Masikini watani: Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Urambo ajiunga CCM, asema CHADEMA imeuzwa kwa mafisadi

watakao bakia chadema ni wenye mihemko ya kisiasa na si vinginevyo, kwa sababu ukweli wanaujua lakini wana kumbatia uchafu, wenye akili timamu wanazidi kuondoka.hongereni mnaotoka huko si mahala salama
 
Sasa ametoka ACT au CHADEMA. Maana taarifa za awali zinaonesha alijiunga na ACT baada ya kutoka CHADEMA.
 
Mtaji wa wana siasa ni umaskini wa watz ... hivi kweli urambo mnakubali muongozwe na familia moja miaka nenda rudi na hali umaskini ukizidi? duuuu
 
watakao bakia chadema ni wenye mihemko ya kisiasa na si vinginevyo, kwa sababu ukweli wanaujua lakini wana kumbatia uchafu, wenye akili timamu wanazidi kuondoka.hongereni mnaotoka huko si mahala salama

Posts count : 83

Other : member

🆔 za namna hii ni za msimu

Ninaamini hata tukikuuliza umemaanisha nini utaishia kubabaika tuu
 
Kila mtu anajua jinsi watu wa Urambo na maeneo mengi ya Tabora walivyopofushwa macho ya kiakili. We fikiria Sita anamwachia mkewe agombee ubunge jimbo ambalo hakufanya lolote la maana na bado watu wanampa kura. Watu wa namna hiyo utawaitaje?
 
Kwani huyo katibu ndo anapiga kura??hata waondoke viongozi wote wa ukawa wananchi tutafanya maamuzi ya mabadilko
 
Hakika BUNDI ametua na kujenga kiota katika nyumba ya jirani, kama ni mkosi basi huu ni Babu kubwa..Katibu Mwingine wa Wilaya akihama CHADEMA na kujiunga na CCM wilayani Urambo.

Katika hali isiyo ya kawaida Katibu wa Wilaya ya Urambo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu Obedi Malola amekihama Chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akisema "UKWELI" mchungu juu ya kile kinachoendelea ndani ya Chadema.

Katibu huyo wa Wilaya - CDM (aliyehama) ameeleza sababu zilizomuhamisha CHADEMA kuwa;
1. CHADEMA imeacha misingi yake ya kutetea wanyonge na masikini wa nchi hii, na badala yake imeanza kutetea na kusafisha wezi, wanyonyaji na walanguzi wa nchi hii.

2. Amesema ameshindwa kumvumilia MBOWE aliyeamua kuiuza CHADEMA kwa mafisadi, yeye si sehemu ya wizi wa nchi hii, hayuko tayari kusafisha na kutetea wezi na wala rushwa.

3. Amesema CHADEMA inapokea ruzuku milioni 334, lakini ofisi ya CHADEMA ya wilaya hiyo inadaiwa pango na kwamba wametupiwa vifaa vya ofisi nje.

4. Pia, amesema CHADEMA wapo watu wema, lakini kwa woga wameamua kukaa kimya wakati MBOWE akikipoteza chama hicho, yeye haogopi na kwamba anajua kwa HAKI na UKWELI kuwa MAGUFULI atakuwa Rais bora wa nchi hii..ameiona kazi yake na anaamini ni CHAGUO SAHIHI.

Amtaka MAGUFULI akishaapishwa, baada ya kumaliza Hotuba yake bungeni apitishe na muswada wa kuanzisha mahakama ya wezi na mafisadi ili kabla mwaka huu haujaisha Wezi na mafisadi wawe wameshapelekwa jela;

NB:
Hii hapa VIDEO kamili ya alichokiongea Katibu Huyo mbele ya Umati wa wananchi wa Urambo.

