Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Kuna nyepesi zinasema Serikali ilitenga katika bajeti yake karibu Tshs Billion48 kwa ajili ya mikopo kwa watumishi wa Serikali ili waweze kununua vitu kama Magari, Samani za ndani na Matengenezo ya magari. Inasemekana katika kiasi hicho ni zaidi ya Billion32 karibu 70% zimekopeshwa kwa wabunge tuu, kiasi kinacho baki yaani chini ya 30% ndicho kitakachokopeshwa kwa watumishi woote serikalini nchi nzima. na mbaya zaidi inasemekana kiasi cha 90,000,000 alichokopeswa kila mbunge kwa wabunge karibu 360, yaani 360x90,000,000=32.4Bn ni nusu tuu ndo mbunge anatakiwa kuirudisha kama mkopo, inayobaki atalipiwa na serikali.
Swali linakuja, kama haya ni ya kweli ni kwanini wabunge wamepewa kipaumbele kiasi hiki?
Swali linakuja, kama haya ni ya kweli ni kwanini wabunge wamepewa kipaumbele kiasi hiki?