifanya niwe hivi hivyo sihitaji kulaumiwa? au unasema je katika hili! maana sidhani kama taahira anaweza kuwa mnafiki kama unavyosema kwa kuwa anakuwa hana fikra sahihi katika hali ya kawaida!
 
Sasa haudhani kwamba pengine utaahira wangu ndio unanifanya niwe hivi hivyo sihitaji kulaumiwa? au unasema je katika hili! maana sidhani kama taahira anaweza kuwa mnafiki kama unavyosema kwa kuwa anakuwa hana fikra sahihi katika hali ya kawaida!

Njaa zinakusumbua
 
Mkuu Betlehem unamshangaa nini dada Christina? Unataka kuniambia kuwa ni kweli serikali hainunui magari ya bei mbayaa? Magari yananunuliwa kwa kupitia mgongo wa kuomba kibali!!!! Tehe Tehe!! Sema ni utaratibu tu umebadilika katika kuyanunua. Landcruiser moja PRADO new model ni shilingi ngapi? Hizo zinatosha kujenga shule ya msingi au Dispensary na vifaa na madawa. Christina yuko sahihi. Kwa nini wasinunue Vitara? Lukuvi alitetea bajeti ya sh. 180,000,000 kununua RAV 4 moja! Mshangao!!!! Zinatosha kujenga Dispensari angalao kwa 90%.
 
Hivi huyu christina aliwahi kuolewa au ana mume now?
mbona anatu ia jina la baba still?
watoto?
ana mtu now? bf?

Yuko single mkuu changamkia the Boss!!! Aliolewa na jamaa mmoja Mhaya kama sikosei ndoa kabisa. Bahati mbaya alifariki miaka ile ya 1990s. Alimwachia mtoto mmoja nafikiri atakuwa ni binti mkubwa sasa wa chuo kama alifaulu vizuri. Alikuwa ni dada aliyetulia sana na mtu wa maombi. Alisoma na dada yangu Kilakala Secondary na walikuwa Chuo wote. She is intelligent as well. Like brother like sister. Na alijikita tu katika kumlea mtoto wake na hakutaka kuolewa tena. I hope bado ni rafiki wa dada yangu maana kila mtu yuko na familia yake sasa.
 
Mkuu Betlehem unamshangaa nini dada Christina? Unataka kuniambia kuwa ni kweli serikali hainunui magari ya bei mbayaa? Magari yananunuliwa kwa kupitia mgongo wa kuomba kibali!!!! Tehe Tehe!! Sema ni utaratibu tu umebadilika katika kuyanunua. Landcruiser moja PRADO new model ni shilingi ngapi? Hizo zinatosha kujenga shule ya msingi au Dispensary na vifaa na madawa. Christina yuko sahihi. Kwa nini wasinunue Vitara? Lukuvi alitetea bajeti ya sh. 180,000,000 kununua RAV 4 moja! Mshangao!!!! Zinatosha kujenga Dispensari angalao kwa 90%.
Ndugu yangu Zogwale , labda kama tu hujanielewa.Mimi sijamshangaa Dada Christina hata Kidogo.Nakubaliana kabisa na hoja yake.Soma vizuri tu utanielewa.Ninachosema ni kwamba hayo mambo yana force behind inayosukuma hata hayo magari yakaendelea kununuliwa.Ni zaidi ya tunavyo zungumza kirahisi rahisi tu.Na ndio maana nachelea kumhurumia dada yangu (sio kumshangaa!) kwa sababu na hisi hajui kwa undani force zilizopo nyuma ya kile anachokipinga, ndio maana namuuliza kama ameitafakari vizuri historia?
 
Last edited by a moderator:
Hawajitambui hao chadema naona huyo Dada anaugua ugonjwa kama wa kaka yake
 
Salaam,
Nimemuonea huruma dada yangu Christina Mughway Lissu na kupata msukumo wa kumshauri jambo!
'Kwa kuwa sina ushahidi wowote kwamba alikuwa anazuga; Binafsi namchukulia kama mtu aliekuwa na nia njema huku akisukumwa na uzalendo kutoka ndani ya nafsi yake!.'


Ni leo mchana wakati akichangia Bajeti ya wizara ya fedha: Dada yetu mpendwa ndugu Christiana Maghway Lissu alimtaka waziri wa fedha kufafanua kwamba ni kwa sababu gani serikali inanunua magari ya/kwa bei ya juu sana 'Mashangingi?' na wakati bajeti ya nchi ni finyu.Dada yetu huyu aliongeza kwa kusema thamani ya magari hayo ni sawa na dispensary!.

Dada Christina Lissu; Haukuwahi kupata taarifa kwamba suala la kupinga ununuzi wa mashangingi kwa kodi za wananchi badala ya kununua magari ya bei ya kati lilikuwa ni suala la muda mrefu, au umesahau tu?Haukupata habari kwamba hoja ilitolewa kwamba tatizo ilikuwa ni serikali ya ccm na wabunge wake na hivyo ni wapinzani ambao walitakiwa kuhakikisha wanasukumu hoja hiyo?, au pengine umesahau?Haukusikia kwamba wapinzani walikubaliana kugomea magari hayo ili kushinikiza hoja hiyo, au pengine umesahau tu dada yangu mpendwa.

