Masikini wanachama wa CCM, mitaani wanazidi kupungua sana sana.

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Si zamani sana ilikuwa kila kona unaona bendera ya CCM inapepea na wanachama wa Chama hiki Cha CCM wametapakaa na utawajua kwa mashati yao yenye nembo za CCM na wavaa khanga nao umanjano na kijani.

Sasa kuvaa nguo ya CCM ukatembea nayo mtaani ni shida na kumuona mtu kuvaa sare zao kama zamani wakitangatanga ,huwaoni wamekuwa adimu sana ,Huwaga najiuliza chama kimepata ugonjwa gani mbona wanachama wanapukutika ,inafahamika Pemba hakuna wanachama wa CCM ,je hali hio ndio imeanza kuhamia huku kwetu Tanganyika ?

Wananchi wanazidi kuelewa kuwa CCM kimepoteza sifa ya kuwa Chama Cha Siasa ,kwa sasa ni mkusanyiko wa magenge chini ya mwevuli wa CCM.
 
Back
Top Bottom