Masikini Nape! CCM hawamwitaji tena Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masikini Nape! CCM hawamwitaji tena Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Sep 17, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kutoka Gazeti la MwanaHALISI - Sept 14, 2011


  NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa hali si shwari tena. Wanaojiita waasisi wa "mpango wa chama wa kujivua gamba" wameanza kutuhumiana kukivuruga chama, imefahamika. Taarifa zinasema mlengwa mkuu wa kinachoitwa, "kukivuruga chama" ni Nape Nnauye, katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi.

  Hatua ya Mukama inatokana na uamuzi wa CCM kumpigia magoti Rostam Aziz, mmoja wa watuhumiwa watatu wa ufisadi wanaotakiwa kujiondoa ndani ya chama hicho. Wengine wanaotakiwa kuondoka ni Edward Lowassa na Andrew Chenge.

  Kwa mujibu wa waliokaribu na Nape, safari ya kiongozi huyo mjini Igunga ililenga kuwatambia baadhi ya wapinzani wake wa kisiasa waliodai Rais Kikwete amempiga marufuku kukanyaga huko wakati huu wa kampeni.

  Kuthibitisha madai hayo, Nape aliandika katika mtandao wa JamiiForum, mara baada ya tukio hilo la Igunga, "Mlisema chama kimempiga marufuku Nape kukanyaga Igunga, nikasema tusubiri. Leo, mmeona nilivyotinga Igunga…"

  Kwa mujibu wa mashuhuda, mara baada ya Nape kutoka nyumbani kwa wazazi wa Peter Ezekiel, alikwenda moja kwa moja kwenye baa maarufu iitwayo The Peak, ambapo inadaiwa alinisurika kichapo kutoka kwa mmoja wa mabaunsa wa CCM.

  Inadaiwa kijana huyo wa miraba minne aliyefahamika kwa jina moja la Shaban, ambaye inadaiwa ni kutoka kwa kundi la Rostam Aziz, mara baada ya kumuona Nape kwenye baa hiyo alifoka, "Wewe unatafuta nini hapa?"

  Naye Nape akajibu, "Wewe unafahamu unaongea na nani?" Shaban akajibu, "Ndiyo. Nafahamu kwamba wewe ni Nape Nnauye."

  Kauli hiyo ilianza kumfanya Nape anyong'onyee kidogo, lakini mtoa taarifa anasema alijipa nguvu na kusema, "…Nimekuja kikazi. Tupishe tunamazungumzo yetu."

  Shaban aligoma kuondoka na kisha akasema, "…Ondoka hapa, vinginevyo tutakuonyesha. Umekuja kutuharibia uchaguzi siyo?"

  Mara baada ya kauli hiyo, taarifa zinasema Nape aliondoka katika eneo hilo na kuingia kwenye gari lake haraka kuelekea Singida.

  Alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Igunga kwa nini anadhani amefanyiwa vurugu, Nape alisema, "Hakuna kitu. Nilikuwa napita njia tu."

  Sokomoko hilo lilitinga hadi kwa viongozi wake wakuu wa chama, Mukama na Rais Kikwete. Inadaiwa mara baada ya kupata taarifa hizo, Mukama kwa hasira alihoji, "Nape kwa nini umekwenda Igunga?"

  Alisema, "Umekatazwa na Kamati Kuu usiende Igunga, sasa mbona umekwenda?" Alipojaribu kujitetea kwamba alikwenda huko kuhani, Mukama alisema, "Nani amekutuma? Nani amekuruhusu? Kijana, tafadhali usituharibie uchaguzi," Mukama anaripotiwa kufoka.

  Kaazi kweli kweli..................
   
 2. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanini wasingempa kichapo uyo mjinga siasa hawezi anaganga njaa 2 kwa kuleta siasa za kibaguzi.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtu yeyote mwenye akili zake timamu Igunga akikipigia kura CCM hata baada ya kudhalilishwa kiasi cha KULALA NA MKE WAO WA NDOA hadharani, basi ni vema akaanza kujilaumu tu mwenyewe mapema maana watakachofanyiwa mara baada ya uchaguzi huo utakua hausemeki tena midomoni.

  Chaguo ni lenu; kuwaenzi Vibaka na Wapiga Ramli au kutumia fursa hii kujikomboa wenyewe ki-uongozi hapo Igunga.
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Nnauye Jr uko wapi ujibu hoja.
   
 5. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aibu kwake hawezi kuja kujibu hoja hiyo maana anatakiwa azungumzie na Mcheba alieenda kubaka watu huko Igunga vijana wake watamshughulikia au ndo imetoka.
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na hasira angalia sinema ya "kuvua gamba" utafurahi tu. Tatizo hata star wake hajulikani, nani atakufa nani atapona, no one knows.
   
 7. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli Nape ni Kilaza, alitumiwa akatumika sasa wanamwona kama mbwa. Hawezi onyesha hadharani jinsi alivyonyong'onyea lakini anaumia sana moyoni. Anajifanya kupokea kadi za wanachama wa vyama vya upinzani ila soon ataomba kuhifadhiwa Chadema.

  Yaliyokuwa yanasemwa kwamba wao na Sitta wana mpango wa kuidhohofisha CCM kwa manufaa yao binafsi sasa yanamrudi kigeugeu huyu.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Maskini CCM, huna utashi tena! umebaki kuiibia nchi na kujibakiza madarakani kwa nguvu za dola! Ondoka tuachie nchi yetu ikiwa safi!
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimependa maneno yako lakini kwanini husiende kuyaeneza Igunga Mkuu ili ujumbe ufike barabara.
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  Nape tuansubiri tukusikie ka ni ya kweli haya
   
 11. H

  Honey K JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Oldonyo,

  WAGANGA NJAA UNAWAJUA? MAANA HUMU NDANI KILA KITU NAPE ANAGANGA NJAA, KWA TAARIFA SINA NJAA KIASI HICHO, HATA NIKIKAA TU NIKAFANYA KAZI ZANGU MWENYEWE BADO NAWEZA ISHI TENA MAISHA MAZURI PENGINE KULIKO WENGI WANAONIKASHIFU HUMU NA KUDAI NAGANGA NJAA...... NIMEACHIWA URITHI NA MZEE NNAUYE SIO WA PESA BALI ELIMU TENA YAKUTOSHA TU.... SIASA KWANGU NAFANYA KAMA HOBI SI AJIRA HATA KIDOGO...

  MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA....MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU....

  JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA....NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI
   
 12. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mafisadi wako chama gani vile? Ni wale wanaotakiwa kujivua gamba au?
   
 13. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  inaelekea mukama alikuwa hamjui vizuri kijana wake.

   
 14. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Haijalishi kuwa umeenda Igunga ama haujaenda. Hapa suala ni kwamba, ulizuiliwa kwenda Igunga na lile gamba kuu ccm ndo walilipigia magoti! Mbona unakwepa hoja wewe??? Unajisifu na vita dhidi ya mafisadi mbona ndo kwanza yanatamba ndani ya chama chako na wakati zile siku 90 zimeshaisha?

  Aibu yako we mwenyewe Nnauye jr kwa kuamua kuuza utu wako kwa magamba!
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  - C'moon bro for the last ten years unaweza kutuambia ulikuwa unafanya kazi gani zaidi ya siasa??????? - Huo mstari wa kuganga njaa siuungi mkono lakini hili la siasa kutokuwa ajira yako nadhani unatuongopea

  Not everyone who challenges u au CCM ni magwanda, kifupi it's pple against CCM

  Habari ya Nape kukatazwa kwenda Igunga iliandikwa kwenye magazeti chanzo kikiwa hukohuko kwenye NEC/CC ya CCM.
  Mkuu usiwasingizie JF hii imetolewa na MwanaHalisi, gazeti ambalo uko in records kuliita la udaku na kwamba hakuna mtu serious analisoma.

  - Sasa hiyo ungemwambia huyo baunsa wakati ule

  - Ebanae wewe si ndiyo ulisema chama chenu huwa hakipeleki viongozi wa kitaifa kupiga kampeni kama vyama pinzani? Mbona unakula matapishi yako?????

  ...Mkuu kama kweli utaenda Igunga na kuhutubia mikutano ya kampeni ukaonekana kwenye Luninga naahidi $100 kupitia kwa invisible.

  - Duh!!! Mkuu sasa yule fisadi wenu mkuu si ndiye alikuwa hai tebo wakati wa uzinduzi wa kampeni? Kumbuka ile siti ilikuwa ni yako
  - Hawa unaowaita mafisadi na wewe ni mmojawapo wa wakuu wa chama kinachounda serikali mmewachukulia hatua gani????

  Dogo inaonyesha umeshaanza kupoteza focus, maana ule moto wenu wa kujivua gamba nadhani ndiyo umeenda huo. Maana sijamsikia Kiongozi wa CCM yeyote huko Igunga akielezea ni namna gani CCM kilivyo chama bora na kwamba sasa kinajisafisha kwa kuvua magamba. Neno gamba vp nalo ni prohibited Igunga?

  Ya mwisho, ni kaswali kafupi not meant to offend at all, una ID nyingine au zingine zaidi ya hii ya Nnauye Jr humu JF?
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Sep 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nakuonea huruma sana kwa mwenendo wako kwa sababu Marehemu baba yako alikuwa ni mtu mwenye uhakika sana. Nilikutana naye mara nyingi sana miaka ya sabini na themanini kwenye mikutano ya TANU na CCM akiwa na kinanda chake na kusema wapinga mapinduzi wote wageuke kuwa ng'ombe ili wanamapinduzi wawakamue maziwa.

  Ni unfortunate kuwa kweli moto huzaa majivu; kwani umethibistisha tosha kuwa wewe ni majivu yatokanao na moto wa Kanali Nnauye, umegeuka kuwa ng'ombe ili wanapinduzi (na wapinga mapinduzi pia) wapate maziwa!!

  Elimu yako inaonyesha kuwa walakini kiasi fulani.
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  very funny! nape, ungeachana na hii makitu! sasa rostam mlikua mnaangalianaje usoni? dd u have to 'explain' that u were just following instructions ama ilikuwaje?
   
 18. c

  chama JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ushauri binafsi NAPE ACHANA NA SIASA kama ulipata elimu nadhani ni vyema ukaendelea na taaluma yako. Majibu yako yanafanana sana na mwehu aliyepata nafuu.

  Wewe ni katibu mwenezi wa chama tawala moja ya jukumu lako ni kuuza sera za chama chetu ili watanzania hasa vijana warudishe imani kwa chama chetu, wakati mwingine siamini kama ni wewe naona mtu anatumia jina lako kuingia ndani ya forum. Kama ni kweli umesoma basi hukuelewa ulichosoma. Tunategemea kijana kama wewe kusaidia kugeuza mwenendo wa chama chetu lakini wapi umegeuka kama hao wezi na walafi waliomo ndani ya NEC.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nape this post is rubbish, absolutely... utterly rubbish

  How could jibu watu kama uko kanga moko laki si pesa???

  Hao mafisadi ndio wenye jimbo na kwa taarifa yako tu, CCM sasa imekua kama Somalia... ni factions tu!!!! Kwahiyo Igunga sio ya kwako, Igunga na kundi jingine... HALAFU UNAJISIFIA ATI UMEINGIA IGUNGA NA KUTOKA BILA MAFISADI KUJUA KWAHIYO KINAWAUMA... Unanyatia jimbo??? and you still call yourself a leader??

  Get a life Nape... acha siasa kapige piano kanisani Mungu akuokoe

  SHAME ON YOU
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  the boy is a goner............
   
Loading...