Dada yangu Lissu Christina: Historia inaonesha kwamba baada ya kambi ya upinzani kukubaliana kugomea magari hayo ili kuishinikiza serikali kutoendelea kuyanunua na hivyo kutumia kodi vibaya, Kiongozi wa kambi aliliacha gari na baadae kulichukua kimiani,Haukupata kuisikia historia hiyo dada christina?Kama hukuipata au umesahau; ningependa kukumbusha ili twende pamoja Dada Christina!.Unadhani ni nini ilikuwa mantiki na msingi wa jambo hilo? je! unaamini bado kwamba msingi wa tatizo hilo uko ndani ya CCM tena CCM peke yake kama chama? Tafadhali dada christina! hebu tutafakari pamoja.

Dada Christina, kama utakuwa na kumbukumbu kidogo,utakumbuka kwamba suala hili la kupinga ununuzi wa mashangingi kwa bei ya juu, lilikuwa linaenda pamoja na kupinga posho za "kupasha viti moto".Sijui kama unakumbuka kwamba waliojaribu kutekeleza hayo kwa vitendo waliitwa wasaliti na kushughulikiwa
vibaya!
Hivi dada yangu unaweza kukumbuka hata kama ni kwa mbaali, kwamba ni kina nani waliokuwa wamekwamisha issue hii? na ushawahi kufikiri katika hali ya utulivu kwamba waliojaribu kuyasimamia hayo seriosly wako katika hali gani leo kisiasa? je! nawe ungependa kuelekea huko?

Dada Cristina! Binafsi nimejifunza kutokana na historia.Kuna baadhi ya mambo katika siasa, hata uwe na nia nzuri kiasi gani, hauwezi kufanikisha mwenyewe kama wenzako hawaungi mkono kile unachokitetea kwa dhati yake naili upate watu wanaofikiri katika utaratibu fulani, unatakiwa kuanzia mbali.Mambo ya namna hiyo yanahitaji mpango madhubuti kweli kweli ili kuweza kufanikiwa zaidi ya kuongea simple tu bungeni mbele ya watu wanaoona hoja yako kama kituko moyoni wakipiga makofi mezani.

Dada lissu Christina; Suala la posho zisizo za lazima, Mashangingi na mambo mengine kama hayo, ni suala linalowachukiza wananchi wengi ila kwa bahati mbaya suala hilo ni pana zaidi ya CCM na serikali hii unayoiona.Hivi wakati unatoa hoja yako, uliangalia ni nani yu nyuma yako,kushoto kwako na kulia kwako?.Nikuulize tu kaswali ka kizushi; Hivi mfano waziri wakati anajibu akaamua kusema "Sasa seerikali itanunua Landrover tu, hakuna mchezo hapa!" hivi ni kina nani watakaopitisha hilo? Tehe! nakutania tu dada yangu Christina! lakini hivi unadhani tatizo ni waziri?

Dada Cristina, nakushauri; kama mambo haya yanakukera kweli kwa dhati ya moyo wako kama ambavyo nimeamini, basi mambo haya yanataka mkakati zaidi ya kuchangia bungeni.Tutafakari pamoja.Je! ni mkakati wa siri au wa wazi! tehe! tehe! tehe!. Any way ambacho nina uhakika nacho ni kwamba unahitajika mkakati.

Yaani wanadamu bwana, sasa huyu kamfanya je mwenzake?

View attachment 162559
​

rubbish
 
Mi nina wasiwasi na ubongo wako, utakuwa kiazi hebu jichunguze vizuri. Mbowe aligomea gari siyo atembee kwa miguu bali abadilishiwe gari, serikali ya ccm waligoma hivyo akalazimika kulitumia. Posho waligomea lakini kanuni za bunge zinawalazimisha wazichukuwe. Nasema akili yako ni ndogo kwa sababu Mbowe kutembelea kutotumia shangingi kusingepunguza gharama kwa serikali maana yeye ni mmoja kati ya mamia ya viongozi wa serikali. Pia alifikiri vyema kwamba gharama za serikali haziwez kupunguzwa kwa njia hiyo ila kwa kuung'oa mfumo mzima fisadi wa ccm na serikali yake ili kuweza kubadili sera, sheria na kanununi zinazochangia matumizi makubwa yasiyo na tija. Pili nimekufananisha na kiazi kwa sababu Mbowe kutumia shangingi hakuondowi hoja ya matumizi makubwa serikalini. Hivyo unapopinga hoja acha kutumia watu tumia hoja. Hoja ya mbunge ilikuwa shangingi moja ni sawa na dispensary hivyo ni gharama kubwa kwa serikali yenye ufinyu wa bajeti.Pia two wrongs can not make right. Siku nyingine fikiri kabla ya kuandika maana wanasoma wenye akili jipime mwenyewe kwa ----- huu wa kutaka hoja ya msingi iachwe kwa sababu tu haikufanikiwa awali ni kukosa akili kulikopindukia. JENGA HOJA ACHA MAJUNGU NA KUHALALISHA UOVU KWA MIFANO
 
Back
Top Bottom