Dhana ya kupambana hawaijui, ndo maana wanakua wakihangaika. Mpambanaji wakweli, harudi nyuma. Pole yao sisi twasonga mbele.
Niwangapi walirudi na kusaliti mapambano ya uhuru wakati wa Nyerere? Mbona walikuwepo waliona nivema kubaki na wakoloni. Leo tena wapo na njaa zao wanaona niheli kuendelea kunyanyasika na ccm, kuliko kupata ukombozi wa kweli.
 
Last edited by a moderator:
Sasa anasema chadema kilikuwa chama cha kutetea wanyonge na sasa kimebadilika je CCM ndio kimekuwa cha kutetea wanyonge? Kweli shikamoo Njaa
 
Juliana Shonza Mbona wewe ulinunuliwa na CCM??

ni sababu ipi iliyokufanya ukafukuzwa CHADEMA kama siyo baada ya kununuliwa??

Leo hii umepewa kazi ya kupiga propaganda ndani ya mitandao. hakika ungejua jinsi unavyojidharirisha kwa jamii wala usingetoa mada yoyote katika mitandao. Na ndio maana Thread yako ukiweka hapa watu wanakushambulia sana.

Mimi binafsi sikushangai sana, najua si kosa lako, sababu ya wewe kuwa hivyo ni hii hapa chini:-

Last edited by a moderator:
Mmetapeliwa tena!Huyu aliondoka CDM siku nyingi akaenda ACT na topic yake ipo humu JF
 
CDM masrahi wamekwisha make tingatinga limeamua hadi kukomba mboga, mmekwisha Chadomo ..hapa kazi tu.
 
Hakika BUNDI ametua na kujenga kiota katika nyumba ya jirani, kama ni mkosi basi huu ni Babu kubwa..Katibu Mwingine wa Wilaya akihama CHADEMA na kujiunga na CCM wilayani Urambo.

Katika hali isiyo ya kawaida Katibu wa Wilaya ya Urambo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu Obedi Malola amekihama Chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akisema "UKWELI" mchungu juu ya kile kinachoendelea ndani ya Chadema.

Katibu huyo wa Wilaya - CDM (aliyehama) ameeleza sababu zilizomuhamisha CHADEMA kuwa;
1. CHADEMA imeacha misingi yake ya kutetea wanyonge na masikini wa nchi hii, na badala yake imeanza kutetea na kusafisha wezi, wanyonyaji na walanguzi wa nchi hii.

2. Amesema ameshindwa kumvumilia MBOWE aliyeamua kuiuza CHADEMA kwa mafisadi, yeye si sehemu ya wizi wa nchi hii, hayuko tayari kusafisha na kutetea wezi na wala rushwa.

3. Amesema CHADEMA inapokea ruzuku milioni 334, lakini ofisi ya CHADEMA ya wilaya hiyo inadaiwa pango na kwamba wametupiwa vifaa vya ofisi nje.

4. Pia, amesema CHADEMA wapo watu wema, lakini kwa woga wameamua kukaa kimya wakati MBOWE akikipoteza chama hicho, yeye haogopi na kwamba anajua kwa HAKI na UKWELI kuwa MAGUFULI atakuwa Rais bora wa nchi hii..ameiona kazi yake na anaamini ni CHAGUO SAHIHI.

Amtaka MAGUFULI akishaapishwa, baada ya kumaliza Hotuba yake bungeni apitishe na muswada wa kuanzisha mahakama ya wezi na mafisadi ili kabla mwaka huu haujaisha Wezi na mafisadi wawe wameshapelekwa jela;

NB:
Hii hapa VIDEO kamili ya alichokiongea Katibu Huyo mbele ya Umati wa wananchi wa Urambo.

Badala ya kueleza na kutuelimisha kuhusu ILANI yenu ya toka mwaka 1995,mko busy na CHADEMA mwaka huu yetu macho

Unaona sasa ulivyopata aibu kumbe ni mwanachama wa ACT kwa Zitto,ungemwambia Zitto,katibu wake amehamia chama cha Mchwa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom