Nadhani kwa mbaali mleta uzi alikua anataka kumsifia mbunge wa mahakama, anyway binafsi kama msimamo wangu, sioni tatizo lolote kwa kiongozi mkubwa kama waziri, rais, spika wa bunge kutumia magari hayo ya bei mbaya (kwa issue ya security n.k) lakini haniingi akilia kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi sijui mhasibu wa wilaya etc kua na magari ya jinsi hiyo, kweli hilo ni ufujaji wa pesa za uma pasipo sababu ya msingi. Nimewhi kwenda wilaya fulani ambayo kwasasa ni miongoni mwa mikoa mipya, kitu kilichonishangaza and of course nashangaa hadi leo ni hiki, muda mfupi tu wa wilaya hiyo kua mkoa nimekutana na mashangingi ya ukweli na yote mapya, nilicho jiuliza ni hiki, kama mkoa huo tu ulipewa shangingi zaidi ya 10, unazungumzia Tsh2.0Bilion so pesa za siasa zinapatikana kirahisi sana, mbona za maendeleo hua tunaambiwa jamani kasungura ketu bado kadogo? Kumbe ndio maana haitakuja kutokea eti pesa za posho za wabunge kua hakuna.
Kwenye ile issue ya mbunge 1 kutochukua posho, ningempongeza sana kama kweli angekua mwadilifu kweli kweli, lakini si ni mbunge huyo huyo ambaye maisha yake mtaani hayatafsiri kabisa kile kipato chake halali? Uwe na magari kadhaa, unao mkpo wa serikali, nyumba ya kupanga ya NSSF na unalo Nissani Safari la kukodi toka kwa Nimrod Mkono, guys kwa kipato kipi? Ninachokijua, mbunge kama hachukui posho, net pay yake haiwezi zidi Tsh 4M, kwa kipato hicho, je inawezeka kua na style hiyo ya maisha? Miongoni mwa wapinzani wakubwa wa kufutwa kwa posho za vikao ni wabunge wa ccm, kwa CHADEMA yupo yule mbunge wa Kisukuma but rafudhi ya Ki-visiwani, kitu cha ajabu sana rafiki wa karibu sana wa mbunge huyu asiyechukua posho, hao ndio rafiki zake, mkuu huwezi kusoma lakini hta picha tu huwezi kuitafsiri!!!?